Nimsaidieje mdogo wangu? Tafadhali naombeni ushauri wenu wanajamvi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimsaidieje mdogo wangu? Tafadhali naombeni ushauri wenu wanajamvi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mamakunda, Feb 3, 2011.

 1. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mtumishi wa serikali ngazi ya mshahara TGTS D,nimeolewa na nina mtoto mmoja, pia ninaishi na watoto wengine wawili ambao tunawasomesha secondari. Kwa ujumla maisha ni magumu ukilinganisha kipato na hiyo extended family.

  Tatizo langu ni kwamba nina mdogo wangu wa kiume ambaye alimaliza form six mwaka jana akapata division three masomo ya arts, kutokana na hiyo division na nature ya masomo na jinsia yake, kupata mkopo wa kujiunga na chuo kikuu si rahisi hivyo nikamshauri akasomee kwanza diploma ya ualimu ambayo hata mie mlezi wake nitamudu kumlipia ili angalau apate kazi.

  Tangu mwanzo kijana hapendi kusikia neno ualimu, anataka kusikia kazi zile zenye mapesa mengi lakini kutokana na economic background inakuwa ngumu kumlipia ada kwenye kozi anayotaka. Hivyo tulijitahidi kumshauri na kumpa mifano hai na baadaye akakubali. Lengo la kumshawishi akasomee ualimu ni kwamba ataweza kupata ajira kirahisi na pia kujiendeleza ni rahisi na pia pesa atakayolipwa itamsaidia kujiendeleza mwenyewe kwenye profession aitakayo. Nikajitahidi kumtafutia chuo cha serikali kikapatikana na nikalipa ada na mtumizi mengine.

  Sasa baada ya TCU kutoa majina alipata chuo kikuu kama alivyotaka ila kwa bahati mbaya hakupata mkopo kitu ambacho na mie nilimdokezea toka mwanzo kwamba kupata mkopo si rahisi. Lakini kijana aliamua kuacha mafunzo ya ualimu na kwenda huko IFM bila hata ya kuniambia mimi dada yake toka mwaka jana 2010,mwezi wa 11 . Amefuatilia mkopo mpaka amechemka sasa ndo anatuma ujumbe eti hajapata mkopo nimtumie pesa.

  Jamani kama mnavyoyajua maisha ya chuo, accommodation, stationery, meal, na vingine vingi. kwa uwezo wangu kamwe siwezi kulipa hata kama nitasema tutakula majani ili kijana asome, Mbaya zaidi kule chuoni kwenye diploma alitoroka na hawawezi kumpokea tena. Mpaka aombe upya mwakani.

  Nategemea mawazo kutoka kwenu, source ni mimi mwenyewe!
   
 2. semango

  semango JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  pole sana mamakunda.kikubwa cha kwanza ni kuhakikisha bwana mdogo anaelewa hali halisi ya maisha yako.fanya kila njia kwanza aelewe unajinyima kiasi gani ili tu uweze kusurvive na kutunza familia uliyonayo.akishaelewa then ndio umpe somo upya juu ya kwenda kusomea ualimu.kwa kweli coarse zingine huwa ni gharama kubwa so option ya ualimu ndio the best kwake hasa ukizingatia financial situation ya familia.ninaimani akielewa ugumu halisi wa maisha hatasumbua tena.tupo wengi sana ambao ugumu wa maisha umetudivert kutoka kwenye career ambazo zilikua ndio ndoto tangu utotoni but life goes on!!
   
 3. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli kama kumuelewesha nilishajaribu vya kutosha, ilifika hatua hata mume wangu akampigia magoti akamwambia kwamba hatuna namna nyingine ya kumsaidia, ila ni hiyo ya kusoma ualimu ili angalau apate kazi itakayomwezesha, tukampa na mifano halisi ya watu wazito waliopitia ualimu na wengine waliweza kubadilisha profession ndani ya ualimu. Lakini mdogo wangu ni rigid hataki kusikia ushauri, yeye na uhasibu tu. Mpaka hapa sielewi itakuwaje.

   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mamakunda,

  Naona wewe unalea panya kwenye debe la unga. Shauri yako, siku ukichungulia utakuata hakuna kitu tena. Sijui utamlilia nani.

  Huyo kijana mwache afukuzwe chuo na baada ya hapo asikanyage kwako tena, kwani kitu alichokifanya ni dharau kubwa. Aende kijijini kwa wazazi wake. Akikaa huko hadi muhula mwingine wa masomo lazima akili yaka itarudi na kama ikabaki hivyo basi ujue huyo siyo riziki! Pumbavu mkubwa huyo....!!!!:sad::sad::sad::sad::sad::sad::sad::sad::mad::mad::mad::mad::mad::mad:

  Babu DC!
   
 5. C

  Chamkoroma Senior Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu akubariki kwa juhudi kubwa uliyoonyesha kwa mdogo wako japo yeye haoni ila anafata mkumbo wa mabest wake wapo IFM na yeye anataka kuwa acc. ni ngumu jikune uwezapo, mimi ni mzazi nawaambia wanangu pia usipojitahidi kufika viwango utaend ualimu kisha utabadili mwenyewe mbele ya safari, kama hataki waambi wazazi kama wanaweza wasaidie kama ngumu mwache aamue yeye, watotompaka afike mwisho ndipo aamue kurudi, hna huna tu uuze nymba asome anachotaka? hataki basi endelea kumwambia sina hataki a reseat akifauli zaidi aende mbele kwa mkopo wakati mwingine kwanza bado mdogo anaweza kurist akipasua paper dDIV 1 basi aende UDSM.
  Pole lkn ni challenge yatapioata tu.
   
 6. Linamo

  Linamo JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 9,055
  Likes Received: 21,275
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu"asisome kwa kufata mkumbo"ajikune mkono unapofika atajutia.
   
 7. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ulichokifanya mama ni sahihi kabisa. Mimi mwenyewe nakwambia nilipata div three nikakosa chuo. Tangu mwanzo nilipenda sana kuwa mhasibu. Nikaenda ualimu na nikasoma kwa bidii. Sasa hivi nina masters na CPA. Kama anataka kuendelea ifm mwambie atafute means yeye. Akishindwa na ikibidi arudi home mrudishe kijijini akakae huko hadi msimu wa vyuo vya ualimu utakapoanza. Atashika adabu. Anakuonea kwa kuwa wewe na mwanamke, ingekuwa mimi angerudi na makofi juu
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hicho ndio anachokistahili. Jitu linasaidiwa halafu linataka kuleta nyodo? Yaani nimekasirika sana. Ni kama wale wanaoenda kwa ndugu halafu wanaleta upuuzi wa kuchagua chakula. Nikimnasa wa namna hiyo nitamkung'uta mikanda hadi ashike adabu. Akasome ualimu na kama hataki aende mtaani akatafute pesa yake ili aone kama ni rahisi. Mijitu ya hivyo hata haikawii kuwa mibwabwa.

  Babu DC.
   
 9. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Yaani hapa nimesoma maelezo yako dada na comment nzuri za wanaJF mpaka nimeshindwa pa kuanzia.... Ila la msingi muache huyo kijana arudi kijijini akae mpaka muhula mwingine atapata akili.... ila kamwe usimruhusu akae kwako, aende kijijini akaone jinsi maisha yalivyo na ajue maisha ni kuishi sio kuiga!!!
   
 10. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyo nduguyo hana shukurani asikusumbue. Akili hana, uwezo hana. Ulichofanya ni sahihi kabisa katika kumsaidia. Kama hasaidiki, achana naye. Mrudishe kwao. Kidogo ukipatacho somesha wanao.
   
