Nina kiburi (I am proud) kuwa mTanzania

Kabla sijaudhi wengi, nilikuwa natania. It is all good. Mkuu ameapologise na ameonyesha namna gani muungwana anavyotakiwa ku'behave'. Shukrani kwa wote.
 
Ahsante kwa hayo, nnaomba radhi kwa kuwaudhi watu, si niya yangu kumuudhi mtu bali kilichoniudhi, ni simply mimi nilikuwa nachangia thread na nikasema yangu ya kupinga ubaguzi, na muyu mwanamke akanipachika jina na kushadidia ndio langu. Nikamuambia kiutaratibu, siyo mimi huyo amsemae, lakini kakazania tu.

Anyways, narudia tena, kwa kusema: naomba msamaha kwa kuwaudhi wengi, I was out of hand kwa kupachikwa jina ambalo si langu. I hope you will all understand and forgive me. And thank you bro.


Safi sana Zomba achana na mambo haya tuendelee hii ni JF ni sawa na baharini ila hapa tuna utaratibu maana sisi ni watu wazima na akili zetu .
 
Karl Peters na Livingstone walikuwa wakizipenda sana nchi zao ndo maana walionndoka makwao wakaja kwetu na kutumia muda mrefu sana kukatiza nyika na kuongea na watu. Kazi zao ziliweza kukuza chumi za nchi zao mara dufu.

Uzalendo maana yake siyo kukaa ndani ya mipaka ya nchi yako na kushiriki mgao wa umasikini. Uzalendo ni kutoa mchango wowote uwezao kutoa kwa nchi yako popote pale ulipo.

Wapo wanaokimbia ukweli wa hali halisi ya maisha ya Tanzania kwa kuiba na kupokea Rushwa wakiwa ndani ya mipaka ya Tanzania.
Wako wanaoamka na kukaa mabarazani wakicheza bao huku wakinywa kahawa na kashata za kununuliwa.
Hawa uzalendo wao ni upi?
Kuishi Tanzania????

Ndugu yangu hili somo lilimshinda Lowassa... gumu kweli..
 
Asubuhi hii nilifika kazini nikiwa mchovu baada ya kukesha kwenye simu kujua nini kinaendela kule idodomya. Nilikuwa bado na hasira na uchungu baada ya kufikia hitimisho kuwa Tanzania kuna watu baadhi tu wenye uwezo wa kuongoza nchi yetu na hakuna kitu naweza kufanya kwa sasa.

Katika kupitia email toka kwa bosi, email yake ya kwanza ilikuwa ni hii story ya bbc ambayo alisisitiza sana kuwa imemshangaza kuwa kitu kama hiki chaweza kutokea Afrika:



Kwa vile JF ilikuwa down, ikabidi nianzishe mazungumzo ya haraka na bosi wangu kuhusu hii email. Akasisitiza kuwa ameshangazwa sana na hii habari kwa vile yeye aliamini kuwa kitu kama hiki hakiwezi kutokea Afrika. Ifahamike kuwa wiki zaidi ya tano hapa ofisini habari zimekuwa tu kuhusu Kenya na namna Kibaki na wezi wenzake walivyokataa kuachia madaraka.

Imenitia moyo na kunifurahisha baada ya bosi wangu kuwaita baadhi ya wafanyakazi wenzagu (kina Euberstein) na kuwaeleza kuwa waziri mkuu katika nchi ya Afrika amejiuzulu kwa rushwa. Kwa haraka haraka nikamkumbuka Mwanakijiji na visimu vyake vyote alivyokuwa anapiga Tanzania kufuatilia mambo ya nyumbani, na pia nikakumbuka jinsi wana JF (ikiwemo wabunge na wajumbe wa kamati ya Mwakyembe) walivyoshirikiana behind the scene kuhakikisha kuwa Lowasa na wenzake wanaondoka.

Kwa kweli nimefurahia sana kuwa part ya process kubwa hii na imenipa kiburi tena kujiita mtanzania hapa kazini. Watu wengi hapa (ambao wengi wana liberal views za international politiks) walikuwa very proud na Tanzania.

Nina kiburi sana kuwa mTanzania leo. Kwa leo nitamshukuru Lowasa kwa kukubali kutoka the easy way, nitamshukuru Kikwete pia kwa kutokuwa kichwa ngumu na slow kwenye maamuzi, nitawashukuru wote hasa wabunge wa ccm kama Mama Malecela nk ambao pia walisaidia kufanikisha hii vita.

