Nina mashaka na uwezo wa CHADEMA kuongoza SERIKALI 2015

Ndugu Revolutionery,
Usipate taabu...wapo watanzania wengi tu wakuendesha nchi hii...wakiwemo ambao bado wako katika serikali hii....hii ni hofu ya wengi kuwa kubadili serikali maana yake mpaka Polisi wote wafukuzwe...la khasha...hata Mandela alipochukua nchi ni polisi walewale waliokuwa wakiwasumbua ndio wako hata leo...watakaoenda na maji ni hawa unaowasikia wakipiga mayowe....RC,DC,Mawaziri(baadhi watabaki)
 
La kwamba nina upeo mdogo katika mifumo ya uongozi, ni mtazamo wako sikukatazi, na yawezekana una upeo mdogo sana kiasi kwamba huna uwezo wa kupata concept ya nilichoelezea hapa.

Unazungumzia Malecturers ni Chadema so what? 90% kivipi? a huo upeo ulionao ndio unakwambia huko tuendako mawaziri hawatatokana na wabunge? what are you refering to? katiba mpya? ambayo hata mchakato haujaanza, au? I am a realist, ndio tofauti yetu! I think in terms of how things work out, best and worst case scenarios, envision possible difficulties and opportunities and that is when I came up with this article.

Sie ni Tanzania, ya Bingu wa Mutharika yepi, unajua alifikaje hapo? tunajifunza nini, difficulties, opportunutues ni zipi?

Sugu ni mfano tu, atleast unaacknowledge kwamba waliopo bado hajitoshelezi!

Unaposema Serikali makini siku zote itawaacha wanasiasa wapige porojo za kisiasa na wataalam ndio watakabidhiwa jukumu la kujenga nchi. Unamaanisha nini? kwa hiyo wakina Mbowe, Slaa, Mnyika, Mdee, Tundu Lisu, Zitto etc watakuwa wanafanya nini?

Ndugu mtoa mada samahani kama nitakukwaza, ila ukweli ni kwamba upeo wako ni mdogo sana katika mifumo ya uongozi, Nilichomuelewa mimi Dr Slaa aliahidi kuunda serikali ndogo isiyozidi mawaziri 20, na ukumbuke huko tuendako mawaziri hawatotokana na wabunge ilo ni moja ya madai makuu ndani ya katiba mpya.
Pale UDSM 90% ya malecture wote ni Chadema, usione watu wako kimya ukadhani CHADEMA ina uhaba wa wasomi, na ukumbuke serikali ijayo haitohitaji uwe mbunge au mwanasiasa kuweza kuitumikia nchi yako.
Nakupa changamoto unijibu Bingu wa Mutharika ameundaje serikali yake? au nieleze mgombea binafsi akiruhusiwa na akishinda ataundaje serikali yake? ndio maana hata Nduka amebeza huu utafiti wako butu.

Serikali makini siku zote itawaacha wanasiasa wapige porojo za kisiasa na wataalam ndio watakabidhiwa jukumu la kujenga nchi. usiwahesabu akina SUGU kwamba ndio serikali ijayo ya CHADEMA, hapana hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe,, asilimia kubwa ya wabunge wa CHADEMA kazi yao kuu itakuwa ni kuisimamia serikali yao na kuiwajibisha pale itakapokwenda kinyume na matarajio ya Watanzania.
 
Asante Sana kwa kusema haya, ndio ninachoona mimi exactly, kwamba ndio wanaweza lakini they need to work on it, hawataki kuelezwa wabishi, I can realy see Chadema's downfall wakichukua madaraka kama wabishi kujifunza na kufanyia kazi kasoro zao, Soma Ilani zao za uchaguzi, ni shallow kabisa, They can do more serious staff.

Wewe umesema vyema I salute!

chadema ni a big mystery than a reality...

nguvu ya chadema inatokana na udhaifu wa ccm,

yaani bila ccm dhaifu na ya kifisadi,chadema haina nguvu

hawana nguvu ya kwamba wana better organisation
au a better vision......

waulize sera zao za viwanda kwa mfano,
utasikia tu, 'tutaimarisha viwanda'

kama vile ccm tu,siasa zaidi kuliko visionaries

na sasa wana tatizo kubwa zaidi kuliko ccm

ni tatizo la kutokukubali kukosolewa na kupingwa..

kuna thread nilianzisha hapa,inaitwa' Chadema wananidissapoint kwa kweli'

ukiona hata majibu ya dr slaa kwenye hiyo thread utashangaa,ni aibu kwa kweli...

