Nimrudishie pesa zake?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Wakuu, nilitendwa na dada mmoja miaka mitatu iliyopita. Nilipata secondment Nigeria kikazi kwa kama miezi kumi hivi, baada ya kurudi nikamkuta na kitumbo cha miezi 3. Huyu alikuwa mtarajiwa wangu ambaye tulifahamiana na kuaminiana sana kiasi hata cha account na vipato vyetu kuwa wazi kwa wote. Baada ya kutendwa sikuwa na hamu tena ya kuwa na mahusiano, maana sikuwa nawaamini wadada tena. Niliamua kufocus kwenye shughuli zangu binafsi ambazo kimsingi zimenipa maendeleo kiasi.

Pamoja na kwamba dada huyu aliolewa, lakini kwa kama miezi 14 sasa, amekuwa akinitafuta mara kwa mara akiomba msamaha na kusisitiza kuwa bado ananipenda. Nimekuwa nikimkwepa sana lakini hakati tamaa kila ninakojificha, hunitafuta mpaka kunipata. Nilimkalisha chini na kumuonya kuwa kamwe siwezi kumrudia maana amekuwa mke wa mtu na ni hatari kucheza na wake za watu.
Cha ajabu nimekuta kaniwekea kwenye akaunti yangu fedha taslim kama 4m na kasha kunitext pole kwa yote, fungu hilo likufariji. Baadaye alituma ujumbe kwa email akionyesha masikitiko yake kwa aliyoyafanya na kusema nipokee hizo hela na wakati wowote nikiwa na shida nimtafute maana yuko tayari kwa lolote.

Kwa ufupi nimeapa SIMTAFUTI hata kwa dawa. Wadau mnanishaurije, nimrudishie pesa zake?

Wasalaam,
HorsePower Kufakunoga
 
Chukua mshiko acha kujibaraguza wewe. siku hizi bwana haya mapenzi haya[po na akija tena anataka kukupa chakula wee kaa chini kula chakula.......
 
Usirudishe pesa, kwa uelewa wangu mdogo naona anania ya kukununua, kula pesa na usimtafute kama ulivosema, ukionananae tu utashirikiananae maana vishawishi vitakuwa vingi, tumia pesa uchune, ikiwezekana mawasiliano na yeye ata katika simu yasiwepo kabisa mwisho wa siku atakubali matokeo na ataacha kukutafuta, Kipo kilichomsibu huko ndio maana mawazo yake yamerudi kwako
 
Wakuu, nilitendwa na dada mmoja miaka mitatu iliyopita. Nilipata secondment Nigeria kikazi kwa kama miezi kumi hivi, baada ya kurudi nikamkuta na kitumbo cha miezi 3. Huyu alikuwa mtarajiwa wangu ambaye tulifahamiana na kuaminiana sana kiasi hata cha account na vipato vyetu kuwa wazi kwa wote. Baada ya kutendwa sikuwa na hamu tena ya kuwa na mahusiano, maana sikuwa nawaamini wadada tena. Niliamua kufocus kwenye shughuli zangu binafsi ambazo kimsingi zimenipa maendeleo kiasi.

Pamoja na kwamba dada huyu aliolewa, lakini kwa kama miezi 14 sasa, amekuwa akinitafuta mara kwa mara akiomba msamaha na kusisitiza kuwa bado ananipenda. Nimekuwa nikimkwepa sana lakini hakati tamaa kila ninakojificha, hunitafuta mpaka kunipata. Nilimkalisha chini na kumuonya kuwa kamwe siwezi kumrudia maana amekuwa mke wa mtu na ni hatari kucheza na wake za watu.
Cha ajabu nimekuta kaniwekea kwenye akaunti yangu fedha taslim kama 4m na kasha kunitext pole kwa yote, fungu hilo likufariji. Baadaye alituma ujumbe kwa email akionyesha masikitiko yake kwa aliyoyafanya na kusema nipokee hizo hela na wakati wowote nikiwa na shida nimtafute maana yuko tayari kwa lolote.

Kwa ufupi nimeapa SIMTAFUTI hata kwa dawa. Wadau mnanishaurije, nimrudishie pesa zake?

Wasalaam,
HorsePower Kufakunoga

pesa chukua, but mahusiano ya mapenzi acha...mke wa mtu sumu
 
Kama huna njaa ya pesa ni bora umrudishie tena mkononi mwambie pesa zako hizi hapa.
 
Mtoa mada usithubutu kumtafuta ukampa pesa yake mkononi hakuna hiko kitu, kama unataka mahusiano nae tena ndio utakuwa umetengeneza njia

Kama huna njaa ya pesa ni bora umrudishie tena mkononi mwambie pesa zako hizi hapa.
 
Fedha chukua. Sababu hukuomba na wala hukuzihitaji. Fanya hivi: Wapelekee msaada watu wenye mahitaji na wanahitaji msaada kwa kweli. Mfano waweza kutoa msaada kwa watoto yatima, ambao wanalelewa katika vituo mbali mbali, kwa kuwalipia Ada na michango mbalimbali kwa wale ambao wapo mashuleni kupitia vituo vyao. HAKIKA MCHANGO WAKO UTAKUWA WA MANUFAA SANA KWA HAO WENYE MAHITAJI NA MUNGU HAKIKA ATABARIKI KAZI ZA MIKONO YAKO. Mshukuru huyo X friend wako na baki na msimamo wako kwamba yeye tayari ni mke wa mtu.
 
Fanyia kazi hiyo pesa acha ujinga, usikubali mahusiano ya kimapenzi na mke wa mtu, utakuja kufa kifo cha utatanishi bure. Kama huna mpenzi tafuta angalau wa kubadilishana mawazo, itakusaidia kujiepusha naye kabisa.
 
Huyo dada amekuhonga hiyo hela ili umpende tena na mrudiane ktk mahusiano yenu kitu ambacho si sahihi. :A S-coffee:
Hiyo hela kula tu na ukiwa na shida usithubutu kumuomba chochote akusaidie.
Muombe Mungu akupe mke mwema, uoe undelee na maisha yako.
 
Dah!!hivi kumbe mapenz ya hivi bado yapo!!!
Kaka ww tumia tu hiyo hela na ikupoze maumivu kikweli,
Namwomba mungu aniepushie mapenz ya hivi mpaka kuhonga mwanaume,AMEN.
 
Mke wa mtu sumu kama unae mchumba / Gfriend mtafute huyo dada ukiwa na huyo gfriend ako umtambulishe inaweza kupunguza usumbufu kwako, pia ingekuwa fresh zaidi kama ungemrudishia hela zake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom