Nina mashaka na wanaoitwa wanyonge

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,106
3,523
Habari wanajamvi !

Awali ya yote poleni kwa msiba! Niende moja kwa moja kwenye mada. Wanyonge wana shida tena kubwa sana. Twendeni pamoja taratibu mtajua shida ilipo. Siku moja nikiwa mahali fulani nikasikia mnyonge mmoja anasema ' afadhali sasa tumeanza kuheshimiana.' Kwake yeye kitendo cha watumishi wa umma kutokuongezewa mishahara kwa kipindi cha miaka mitano, yeye alifarijika sana.

Wanyonge wapo wengi sana! Karibu wote hufurahia madhira wayapatao watumishi wa umma au wafanyabiashara waliofanikiwa. Nikamsikia mnyonge mmoja anafurahia kuona wahitimu wa vyuo vikuu wakiishia kuchoma mahindi au kuosha magari baada ya kukosa ajira serikalini au taasisi binafsi.Kwao wao wote tukiwa masikini ndio faraja yao.

Nilikuwepo siku wakazi Wa Ubungo mpaka Mbezi huko wakibomolewa nyumba zao bila fidia yoyote , nikamsikia mnyonge mmoja anasema ' huyo ndio Magu bwana , hana huruma na mafisadi bwana' . Kwake yeye kila mwenye nyumba nzuri ni fisadi.

Wanyonge mahali fulani ni wajinga! Ndio maana wanatumiwa na wanasiasa kama stepping stone. Wanatumika na manabii wa uongo kujitajirisha. Wana fikiria wanaweza kuwa matajiri kwa kuombewa...! Bila kufanya kazi.

Juzi nimeona wanao lia na kuzimia wengi ni hao masikini wavaa kandambili. Sijaona hata waziri mmoja akizimia.

SASA JIULIZE KATI YA WAZIRI NA HAWA WANYONGE NANI ALIMFAHAMU KWA KARIBU RAIS MAGUFULI? wanyonge badilikeni!!
 
Hawa wanyonge ni moja ya kundi la watu wajinga kupitiliza. Uwezo wao wa kufikiri uko chini mpaka inashangaza! Yaani ukimuona mtu anajisifia hadharani eti ni mnyonge, kama upo karibu nae, wewe tandika tu vibao! 👋

Nitakuja kukuwekea dhamana na hata kukulipia kabisa faini mahakamani. Useless people kabisa!! Wamechangia sana hawa sisi Watumishi wa umma kuishi maisha magumu wakishirikiana na Rais wao.
 
Mimi kiukweli huwa sikubaliani kabisa na hii falsafa ya wanaoitwa Wanyonge.

Ni kundi linalotengenezwa na watawala kwa maslahi ya watawala wenyewe.

Mfano, nchi za Africa,Tanzania ikiwemo,tulijengewa na wakoloni fikra na tukaikubali kwamba ni maskini ambao tunatakiwa kusaidiwa.

Hii iliwarahisishia sana kututawala kwa kutupa vimsaada ambavyo,kwa mawazo yetu finyu,tuliona ni msaada mkubwa sana kwetu na tukawa tunawakweza.Mpaka leo fikra hizo mbaya hazijatoweka miongoni mwetu.

Vivyo hivyo, Wanaoitwa Wanyonge wametengenezwa ili wawe mtaji wa wanasiasa kupata mamlaka.

Wanaoitwa wanyonge wakipewa nafuu fulani,hata kama ni haki yao ya msingi,hufurahi na kuwaona watoaji kama Mungu wao.

Kwa hiyo,namaliza kwa kuwataka wote wanaojiona wako kwenye kundi la wanoitwa wanyonge wajitambue na kujiona kuwa sio wanyonge na kama wanapatiwa nafuu yoyote na watawala wafahamu kuwa hiyo ni haki yao sio hisani.

Au ninasena uongo ndugu zangu?
 
Siku zote mwenye shida ndio huumia mtetezi wake anapoaga dunia.

Umeandika sana pumba hapa. Kumbuka tu Machinga, Mama ntilie na Bodaboda jinsi walivyokuwa wanajitanua kwenye hii nchi yao tangu JPM aingie madarakani.

Kumbuka watu walivyo kuwa wana furahia usalama wa nchi yao. Mabasi kutembea usiku na mchana.

Pengine wewe pia ni mnyonge ila hujijui, siku ukijijua utaona namna JPM alivyo kugusa pengine kwenye miradi mbalimbali.

Rest easy our Hero.
 
Siku zote mwenye shida ndio huumia mtetezi wake anapoaga dunia.

Umeandika sana pumba hapa. Kumbuka tu Machinga, Mama ntilie na Bodaboda jinsi walivyokuwa wanajitanua kwenye hii nchi yao tangu JPM aingie madarakani.

Kumbuka watu walivyo kuwa wana furahia usalama wa nchi yao. Mabasi kutembea usiku na mchana.

Pengine wewe pia ni mnyonge ila hujijui, siku ukijijua utaona namna JPM alivyo kugusa pengine kwenye miradi mbalimbali.

Rest easy our Hero.
Unateseka ukiwa wapi?
 
Back
Top Bottom