juzi tu hapa jenerali ulimwengu kawashauri kile kile nilichoshauri mimi

kwamba watulie na wajipange,majukumu wanayoyaomba ni makubwa mno

but still hawaelewi kabisa
 
Ndugu mtoa mada samahani kama nitakukwaza, ila ukweli ni kwamba upeo wako ni mdogo sana katika mifumo ya uongozi, Nilichomuelewa mimi Dr Slaa aliahidi kuunda serikali ndogo isiyozidi mawaziri 20, na ukumbuke huko tuendako mawaziri hawatotokana na wabunge ilo ni moja ya madai makuu ndani ya katiba mpya.
Pale UDSM 90% ya malecture wote ni Chadema, usione watu wako kimya ukadhani CHADEMA ina uhaba wa wasomi, na ukumbuke serikali ijayo haitohitaji uwe mbunge au mwanasiasa kuweza kuitumikia nchi yako.
Nakupa changamoto unijibu Bingu wa Mutharika ameundaje serikali yake? au nieleze mgombea binafsi akiruhusiwa na akishinda ataundaje serikali yake? ndio maana hata Nduka amebeza huu utafiti wako butu.

Serikali makini siku zote itawaacha wanasiasa wapige porojo za kisiasa na wataalam ndio watakabidhiwa jukumu la kujenga nchi. usiwahesabu akina SUGU kwamba ndio serikali ijayo ya CHADEMA, hapana hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe,, asilimia kubwa ya wabunge wa CHADEMA kazi yao kuu itakuwa ni kuisimamia serikali yao na kuiwajibisha pale itakapokwenda kinyume na matarajio ya Watanzania.

Mr upeo wangu mdogo, usiyependa kufikiri soma na haya hapa chini abda yatakusaidia kujua nani upeo wake mdogo katika uongozi

chadema ni a big mystery than a reality...

nguvu ya chadema inatokana na udhaifu wa ccm,

yaani bila ccm dhaifu na ya kifisadi,chadema haina nguvu

hawana nguvu ya kwamba wana better organisation
au a better vision......

waulize sera zao za viwanda kwa mfano,
utasikia tu, 'tutaimarisha viwanda'

kama vile ccm tu,siasa zaidi kuliko visionaries

na sasa wana tatizo kubwa zaidi kuliko ccm

ni tatizo la kutokukubali kukosolewa na kupingwa..

kuna thread nilianzisha hapa,inaitwa' Chadema wananidissapoint kwa kweli'

ukiona hata majibu ya dr slaa kwenye hiyo thread utashangaa,ni aibu kwa kweli...

juzi tu hapa jenerali ulimwengu kawashauri kile kile nilichoshauri mimi

kwamba watulie na wajipange,majukumu wanayoyaomba ni makubwa mno

but still hawaelewi kabisa
 
Kwanza nikupe pole kwa KUKIVAMIA CHADEMA juu kwa juu nakushauri tafuta Ilani ya Uchaguzi ya Chadema then Utapata Majibu yote pia Kwa Akili ya kawaida Fikiria kwenye Mchakato wa kuwapata Wagombea UBUNGE walijitokeza wanachama wangapi ???vile kwanye Harakati za Kuwania Udiwani pia Kuwania Viti Maaalum na Je unawajua wanaoratibu kazi za Chadema Nje ya hao wabunge uliowataja ikiwa ni Mikoani ,Wilayani na Mitaani???

ACHA FIKRA POTOVU ,,,,,Uoga wako ndyo Umaskini wako.
 
Mh Kwayus,asante, sijaivamia Chadema naifahamu. Ninaifuatilia sana. Niko na watu wa inner circles kabisa. Nakipenda na napenda kifanyie kazi kasoro zake ili kifanye vizuri zaidi. Hata kwa hayo unayoyasema bado Chadema kinahitaji improvement and that's what I'm saying, Chadema is far from being perfect. Hizo ilani za uchaguzi sio tu nazijua nimeshazichambua na kuzijadili pia. Weka hapa (copy paste) ya Uchumi, nikupe mapungu yake, kwanza contradictions kibao tangu itikadi ya Chama, sera nk, Kwanini hamtaki kuadmit na kufanyia kazi, You are just being illogical and naïve.
Kwanza nikupe pole kwa KUKIVAMIA CHADEMA juu kwa juu nakushauri tafuta Ilani ya Uchaguzi ya Chadema then Utapata Majibu yote pia Kwa Akili ya kawaida Fikiria kwenye Mchakato wa kuwapata Wagombea UBUNGE walijitokeza wanachama wangapi ???vile kwanye Harakati za Kuwania Udiwani pia Kuwania Viti Maaalum na Je unawajua wanaoratibu kazi za Chadema Nje ya hao wabunge uliowataja ikiwa ni Mikoani ,Wilayani na Mitaani???ACHA FIKRA POTOVU ,,,,,Uoga wako ndyo Umaskini wako.
 
