Kila mara nyingine tunakumbushana tu; tatizo letu wewe na mimi na wengine wote; linajitokeza katika haya uliyo andika katika mstari huu.Hivi kweli nchi hii tuna watu wenye upeo mdogo kiasi hiki? Siamini na wala sishawishiki kuamini kwamba Rais alikuwa anayatarajia hayo.
Kuna sababu zipi zinazokufanya wewe usiamini kuwa hayo yanayofanywa na hao watu siyo matakwa yake mwenyewe yafanywe!
Hawa watu wote wanashindana wenyewe kwa wenyewe kuonyesha upumbavu anaouhimiza mtu mwenyewe, sasa ulitaka wafanye kinyume chake?
Siku Samia akionyesha tu dalili za kuwa upumbavu huo hautaki, hutawaona tena hao watu wakipigana vikumbo kufanya hayo wanayo yafanya sasa hivi
Nimalizie kwa kusema kuwa inawezekana Samia mwenyewe kisha hitimisha kwamba waTanzania ndiyo hayo tunayo yapenda, ya kumtukuza kama kimungu fulani, na kwamba hali hiyo ndiyo njia itakayomwezesha kuendelea kutawala hawa wapumbavu.
Angetambua kwamba kuna waTanzania wanaodharau ujinga huo asingeendelea kuukumbatia na kuuruhusu kila mahali.
Hivi waTanzania kweli ni wapumbavu kama anavyo dhani yeye?

