Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,074
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa upumbavu ni sifa sawa na ilivyo ufupi au urefu; yaani huwezi kuubadili. Ina maana, kwa tafsiri ya Mwalimu Nyerere, mpumbavu huwezi kumbadilisha akawa mwerevu.
Pole sana ndugu zetu wa Hanang kwa janga hili kubwa lililowapateni.
Wananchi tuliposikia Rais anaenda Hanang tuliamini kuwa anaenda kuwapa faraja waathirika, sawa na baadhi ya wengine wanavyostahili kufanya.
Lakini kwa bahati mbaya inaonekana Serikali na ikulu imejaa watu wa ajabu, ambao wamevuka hata ule mstari wa ujinga. Badala ya kuifanya ziara ya Rais kuwa ni ziara ya kuwapa faraja waathirika, wao wakaigeuza ziara hiyo kuwa ya uchawa. Yaani ziara ya kumsifia na kumpamba Rais.
Hawa watu ambao kwa kweli wamevuka hata kiwango cha ujinga, walishindwa kumtafutia mahali sahihi Rais wakampambe kwa uchawa wao wa kinafiki mpaka wakatumie misiba ya watu wa Hanang? Wakaandaa mpaka vikundi vya sanaa, ambavyo badala ya kuwafariji waathirika, wao kàzi yao ikawa kumsifu na kumwabudu Rais.
Hivi kweli nchi hii tuna watu wenye upeo mdogo kiasi hiki? Siamini na wala sishawishiki kuamini kwamba Rais alikuwa anayatarajia hayo.
USHAURI
Mambo kama haya ya hovyo, yanampa ujumbe Rais kuwa ndani ya Serikali yake amejaza watu wa hovyo wasioelewa hata kitu gani kifanyike wakati gani!!