CCM leo imeachwa mbali sana kimikakati na wapinzani wao Chadema haiwezi tena kushindana kwa wigo wowote ule wa hoja iwe bungeni au nje ya bunge. CCM imeacha majukumu yake na kuikabidhi mizigo serikali iweze kupambana na Chadema. Tunashuhudia matamko ya kisiasa yakitolewa na wakuu wa mikoa badala ya viongozi wa CCM. Juzi mkuu wa mkoa Arusha Magesa Mulongo alisema atahakikisha anapambana na Chadema na viongozi wake ikiwezekana kuwafunga wote jela, jana tumemsikia mkuu wa makoa Mbeya Abbas Kandoro akisema vurugu zilizotokea zinamkono wa kisiasa na viongozi waliohusika atawashughurikia. Ukifuatilia matukio haya utagundua wazi kuwa hawa viongozi wa serikali wanatumika kisiasa na inaonyesha CCM haiwezi tena kushindana na Chadema kwa hiyo leo Chadema inashindana na serikali. Ndio maana nasema Chadema imevuka levo ya kuwa chama sasa inatakiwa ijipange kupambana na serikali ili ichukue dola maana siku hizi ni wazi chama tawala CCM kinaiogopa Chadema.

MSUGUANO kati ya Serikali na Chadema sasa ni bayana kufuatia kauli mbalimbali za viongozi wa Serikali kukosoa hadharani mwenendo na utendaji wa chama hicho kikuu cha upinzania nchini.

Hatua hii imekuja wakati hali tete ya kisiasa ikiendelea kugubika Jiji la Arusha huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiri hadharani kuwa maandamano yanayofanywa na Chadema kwa kaulimbiu ya 'Nguvu ya umma,' yanainyima usingizi serikali.

Mbali na Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulungo, amekuja juu na kudai kuwa harakati zinazoendeshwa sasa na Chadema, hazina nia njema na kwamba ni mkakati wa maksudi kutaka mkoa huo usitawalike.

Wachunguzi wa mambo ya siasa nchini wanatafsiri kauli za viongozi hao kuwa zimefungua ukurasa mpya unaodhihirisha kuwepo msuguano mkubwa na wazi kati ya Serikali na Chadema.

Kwa muda mrefu Chadema imekuwa ikilaumu mambo kadhaa ikiwemo kunyimwa vibali vya maandamano na makada wake kuswekwa rumande na kudai kwamba nyuma ya matukio hayo, kuna mkono wa Serikali.

Mwanzoni mwa wiki hii viongozi wa Chadema akiwamo, Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu walikamatwa kwa kosa la kufanya mkusanyiko bila kibali cha polisi katika Uwanja wa NMC mjini Arusha.

Hata hivyo, hatua hiyo inaonekana kupingwa na baadhi ya viongozi wa dini, wanasiasa na wafanyabiashara mkoani Arusha kwa maelezo kwamba vurugu, vitisho na matumizi ya vyombo vya dola kamwe hayawezi kuleta suluhu ya migogoro ya kisiasa na kushauri kuwepo mazungumzo na majadiliano kati ya makundi husika.

Kauli za viongozi wa dini

Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti jana, Askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Wilaya ya Arusha, Abbas Ramadhani Mkindi ‘Darweshi,' kwa pamoja waliwataka viongozi wa serikali na vyama vya siasa mkoani Arusha, kuacha ubabe, vitisho na kuhasimiana badala yake waonyeshe nia ya kweli kumaliza mgogoro huo.

"Hali ni mbaya Arusha katika nyanja zote. Kisiasa kuna machafuko yanayotuathiri wote, waliomo na tusiokuwemo. Katika matatizo na machafuko haya, huwezi kunyooshea kidole mtu au chama chochote cha siasa, muhimu hivi sasa ni kufanyika majadiliano bila ubaguzi wala kudharauliana ili turejeshe amani mjini mwetu," alishauri Askofu Laizer alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

Askofu huyo, alisema Arusha inahitaji viongozi makini wanaozingatia utawala wa sheria, diplomasia na wenye staha katika kushughulikia changamoto zilizopo, kama mgawanyiko mkubwa wa kiitikadi ulioibuka kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.

