Nina mashaka na wanaoitwa wanyonge

Nina mashaka na wanaoitwa wanyonge

Sifa kubwa ya 'wanyonge' ni watu wasiojielewa.. wanajua shida ni kiungo mojawapo kwenye mwili. Hawajui nini kinatakiwa au kilitakiwa kufanyika, hawajui kazi ya watawala wao ni nini.

Ndio maana Marekani walitilia shaka uwezo wa 'wanyonge' kuchagua kiongozi wa nchi, wakaamua watu wachache wenye busara(electoral college) ndio wachague Rais!
wanyonge ndiyo siraha ya wana siasa uchwara.make ndiyo hivo watu wasiotaka kufanya kazi wazembe.wezi wanapenda kujiita.
Hao wanaojiona wanyonge wanatumiwa tu!!!

Hata chato inatumiwa tu.hkn mtu asiyependa ufisadi.hata malaika wote mafisadi. Mbinguni wataenda mafisadi, ole wako ulete habari za ulala hoi mbinguni adhabu mara mbili!!!! Fisadi number moja Mungu mwenyewe.Anasena Dunia na vyote vilivyomo.......saa si fisadi?

Ndo maana amekufa ni kinyume na maagizo ya Mungu!! Tulio wa Mungu sisi ni mafisadi kufuru si Mungu katupatia??

Ukiwa mlala hoi mbinguni huendi unaenda chafua tu vyoo vya kule.utanukishia majasho malaika wasafi.

kwa Mungu ni kusafi.ukienda kule utapewa mali kulingana ma utaalam mfano dreva wa ndege unapewa unaendesha yako..


Shetani alitaka Huo ufisadi akakosa ufisadi.sasa anataka walala hoi wenzake.na amewapata wengi mwingine huyu. Lkn mjiulize

Jitu lina midege jizi korofi.uaji .choyo.chuki.ubaguzi.linapiga cha juu. kinyongo kisichoisha bado litetee et wanyonge?? mbuurrlaaa!!
 
The hoi polloi, lumpenproletariat, na sasa wanyonge.

Ukisikia majina haya wanapewa watu ujue wanaandaliwa kudanganywa na kudharauliwa au vyote huku wakipakwa mafuta kwa mgongo wa chupa ili waendelee kuwa wafuasi.

Kwa maneno mengine wanaandaliwa kuwa tabaka la chini kabisa katika jamii.

Na wakishadanganyika ni vigumu sana kuwatoa huko kwa sababu unyonge ni kama uraibu wa mihadarati. Ukishakubali kuwa mnyonge unafurahia kuendelea kuwa mnyonge na kuwapenda wale wanaoshangilia unyonge wako huku ukiwachukia sana wale wanaojaribu kukutoa kwenye unyonge kwa kukuonesha ukweli.

Kukubali kufanywa mnyonge ni kukubali kufanywa mtumwa.
 
Tokea 2015 graduates tunabangaiza mtaani. Tunaambiwa tujiajiri, lakini wao wameajiriwa na hawataki hata kustaafu. Na waliopo kwenye ajira hawapandishwi ili wapya waingie kwenye system na waliofanikiwa kujiajiri biashara zimekua ngumu sababu mtaani hakuna pesa. RIP

Walishachoka na wanyonge wasioenda shule.

Graduates mnaandaliwa kuwa wanyonge.

Amkeni mkatae unyonge akilini mwenu!
 
Habari wanajamvi !

Awali ya yote poleni kwa msiba! Niende moja kwa moja kwenye mada. Wanyonge wana shida tena kubwa sana. Twendeni pamoja taratibu mtajua shida ilipo. Siku moja nikiwa mahali fulani nikasikia mnyonge mmoja anasema ' afadhali sasa tumeanza kuheshimiana.' Kwake yeye kitendo cha watumishi wa umma kutokuongezewa mishahara kwa kipindi cha miaka mitano, yeye alifarijika sana.

Wanyonge wapo wengi sana! Karibu wote hufurahia madhira wayapatao watumishi wa umma au wafanyabiashara waliofanikiwa. Nikamsikia mnyonge mmoja anafurahia kuona wahitimu wa vyuo vikuu wakiishia kuchoma mahindi au kuosha magari baada ya kukosa ajira serikalini au taasisi binafsi.Kwao wao wote tukiwa masikini ndio faraja yao.

