Mimi kiukweli huwa sikubaliani kabisa na hii falsafa ya wanaoitwa Wanyonge.
Ni kundi linalotengenezwa na watawala kwa maslahi ya watawala wenyewe.
Mfano, nchi za Africa,Tanzania ikiwemo,tulijengewa na wakoloni fikra na tukaikubali kwamba ni maskini ambao tunatakiwa kusaidiwa.
Hii iliwarahisishia sana kututawala kwa kutupa vimsaada ambavyo,kwa mawazo yetu finyu,tuliona ni msaada mkubwa sana kwetu na tukawa tunawakweza.Mpaka leo fikra hizo mbaya hazijatoweka miongoni mwetu.
Vivyo hivyo, Wanaoitwa Wanyonge wametengenezwa ili wawe mtaji wa wanasiasa kupata mamlaka.
Wanaoitwa wanyonge wakipewa nafuu fulani,hata kama ni haki yao ya msingi,hufurahi na kuwaona watoaji kama Mungu wao.
Kwa hiyo,namaliza kwa kuwataka wote wanaojiona wako kwenye kundi la wanoitwa wanyonge wajitambue na kujiona kuwa sio wanyonge na kama wanapatiwa nafuu yoyote na watawala wafahamu kuwa hiyo ni haki yao sio hisani.
Au ninasena uongo ndugu zangu?