Nina kiburi sana kuwa mtanzania leo. Nchi ambayo mashujaa kama Nyerere, Slaa, na Zitto wanaiita nchi yao. Ninafurahi, ninacheka, na ingawa hili baraza ni bovu sana, lakini nina raha kuwa Mramba amekwenda......

Hongera wote waliofanya kazi kubwa, muda mwingine inabidi tupate kitu cha kufurahia kabla hatujacollapse kwa mishinikizo ya damu na misongo ya mawazo.

Nafurahia na nina kiburi sana kuwa mTanzania.

Nadhani ni mapema mno kuanza kumsifia Kikwete kwa hili baraza la mawaziri la kina chenge, nchimbi na wenzake. Kama umekosa cha kuandika ni vizuri muda mwingine utulie tu kama wenzako hapa.

Hiki ni kiini macho tu Kikwete anawafanyia watanzania kama wewe mnasahau kabisa kuwa nchi karibu yote imeuzwa kwa buzwagi na wenzake. karaghabhao
 
Nimefurahishwa sana na hii posti kwa sababu kubwa mbili: kwanza kwa moyo wa wa uungwana wa wanaogombana na kusamehe (hongera Zombe). Lakini lililo kubwa ni kutambua kwamba JF (Hususan mwafrika wa Kike) sio kazi yake kusagia na kukandia tu kila kitu kinachofanyika TZ hata kama sio timilifu (kama hili baraza letu la mawaziri) lakini kumbe tunapongeza pia.

Hongera sana Mwafrika wa Kike, hongereni sana JF!
 
Kuna mafanikio kidogo, lakini shina la matatizo bado liko pale pale. Mafanikio ni pamoja na kupungua kwa ukubwa wa baraza la mawaziri (toka 61 hadi 37). Nampongeza JK kwa hilo. Nampongeza JK vile vile kwa kuwa msikivu na mvumilivu wa criticism.

Tatizo la mfumo mbovu unaoruhusu wabaya kuuza nchi bado liko pale pale. Serikali haijakubali Bunge liridhie mikataba kati yake na wawekezaji. Katiba yetu inasema wazi kwamba Bunge litasimamia serikali, na kwamba mikataba mikubwa itahitaji ridhaa ya Bunge (nimeshaposti vipengele husika hapa JF).

Ameondoka Karamagi lakini mirija yake imebaki intact. Mkataba wa kampuni yake bandarini utaendelea kurudisha nyuma Watanzania miaka nenda rudi. Ameng'atuka Kingunge, lakini familia yake itaendelea kutudai fedha za parking mjini na za kutumi kituo cha mabasi Ubungo. Alijizolea hizo contracts kwa kutumia nafasi yake. Ameng'atuka bila kukata mirija yake.

I call for some real change. A change that would allow our Bunge to discuss and approve or reject all contracts between the government and investors.

Someone criticized Mwafrika wa Kike for working overseas. I recall someone asking Professor Mazrui once about his working in the US. The good Prof. answered that he was there to provide some vertical counter penetration. Prof. Mazrui writes, in one of his books: "Africa was a virgin continent. She was penetrated by the Europeans". Some Americans work in Tanzania, and some Tanzanians work in the US. It's a global village remember? When will this peasant mentality that all patriotic Tanzanians should work in Tanzania end?
 
zomba,
sasa "unaua timu" mkulu, kama ni hasira nadhani umezimaliza zooooooote. hakuna aliye-perfect hapa, unatoa dukuduku lako halafu yanakwisha tunasonga mbele. wewe toka jana, tena kwenye thread nyingine!! lakini bado tu?? tafadhali sheikh, inatosha kwa heshima yako wewe na sisi members wenzako..........au mpaka tumwite Kofi Annan, au yule "pimbi" tumbo kubwa kaa mimba ya watoto kumi, ati na yeye siku hizi kawa "mpatanishi" wa kimataifa, bwa'kubwa che nkapa??. let go of that B.S, jumuika barzani and have funny!!!.

YournameisMINE, je unamchukia kiasi hiki huyu Rais Mstaafu?!


Zomba;


Lakini:

Nimalizie kwa Uhodari wa msulihishi "YournameisMINE"
nafikiri ametoa mchango mkubwa kuwezesha mabo kuwa sawa.... YournameisMINE ..karibu unamfikia Koff A..mamabo yanaaza kidogo kidogo!!
Azimio Jipya,
ama kweli 'lakini' yako hapo juu kubwa kweli ndugu.... si unaona vile msuluhishi anavyohitaji suluhu pia?!