Kongozi huyo wa kidini mwenye ushawishi na msimamo usioyumba katika mambo yanayohusu jamii, alisema vitisho vya watawala na matumizi ya vyombo vya dola haviwezi kutatua tatizo la Arusha, bali vinaweza kupooza kwa muda na baadaye mambo hayo yataibuka kwa nguvu na mbinu mpya na kusababisha vurugu zaidi.

Alionya kuwa si busara kupuuza madai ya Chadema na kuwashauri viongozi wa Serikali kuacha kutumia nguvu yadola kutunishiana misuli na chama hicho kwani Arusha inaelekea pabaya na likitokea la kutokea, wote watangamia.

''Lazima busara itumike kwa kusikiliza hoja za pande zote husika bila kubezana.'' Alishauri.

Bila kutaja jina, Askofu Laizer alisema kauli za vitisho zinazotolewa na viongozi wa serikali Arusha, zitachochea harakati za wanaodhani wanaonewa, kutafuta haki na pengine kutumia njia za machafuko zaidi na kuchafua hali ya hewa kuliko livyo sasa.

Askofu Lazier alivishauri vyama vya upinzani kuepusha shari kwa kudai haki zao kwa njia ya amani hata kama wanahisi kuonewa, kama ilivyo kwa Arusha ambapo vijana wa CCM (UVCCM), waliandamana na kufanya mkutano wa hadhara bila kibali cha polisi, lakini Chadema walipojaribu kufanya hivyo, walikamatwa na kushtakiwa kwa kusanyiko lisilo halali.

"Vyama vya upinzani vikwepe pale sunami au upepo mkali unapovuma dhidi yao, wainame kidogo kimbunga kipite halafu waendelee mbele.

"Vitumie wataalamu na wasomi waliojaa ndani ya vyama hivyo kutatua matatizo na migogoro inayojitokeza kwa njia ya amani na utulivu," aliasa Askofu Laizer.

Alisema tatizo linalojitokeza nchini hivi sasa ni vyama vya upinzani kutopewa fursa ya kutekeleza na kuendesha shughuli zao za kisiasa kwa uhuru kama ilivyo kwa CCM. Hata hivyo, alivashauri vyama hivyo kufuata sheria na kanuni katika kudai na kutafuta haki yao .

Kwa upande wake, Mkindi alisema viongozi serikalini wasijidanganye kuwa wanaweza kulinda amani kwa mtutu wa bunduki na kushauri vyama vinavyohasimiana vya CCM na Chadema kukutanishwa ili vijadili na kuondoa tofauti zao ili kurejesha amani na usalama Arusha.

"Arusha imechafuka, hakuna amani. Biashara imekufa, hata mikutano ya kitaifa na kimataifa haifanyiki hapa tena kwa wingi kama ilivyozoeleka. Ufumbuzi ni watu kukaa mezani wazungumze, waadiliane na kutatua tofauti zao.

''Chadema wasidharauliwe hata kidogo kwa sababu wana watu wengi wanaowaunga mkono ambao wako tayari kusikiliza na kutekeleza lolote wanaloambiwa," alisema Mkindi

Msimamo wa RC Arusha

Katika siku za karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mulongo amekaririwa akionya kuwa vyombo vya dola vimejipanga kukabiliana na aliowaita, wavuruga amani na waleta machafuko Arusha, na kuelekeza mashambulizi ya moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na chama chake.

"Nikiwa mhimili na msimamizi wa amani na usalama wa mkoa, sitakubali kushuhudia mtu anavuruga amani tena Arusha. Kibaya zaidi wengi wa wanaoleta vurugu hapa wanatoka nje ya mkoa wetu. Imetosha! Tumechoka," alikaririwa mkuu huyo wa mkoa alipozungumza na viongozi na watendaji wa manispaa ya jiji hilo.

Mwafaka CCM na Chadema

Kwa upande wao, viongozi wa Chadema na CCM waliunga mkono hoja ya kujadilina ili kutafuta muafaka wa mgogoro wa Arusha kwa njia ya majadiliano, huku kila upande ukisisitiza kuaminiana na kuheshimiana huku Chadema wakiwatuhumu viongozi wa serikali mkoani Arusha kuwahukumu bila kuwasikiliza malalamiko na hoja zao.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Mkoa wa Arusha, Ephatah Nanyaro, alisema alisema chama chake kiko tayari kujadiliana na yeyote kuhusu amani na mustakabali wa Arusha na kusisitiza kuwa lazima watawala watambue kuwa hawapigi kelele kwa lengo la kufanya mkoa usitawalike kama inavyodaiwa.

Kwa upande wake, Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Arusha, Semmy Kiondo alisema chama chake kiko tayari wakati wowote kukutana na kujadiliana na mtu, chama au chombo chochote ikiwemo Chadema kutafuta amani na maendeleo ya Arusha lakini akasisitiza hakiko tayari kutishiwa, kunikizwa wala kubezwa kwa namna yoyote.

Source: Mwananchi
 
Umechambua vizuri mkuu, sikuwa nimefikiria from that angle. Ni kweli kabisa tunasikia tu waziri mkuu, RC na Polisi ndo wanajibizana na Mwenyekiti na Katibu mkuu wa CDM. huwasikii akina Msekwa (makamu mwenyekiti wa CCM), Mukama(KM) wala JK kama mweyekiti. Hata Nape siku hizi naona ameshajua CDM ipo ni maji marefu kwake.
 
Hivoo sikujua, kwa hiyo CDM wako juu kimkakati mpaka kuiba kura kuliko ccm?

isitokee uchaguzi fulani hapa CDM wakashindwa, halafu mkasema CCM wameiba kura , wakati KIMKAKATI CDM wako juu ya CCM. Think!
 
CDM hawana lolote zaidi ya fujo na udini. Hawatafika kokote labda waolewe na CCM.
 
Hivoo sikujua, kwa hiyo CDM wako juu kimkakati mpaka kuiba kura kuliko ccm?

isitokee uchaguzi fulani hapa CDM wakashindwa, halafu mkasema CCM wameiba kura , wakati KIMKAKATI CDM wako juu ya CCM. Think!

kwa hyo unahalalisha CCM ni wez...
 
CDM hawana lolote zaidi ya fujo na udini. Hawatafika kokote labda waolewe na CCM.
Ni ajabu kuona serikali nzima inababaishwa na chama kisicho na lolote... kwa maana hiyo serikali nayo haina lolote
 
CDM hawana lolote zaidi ya fujo na udini. Hawatafika kokote labda waolewe na CCM.

eti eh, nani kazima soo la mbeya..?fanyeni mdhaha na propaganda za kijinga bila kujua kuwa watz wameshasanda mbinu zenu za kuwagawa..
 
Chadema kupitia Sugu, ndio alietuliza fujo Mbeya baada serikali na CCM kupitia polise na JWTZ kushindwa, Its true chadema imeibwaga serikali. Go on Chadema...
 
siyo inainyima usingizi serikali ya magamba?
Wabunge 23 watainyima vipi serikali usingizi. Nyie endeleeni ya fujo zenu, wananchi wenye akili zao wamesha wasoma. Mtabaki na hilo genge lenu la wavuta bangi wasio jua hata kupiga kura.
 
Chadema kupitia Sugu, ndio alietuliza fujo Mbeya baada serikali na CCM kupitia polise na JWTZ kushindwa, Its true chadema imeibwaga serikali. Go on Chadema...

Katika nyanja ya kuongoza CCM na serikali yake hilo limewashinda, wanchofanya sasa ni kutawala. Uongozi si maguvu na ubabe bali ni ushawishi wako kwa wananchi ili wakusikilize na kuamini unachowaambia.

CCM imekuwa ikiwadanganya wananchi uchaguzi baada ya uchaguzi na kama ilivyo hata kwa mtoto wa miaka miwili kila siku ukimdanganya utamletea pipi itafikia mahali hata kuamini tena na ushawishi wako kwake utaisha.

CCM inachotakiwa kufanya si kukabiliana na CDM, kwa sasa CDM ina upper hand, kwami wananchi hawajawahi kuiweka madarakani na kuipima hivyo wanamatumaini kuwa huenda ikawa mkombozi wao, CCM wanachotakiwa kufanya ni kutatua changamoto za maisha zinazowakabili wananchi kwa sasa, ongezeko la vijana wasio na ajira ni threat ambayo kwa CCM ni kama kirusi cha ukimwi kinacho ji-multiply, muda ukifika ARV(dola) haitasaidia tena kuongeza uhai na hiyo itakuwa hatma ya CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom