hujafafanua ni idara zipi ambazo unataka wakuu wake wawe wanachama wa chadema? mashirika, makampuni, taasisi za umma au?
Mtoa mada kumbuka kuwa ukitoa mawaziri ambao. Ni lazima wawe wabunge kwa ticket ya chama fulani, makatibu wakuu,wakuu wa mikoa na wakuu wa idara mbalimbali hawatakiwi kuwa na itikati za vyama....imekuwa hivyo sbb ya mfumo mbove tulio nao...na kumbuka chini ya serikali ya CDM wakuu wa wilaya watafutwa...so huhitaji kuogopa, tujipange kwa ajili ya kuisuport CDM 2015 maana ndilo tumaini pekee lililobaki
Kaka cjaona hoja hapa! Subir 2takapochukua nchi ndio utaona kama kuna watendaji au hakuna na ucpende kuishi kwa hisia
Umenena vyema mkuu, ukiwa na Rais makini, Makamu wake makini, Waziri mkuu makini, Mawaziri makini na wachapakazi, kinachofuata ni kuweka utawala bora katika mikoa, wilaya na hata vijiji.
Wanaosikika Chadema ni wachache lakini ndani ya Chadema kuna hazina kubwa sana ya viongozi bora, pia kuna wanachama na nje ya chama lakini kuna watu wenye mapenzi mema na nchi hii.
Mfumo uliopo ndio unaoharibu nchi kukumbatia kwamba kila kiongozi lazima atoke ccm, hata kama kuna kiongozi mzuri kwa nafasi ya uwaziri laki hatoki ccm basi hapewi, who knows bwana kama Chadema ikikamata nchi inawezekana akina magufuli wakarudishwa kwenye uwaziri na wakajirekebisha walipo jikwaa na kuwatumikia watanzania, so hofu ondoa ndugu.
Hii thread Kivuli na ina mawazo kivuli, ngoja wananchi vivuli wachangie mawazo vivuli.
Nadhani kosa lako ni kuangalia mfumo wa uongozi wa CCM na kutaka CHADEMA nayo iufuate huo huo. Mfumo wa CCM una ukiritimba mkubwa sana ambao pamoja na mambo mengine umejengwa kwenye msingi wa uswahiba. Hivyo rais anafungua nafasi nyingi za uongozi ili azigawe kwa maswahiba wake.Tunapozungumzia haya ni Chadema kitatoa watendaji wote wakuu na muhimu pindi kitakaposhika madaraka ya nchi.
Yaani kuanzia
- mawaziri
- makatibu,
- wizara,
- Mabalozi
- wakuu wa idara mbalimbali,
- mahakimu,
- wakuu wa mikoa na wilaya.
na wengineo wengi kwa ukubwa wa serikali yetu, tokea wizara, kanda mikoa hadi wilaya.
Revolutionar
Wajua kuwa hao wote unaosema ni watendaji katika serikali na jua kitu kimoja serikali sio CCM au CDM tu serikali ni yawote na wale walioko sasa wanaweza endelea wako wengi wenye uchungu na nchi hii. ila wafanyeje wakati wanapelekwa ila siku utakapo sikia CDM imeshika dola utajua kuwa CDM wako wengi na wengio walikuwa wanataka mabadiliko kaka. usijali ni sehemu ya mipango na hakika kila kitu kitakuwa sawa
Mimi ni mtanzania niliyeichoka CCM, na siamini kama kwelli watanzania tunataka maendeleo kuichekea CCM iendelee kushika hatamu ya nchi.
Kwa kuwa suala la CCM kuondoka madarakani ni lazima, sasa mbadala wake ni Chadema, chama ambacho kinaonesha matumaini makubwa kwa watanzania, chama kinachofumua mengi ambayo watanzania tulikuwa tumefumbwa macho na kutawaliwa kama mazezeta huku tukiambiwa nchi yetu ni maskini.
Bila shaka nina imani kubwa na Chadema katika kuikomboa nchi hii, na sina shaka kama si 2015 basi very soon Chadema kitachukua uongozi wa juu kabisa wa nchi , yaani uraisi na kuongoza nchi.
Tunapozungumzia haya ni Chadema kitatoa watendaji wote wakuu na muhimu pindi kitakaposhika madaraka ya nchi.