SteveD.
 
Nina kiburi sana kuwa mTanzania leo. Kwa leo nitamshukuru Lowasa kwa kukubali kutoka the easy way, nitamshukuru Kikwete pia kwa kutokuwa kichwa ngumu na slow kwenye maamuzi, nitawashukuru wote hasa wabunge wa ccm kama Mama Malecela nk ambao pia walisaidia kufanikisha hii vita. Nina kiburi sana kuwa mtanzania leo. Nchi ambayo mashujaa kama Nyerere, Slaa, na Zitto wanaiita nchi yao. Ninafurahi, ninacheka, na ingawa hili baraza ni bovu sana, lakini nina raha kuwa Mramba amekwenda......

Hongera wote waliofanya kazi kubwa, muda mwingine inabidi tupate kitu cha kufurahia kabla hatujacollapse kwa mishinikizo ya damu na misongo ya mawazo. Nafurahia na nina kiburi sana kuwa mTanzania.

Mkuu Mwafrika Wa Kike,

Salute, na huko peke yako, tuko wa-Tanzania wengi kama wewe, Respect!
 
Well mimi bado kidogo kuwa proud, i am happy not yet proud. I will be very happy and very proud to be a trully Tanzania, with brothers and sisters around the globe who have their thoughts and their hearts here in Bongoland, kama Mramba na Lowassa and company watafikishwa kwenye mkono wa sheria. Kazi inatakiwa ikamilishwe isifanyike nusu.
God our Lord, bless and save Tanzania!
 
Kama Wew Mtanzania Wa Kweli Njoo Tanzania Utuletee Hizo Pesa
Za Mabox Watanzania Wakazae Kwwenye Zahanati Safi Zilizo Bora
 
MwK,

I am proud of my heritage, I am proud of my nationality, I am proud that I am a Tanzanian, I am proud that I am patriotic!
 
I am sure most of contributors here, are not residing in Tanzania, but their ideas, financial, etc brings changes there, so still she have a right to be a proud as a Tanzanian, no matter were she live. Exposure matter

Huyu Zomba ni one-sided myopic creature..na hata siku moja hawezi kutoa point..hivyo msamehe tu..ndivyo alivyo..
 
This was war??? well from my point of a view this girl belongs to nchi ya kusadikika!! Naona sasa utapunguza kuwa pessimistic kind of a person!!

Kiukweli wewe naona hatupo pamoja, vita unayoitaka wewe ni ipi? Au hujui umasikini wetu na hali mbaya ya jamii yetu ni matokeo ya kushindwa vita mbalimbali ikiwemo dhidi ya ufisadi? Nashawishika kuwa u fisadi propagator and facilitator.
 
Kiukweli wewe naona hatupo pamoja, vita unayoitaka wewe ni ipi? Au hujui umasikini wetu na hali mbaya ya jamii yetu ni matokeo ya kushindwa vita mbalimbali ikiwemo dhidi ya ufisadi? Nashawishika kuwa u fisadi propagator and facilitator.



mie sina kiburi na tanzania na nnaomba mungu aniepushiee kiburi.

ila mie nna jifakharisha na kujivunia utanzania wangu na tanzania kwa ujumla.

na haijalishi paka ana rangi gani bali yupi anaeweza kukamata panya ndio bomba.


mwafrika wa kike baadhi ya wakati una maneno ya kihanithi uache hiyo tabia.

nnaamini ukiheshimuwenzio na wao watakuheshimu lkn kujifanya wewe ndio ree ni upuuuzi kama kuwa nje wako wengi tuko nje na hatufanyi ubarazuli kama wako, ni mara nyingi nnakuona kwenye post zako ukitumia lugha za kukebehi wengine


hata hivyo nnawapongeza wale wengi wenye kujivunia utanzania wetu



Tanzania ndiko kwetu
hatuna pengine katu
asitudanganye mtu


nnaipenda tanzaniaaaaa
nnaipenda tanzaniaaaaaa
 
Kama Wew Mtanzania Wa Kweli Njoo Tanzania Utuletee Hizo Pesa
Za Mabox Watanzania Wakazae Kwwenye Zahanati Safi Zilizo Bora

we zakwako ngapi ulizopeleka kwenye zahanati? pamoja na kuwa kwako huko nyumbani umefanya nini cha kuwasaidia watanzania? au ndo wale mnaoingia kwenye vijiwe kutetea ufisadi?
 
Back
Top Bottom