Nilikuwepo siku wakazi Wa Ubungo mpaka Mbezi huko wakibomolewa nyumba zao bila fidia yoyote , nikamsikia mnyonge mmoja anasema ' huyo ndio Magu bwana , hana huruma na mafisadi bwana' . Kwake yeye kila mwenye nyumba nzuri ni fisadi.

Wanyonge mahali fulani ni wajinga! Ndio maana wanatumiwa na wanasiasa kama stepping stone. Wanatumika na manabii wa uongo kujitajirisha. Wana fikiria wanaweza kuwa matajiri kwa kuombewa...! Bila kufanya kazi.

Juzi nimeona wanao lia na kuzimia wengi ni hao masikini wavaa kandambili. Sijaona hata waziri mmoja akizimia.

SASA JIULIZE KATI YA WAZIRI NA HAWA WANYONGE NANI ALIMFAHAMU KWA KARIBU RAIS MAGUFULI? wanyonge badilikeni!!
Wengi wa hao wanaoitwa ama kujiita WANYONGE wana tabia za kichawichawi na husda! Wana kawaida ya kushangilia matatizo ya wengine ili kujisahaulisha yao "wapo walioshangilia Manji kupata misukosuko huku wakiwa waajiriwa wake hii leo wanalia midomo juu kama...." TUTAHESHIMIANA TU
 
Wanyonge ni watu Masikini.
Na umasikini wao wengi wa kupenda au wrong choices.
Wanyonge hao hao wanatumiwa na elites kunyonya na kufurahia madhila ya watu wengine kwa manufaa ya wachache..

Wanyonge ni tool ya kuendelea kutawala.. ukiwasikiliza ukawafanyia yanayokonga nyoyo zao.. watakupa kura.

Wanyonge ni wezi, wazurumaji, matapeli.. na wamejaa kila mahala.. imagine unauza Mikanda kwenye duka unalolipa kodi, na unaleseni ya biashara.. anakuja mtu na mbao za kuokota anagonga gonga mbele ya duka lako anaanza kuuza Mikanda bila kodi ya pango wala EFD mashine.. yeye ana kitambulisho cha mmachinga.. mnyonge huyo.

Biashara zinakufa, wenye majengo ya kukodisha wanakosa wateja, wenye maduka wanalalamika.. ila mnyonge yeye kwake.burdani kabisa...

Unatoa fedha unalipa fidia unanunua shamba.. unapima unamilikishwa... Wanakuja wanyonge wanataka uwapishe kisa wewe wanaona huna kazi nalo.. ndio maana liko wazi... Na serikali sikivu inakunyang'anya inawapa.. walijawa kiburi mno sikuwahi kuona kabla..

Wana sense of intittlement ... Hawajali na ni waharibifu sana. Hawajui haya yote wanayoyakimbilia na kuona wamepata ni very short lived.. na hatima yake inadumaza the entire economy.. wanyonge.

Wanyonge hawakawii kuwa waporaji(looters).

Ingawa wanapenda sana pia kuwa ombaomba(moochers)

Hii ni kwasababu wanaaminishwa sana kwenye uwepo wa vitu vya bure au vitu rahisi rahisi visivyohitaji uwekezaji na matumizi ya akili.
 
Wanyonge hawakawii kuwa waporaji(looters).

Ingawa wanapenda sana pia kuwa ombaomba(moochers)

Hii ni kwasababu wanaaminishwa sana kwenye uwepo wa vitu vya bure au vitu rahisi rahisi visivyohitaji uwekezaji na matumizi ya akili.
Na tuko yodi chache kufikia kwenye looting kama hakutakuwa na immediate serious intervention kutoka kwa serikali na jamii yote.
 
Halafu mambumbumbu sasa
Wanashindwa kufikiria kuwa Raisi anayeupenda ufukara na kujivunia ufukara wa mtu atakuwa ni raisi wa ajabu asiyependa mtu yeyote afanikiwe kimaisha. Magufuli alikuwa anatamani wananchi wote wawe wanyonge (watu wa hali ya chini) hivyo ni ngumu kwa mnyonge kutoboa kuwa tajiri zaidi ya tajiri kufanywa kuwa masikini
 
Back
Top Bottom