 11. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashuru Mamkwe, mimi siishi naye niko mkoa Mwingine kabisa nyanda za juu kusini, Kwa hiyo huko Dar aliamua kwenda kinyemela na akatoroka chuo nilichokuwa tayari nimeshalipa gharama zote kama post inaeleza. Ila kwa kweli kwangu hatakanyaga tena. Yaani mie najibana kazi yenyewe haina marupurupu nasubiri mwisho wa mwezi haf bado mtu anakataa ushauri wangu kama mlezi wake!
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Najua inauma kupoteza pesa zako kumsaidia mtu ambaye haoni kama anasaidiwa na hajui ugumu ambao unakumbana nao ili walau yeye awe binadamu anayejitegemea. Pia inauma kwa sababu ni mdogo wako na damu ni nzito kuliko maji. Ila kwa matendo yake hayo, naomba ujitahidi kuyasahau na kwenda mbele. Na hapo ndipo tunapokushauri usije hata siku moja ukampa nafasi ya kuanza kukueleza upuuzi wake. Kama alijua wazazi hawana uwezo basi alitakiwa kuwa na hekima na kuwasikiliza wale wote waliojitolea kumsaidia. Hakuwa hivyo na ndo maana nikasema huyo si riziki. Akipenda akaolewe ili apate vya bure. Hutakuwa na lawama kwa lolote litakalompata.
   
 13. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakushukuru sana Dark City hakika umeguswa sana na tatizo hili, ila jamaa mwenyewe ni Mwanaume si binti
   
 14. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  pole sana Dada yangu.Huyo mdogo wako hana akili nai naonyesha si mtu wa shukrani,anasaidiwa lakini haoni,achana naye.beba mtu anayebebeka asiye bebeka achana naye.
   
 15. M

  Muinjilisti Senior Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo dogo wako kaniudhi, utafikiri mimi ndiyo dada yake! Kwa kweli anakuonea na anaweza kukuharibia ndoa. Mpaka shemeji yake anampigia magoti ili aelewe hali halisi yeye ubishoo umemjaa. Kisha kaamua mwenda IFM bila kukushirikisha mlipa ada? Labda anaye mwingine aliyemtegemea atamuwezehs maisha yake ya Dar akijua Dada yupo mkoani. Nakushauri waambie wazee kinachoendelea halafu achana naye kabisa. Maana vijijini wanaume kama yeye wameona na wanategemewa, muache dunia imfunze, ikishamfunza, mwenyewe atatafuta ualimu msimu ujao, atakuomba umsaidie, nawe kama ulivyokuwa unamsaidia utamsaidia kadiri Mungu atakavyo kujalia. Maana wajibu wa kumsomesha ni wa wazazi wake, wewe unamsaidia tu, inabidi aelewe hivyo kwanza
   
 16. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  ****** huyo, mjalaana mtoka pabaya, maluun, Al-inkfishah mkubwa huyo! Ulichofanya dadangu hata mbele za Mungu kinaonekana, usibebe mizigo isiyobebeka. Hela uliyopanga kumlipia ada mwakani huko TC nipe mimi niongeze boom langu hapa chuo cha taifa-UDSM. Akaunti namba 01J2014882200 CRDB Kijitonyama.
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimeoana sana kwamba dogo ni kidume lakini cha hovyo. Ndo maana nikasema kana anataka vya dezo mwache akaoelewe. Mwanaume wa namna hiyo hafai kuitwa mume na baadaye baba. Sasa atafaa kwa lipi kama siyo yale mambo ya mwambao kama Zenji, Mombasa na Tanga? Amenikera sana huyo dogo, ni mjinga sana tena sana!
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapo sasa na wewe umezidi...Kama angekuwa nazo za hivyo kiasi cha kuwakatia watu alikutana nao kwenye net si angempeleka dogo direct huko IFM? Hakuna mtu mwenye pesa na roho nzuri kiasi cha kumgawia kila mtu. Hata RA anawalipa watu ujira kwa kufanya kazi zake. Sasa wewe akuwekee kwenye account umemfanyia nini?
   
 19. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante kwa busara zako Muinjilisti, Mungu wangu ninayemwamini akubariki sana,
   
 20. Magpie

  Magpie Member

  #20
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dada huyo kijana muambie asome hiyo diploma ya ualimu, ajitahidi aweze kufaulu kwa kiwango cha B, yaani at least lower second, alafu kwa vile sasa anataka kusoma uhasibu, aje kuomba mkopo kwa kutumia cheti cha diploma kama sifa linganishi (equivalent).
   
Loading...