Heri ya Kuzaliwa Mke wangu Kipenzi

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Jun 29, 2023
286
582
Ni miaka 12 imepita Sasa toka nimalize masomo haikuwa rahisi baada ya miaka 4 ya masomo pale Dar es salaam Kwa Neema ya Mungu tukamaliza masomo

Kwakweli haukuwa rahisi hasa kutokana na changamoto za hapa na pale, nakumbuka kuna kipindi niliona kama sitaweza kumaliza chuo kutokana na changamoto za mahusiano

Haikuwa rahisi Kwa upande wangu ukizingatia nilikuwa kwenye mapenzi Moto Moto Kwa mwaka mmoja chuo kila mmoja alikuwa anafahamu kwamba flani Yuko na flani

Baada ya heart break ya mahusiano yangu nilikuwa nimebakiza mwaka mmoja Tu niweze kumaliza chuo lakini ule mwaka mmoja ulikuwa kama Miaka 100 kusoma nasoma kama sielewe nachosoma ni kitu gani?

Lakini Mungu ni mwingi wa rehema nakumbuka ilikuwa tarehe 25/12/2011 nilipompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yangu mara baada ya kuvunjika mahusiano Yangu Kwa kweli yeye ndiye aliyeondoa upweke wangu na kuanzia siku hiyo maisha ya chuo yalikuwa kama nimebakiza sekundu Tu nimalize chuo

Nilitamani Sana kuanza Maisha ya chuo na Yesu lakini haikuwa mpango wa Mungu nilikuwa Niko kwenye exit door ya kuingia mtaani Kwa kweli Mungu anamipango yake

Mwaka 2012 nikiwa najiandaa kuingia mtaani maswali yalikuwa mengi kuliko majibu , naenda kukutana na ulimwengu halisi na sio tuliokuwanao chuoni, Maisha halisi ya Mtanzania

Nilimwomba Sama Mungu anisaidie nipate kazi kwani sikuwa na connection popote ambapo ningeweza kupata kazi na nilitamani Sana kubakia Dsm Kwa ajili ya sababu zangu nilizokuwa nazo

Nakumbuka ilikuwa ni siku ya mwisho ya kutuaga nikiwa kwenye ibada ndipo nikaskia Mungu anasema Nami Kwa Mtumishi ambaye alikuwa ni mwanafunzi mwenzetu wa chuo jirani

Yule Mtumishi Kwa kweli alikuwa serious na Mungu Maisha yake na Matendo take viliendana na Kile alichokisema kwangu kwenye ukurasa wa watu wenye Imanijina lake lipo

Mungu alisema Nami kuondoka Dar es salaam na kuelekea nyumbani kwamba kuna kazi aliniandalia ya kufanya kwakweli sio kwamba sikusikia nilimskia Mungu anasema namimi live live pasipo chenga

Kwakweli nilikuwa nimelipenda Sana jiji la Dar es salaam , kuna Mambo ambayo niliyaona yalinivutia Sana hasa Uhuru WA kuabudu , nilikuwa tayari kuna makasani ambayo Kwa kweli walinibaliki Sana kwa Maisha ya wakovu

Kipeeke ilo kanisa Mungu aendele kuwatunza Kwa namna wanavyoshughulika na vijana na kujitoa kwenye Huduma za vijana sikuwai kuona kanisa kama lile Kwa kweli Mungu awabariki Kwa kazi Yao njema , matamasha ya kusifu, ibada za vijana za Mwezi , matamasha ya injili, mikesha mbalimbali tena mnachukuliwa chuoni Kwa gharama Zao kwakweli Mungu awabariki Sana

Baada ya kuzunguka Dsm Kwa takribani Miezi 3 pasipo kupata hata kazi ya kujitolea ndipo nikahamua kurudi nyumbani nacho kumbuka nilipofika nyumbani kesho yake nikabeba bahasha zangu kuelekea kwenye ofisi moja Kwa ajili ya kuongea na bosi mmoja ambaye tulifahamiana kipindi cha mafunzo

Nikiwa njiani nikawa nakumbuka kuna kampuni flani niliwai kutumia CVS zangu kwenye email lakini sikuwai kupata kazi nikasema ngoja nijaribu kuwapigia simu ili niwasikia hata kama wakiambia niende ofsini kwako nitakwenda

Simu inapiga Naona simu hiko busy nilichofanya ni kutext Tu Kwa sms na kujitambulisha na kuomba kazi Kwa sms , nikiwa naelekea zangu mjini nakutana na reply njoo ofisi flani na vyeti vyako

Nikageuza Safar huyo nikaenda kwenye ofisi husika hata sikuwa najua hiko maeneo gani lakini kwakuwa ilikuwa ofsini kibwa mjini nilipoonge Tu na konda WA uelekeo niliopewa akaniambia anapafahamu

Nachokumbuka nilipofika nikakutana na bosi hakuna interview nilichoulizwa Tu unataka mshahara wa shillings ngapi? Na baada ya hapo Yule Mkurugenzi WA kampuni akanadika tarehe 10/10/2012 umeajiliwa rasmi kuanzia hapo Maisha yalibadilika tangu siku hiyo na mengine ni story

Wazungu wanasema kuna tofauti Kati ya finish na completely lakini maana ambayo ni Raisi sana yakuelezea maneno Ayo mawili ni Kwa mifano na mfano WA Kwanza

When you married the righty person you are finished but if you married the wrong one you are finish completely

Leo tarehe kama ya Leo ni miaka Mingi ambayo imepita tangu mke wangu amezaliwa kwakweli tangu nimefunga niseme ukwelie kwake nime finished Kwa kweli

Mungu alijua kunifurahisha ninaposherekea Kuzaliwa kwake na miaka kadhaa ya kuwa katika shughuli za uchimi kwakweli Mungu amekuwa wabaraka Sana

Sina chakusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwakunipa mwanamke sahihi katika Maisha yangu na siku ya leo katimiza Miaka kadhaa happy body day my soul mate
 
Back
Top Bottom