Nimsaidieje huyu nguli wa mchezo wa karate?

Nimsaidieje huyu nguli wa mchezo wa karate?

Mkuu mm nipo Moro naweza pata huduma ya kufundishwa kwa ajili ya self defence naomba jibu tafadhali
 
Shule gani nzuri kwa watoto kwa hapa dar es salaam ya karate na goju luu kama unaju unishauri bro kwa miaka hii??miaka yetu ile ilikuwa zanaki secondary school hall!!

nadhani zanaki dojo kwa ajili ya goju ryu bado wana mfumo mzuri japokuwa nilipata kusikia
masuala ya upendeleo ila sikuthibitisha. si vibaya kwenda kujaribu nadhani bado wapo na sempai (sijui kama tayari ni sensei murdhika)
 
Aende kutafuta dojo la wachina pale upanga watamuwezesha ila awe tayari kwa challenge
 
Mh hapa maelezo hayajanyooka vyema,

Mimi nilianza kujifunza 'tong-il moo-do' Ila baadaye nikahama nilikokuwa na sikupata mwalimu wa kunifundisha hicho. Nilipohamia walikuwa wanafundisha 'shotokan' karate. Walichofanya ni kunipambanisha na mtu mwenye mkanda niliokuwa nao kupima level yangu kisha nikaendelea kutoka hapo.

Hii sheria ya aliyekuwa mkanda wa mwisho ndo anatakiwa kukupa unaofuata ni mpya machoni pangu.

Hata hivyo kuna jamaa anaitwa Zaidi Hamisi (sijawasiliana naye kumuomba ruhusa ya kuweka namba yake hapa) ni kocha wa JUDO Tanzania ingawa anafahamu pia aina kadhaa za karate. anaweza kuwa msaada mkubwa sana kwake.

Ukifanya google search hutomkosa na mawasiliano yake. Ukishindwa nitafute nitakupa mawasiliano yake.

Vipaji hivyo si vya kupoteza ingawa ajaribu kunyoosha maelezo yake hapo kwenye mkanda wake. Kuwa professional lazima uwe na sifa husika lasivyo ataishia kufundisha mtaani. Najua vijana wengi walikuwa vizuri kuliko ila ilibidi waanzie mikanda ya chini kwa kuwa walikuwa wanajifunzia mtaani. Of course hata kwa ndugu yako kama kweli ana uwezo anaosema anao, hatochukua muda mrefu kuufikia na kuutetea mkanda mweusi.

Kila la kheri.
Shukran sana mkuu mentor kwa maelezo mazuri,
Tatizo la dogo ni la kiuongozi tu maana toka atoke kwa sensei wake Huko Kigoma amekuwa hana wakumuongoza .

Amepambana mapambano kadhaa na watu tofauti wenye rank ya Black belt na Brown na akawashinda.

Mkuu naomba uniPm namba za huyo mdau tafadhali.
 
mi nina watoto wa3 wote wa kiume, umri mdogo ana mwaka na nusu, anayefuata, mitatu, na mkubwa mi tano, natafuta mwalimu wa Aikido kwa ajili ya hawa vijana.
 
Ni Vema akapata kibali kwanza, hii itasaidia kujuwa yuko wapi anafanya nini.Usije ikawa waharifu wanapitia kwako upat hiyo taaluma ahimu na kutekeleza uhalifu wa kiwango cha juu.Ajiunge na YMCA pale na utaratibu watamuonana kumpatia nafasi,maana ukiwavizuri katika mchezo huko huwezi jificha ukiwa pamoja na wenzako.kuanzia hapo sasa mlango utauwa uko wazi.
YMCA ipo wap mkuu?
 
Mkuu mm nipo Moro naweza pata huduma ya kufundishwa kwa ajili ya self defence naomba jibu tafadhali
Mkuu nimeweka namba za cm hapo juu hebu mpigie muongee muelewane..Yupo tayari kwenda popote kufundisha ila ni kwa nia njema tu.
 
nadhani zanaki dojo kwa ajili ya goju ryu bado wana mfumo mzuri japokuwa nilipata kusikia
masuala ya upendeleo ila sikuthibitisha. si vibaya kwenda kujaribu nadhani bado wapo na sempai (sijui kama tayari ni sensei murdhika)
Mkuu unaweza kunipatia namba za huyo sempai plz?
 
Habari wakuu

Nina mdogo wangu ambae ni nguli ktk mchezo wa karate,kiufupi dogo yupo vzr tu.
Amekuwa mwalimu wa watu wengi mkoani mwanza mpaka baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakimfuata awafundishe mchezo huu.

Kwasasa yupo dar na anataka atumie kipaji chake kujiingizia kipato halali,je nifanyeje ili kumsaidia..?Msaada wakuu kama kuna mtu anaweza kumsaidia Tafadhal awasiliane nae kwa namba hizi 0659227342. Thnx
Mkuu ushauri wangu ni kuwa mwambie aende kwenye hizi shule za academy najua watakubali awape idea ya kuanzisha ishu za activities kwa watoto then awaambie kila mzazi atatongeza elfu 5 tu au 10 katika ada ili mtoto wake aweze fundishwa nakuambia atapata watoto wengi sana mkuu
 
Mkuu ushauri wangu ni kuwa mwambie aende kwenye hizi shule za academy najua watakubali awape idea ya kuanzisha ishu za activities kwa watoto then awaambie kila mzazi atatongeza elfu 5 tu au 10 katika ada ili mtoto wake aweze fundishwa nakuambia atapata watoto wengi sana mkuu
Good Idea mkuu ngoja tujaribu
 
Mkuu unaweza kunipatia namba za huyo sempai plz?

bahati mbaya sina namba yake. ila ukienda zanaki sekondari kwenye saa kumi na moja na nusu au kumi na mbili jioni utakutana wanadojo wakielekea mafunzoni watakupa taarifa zaidi.

uzuri wa goju ryu ni sanaa ya mapambano ndio sababu huikuti kwenye mashindano mbalimbali kama sanaa nyingine za kujilinda.
 
Anacheza karate, mtindo upi Goju ryu au Shotokan?
 
Mwambie aje Dodoma kuna dili kwa hii mambo
 
Back
Top Bottom