Yaani kuanzia
- mawaziri
- makatibu,
- wizara,
- Mabalozi
- wakuu wa idara mbalimbali,
- mahakimu,
- wakuu wa mikoa na wilaya.
na wengineo wengi kwa ukubwa wa serikali yetu, tokea wizara, kanda mikoa hadi wilaya.
Suala ambalo hula linanijia kichwani mara kwa mara ni KUPWAYA kwa Chadema katika kusimamisha serikari hiyo. Na kwa kuwa mimi hufikiria mbele zaidi na napenda sana kuwa realistic huwa naichukua Chadema namna hii na naitapanya katika serikali kwa ukubwa wake, kwa kweli naona inapwaya, Haswa ukuzingatia kwamba chama hakijajikita katika katika kurecruit wanachama katika ngazi zote za ukubwa wa nchi.
Chadema kinapwaya si kwa sababu hakina viongozi na wanachama makini na wachapakazi la hasha, Chama kina watu makini, (Kuanzia, Dr Slaa, Mbowe, Tundu Lisu, Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika, Godbless Lema na wengineo wengi) la hasha bali viongozi hawa makini na wenye uwezo mkubwa hawatoshi kufit katika nyadhifa na idara zote na kutengeneza serikali yenye ufanisi na kasi moja. kimsingi kwa idadi yao wanapwaya.
Ukichukulia mfano tu ile kambi ya upinzani bungeni, inayoongozwa na Mbowe, mgawanyo wamawaziri kivuli katika wizara kivuli hizo ambao ndio unatoa picha ya nani atashika nafasi gani kama Chadema itashika madaraka, waliochaguliwa utagundua kabisa kuwa Chadema hakuna NGUVU KAZI YA KUTOSHA. Kuna wengi ambao ni makini lakini sio 'the best' we can get kwa ajili ya kusimamia maendeleo ya taifa kwa ukubwa wake.
Wako wanaoweza kuwa mawaziri na viongozi makini sehemu mbali mbali serikalini, kama Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Mnyika kiasi, Mbowe, Mdee kiasi........kimsingi hata ninavyoitaja hii list unaona kabisa kwamba tunarun out of options.....nguvu kazi inayohitajika haitoshi. Iitakapokuja katika suala la kuteua Nguvu Kazi kwa ajili ya nyadhifa zote kwa ukubwa wake, naona Chadema inapwaya. Labda waje kutumia kujuana, kitu ambacho hakitaleta tija katika maendeleo (najua Chadema haitafanya hivyo).
Nadhani, Suala la kurecruit wanachama wapya linahitajika kufanyika, tena kila sehemu hadi vijijini, Chama kirecruit wachapakazi, wanachama makini, kitoe mafunzo na warsha mbalimbali ili kuinspire vijana wengi zaidi na kupata nguvu ya kutosha kuendesha nchi wakati utakapofikia. Bila hivyo kwa kweli naona Chadema kinapwaya jamani, hebu nyie wenyewe semeni.
Whaaat?...hivi ndivyo unavyofikiria eeeh!
Licha ya kutokuwa na watu wa kuongoza , CHADEMA a.k.a. MAGWANDA watakuwa wanaiona nchi hii kama uchi wa mtoto. Kwani mtoto akiwa uchi utakuwa wamtizama tu na huna la kufanya
Nakubaliana na wewe, lakini je hiyo inamaanisha Chadema mtachagua watu waliopo sasa katika nyadhifa au, hao watu Chadema itakao chagua watatoka wapi? ni akina nani? nataka tufikirie hivyo!
Sikatai Chadema ina hadhina kubwa, hazina ipi hiyo? hebu kuwa straight to the point! çause najua Chadema bado haijaexploit hazina kubwa sana. Hao wanaosikika wenyewe hawatoshi, hebu angalia serikalini kuna Nyadhifa ngapi halafu, hao unaowaita wanasikika wapange wote utaona kama wanajaa hawajaii?
2. Rais makini kama Dr. W.Slaa mwenye kutenda kama asemavyo (Walk the talk)
.
alishinda ila mzee wa kaya alichakachua tunalijua hilo hata makame shahidi
Hilo halina ubishi ndio maana yeye hivi sasa ni rais kivuli