Bi. Senti 50
JF-Expert Member
- Apr 17, 2007
- 290
- 12
Nimepatwa na utata kidogo, sina mahali pengine pa kuuliza bila kujulikana na ninaomba ushauri wa kweli.
Mimi ni mama single, mwanangu ana miaka minne tu. Mimi na baba yake tuliachana kama mwaka mmoja na nusu baada ya yeye kuamua kuzaa nje ya ndoa yetu.
Nikajitutumua mimi mwenyewe na kwa kiasi kikubwa nimeweza kufanya mambo yangu mimi mwenyewe na maisha siyo mabaya sana. Hata hivyo karibu mwaka mmoja sasa nimekuwa nikijidedicate kumhudumia mwanangu na kuandaa maisha bora ya huko mbeleni na hasa kuamua kukaa single.
Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.
Sasa wamekuja hii juzi na akanikaribisha DDM Hotel kwa chakula cha mchana na akanidondoshea hilo bomu kuwa ananitaka. Sasa tatizo ni kuwa huyu bwana ana mke na watoto (mmoja ameondoka majuzi kwenda US), na mke wake ni mtumishi pia serikalini. Anataka nimpe jibu kabla hawajaondoka na amenihakikishia kuwa ati nisiwe na wasiwasi mimi na mwanangu tutaishi vizuri tu.
Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k
Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.
asanteni and I'm out.
hii imekaa ki mkwawa mkwawaNenda naye lunch halafu unampiga kibuyu. Ana mikakati gani na wewe wakati mkewe akirudi? Yeye yuko interested na short term relationship tena ambayo ni convenient kwake yeye...angekuwa anakujali angefikiria kuhusu mkewe na wewe na feelings kuwa hurt either way.
Nimekuwa nikiwatolea wengi nje kwa sababu najua wanachotaka ni kitu kimoja tu. Sasa tangia kikao cha februari kuna mheshimiwa mmoja ambaye amekuwa akinionesha ukaribu na ukarimu katika mambo mengine na tangu wakati huo hajagusia neno lolote la mapenzi kiasi cha kuanza kumuamini na pole pole nimeanza kujikuta ninavutwa kwake. Hata hivyo sikumtumia "signal" zozote za kuashiria ninavyojisikia.
Nilimuuliza kwanini anataka kuwa nami wakati ana mke? kasema ati mke wake yuko busy sana na hawezi kusafiri mara nyingi na majaribu mengi njiani anataka awe na "mtu" ambaye anamjali n.k
Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.
asanteni and I'm out.
Kwa kweli, najua ni jambo la kipuuzi lakini mwenzenu nimetingwa. Naomba ushauri.
My take you are still young life starts at 40!
na miye naruhusiwa kutoa maoni?
My dear, sijui una umri gani ili niweze kukupa ushauri unaoendana na rika lako. Wengi watanishangaa sana kusema hivi maana kuna mambo mengi ambayo yanamfanya mtu kufanya maamuzi ambayo si sawa kulingana na umri walio nao. Anyway regardless of anything and everything being constant, HUHITAJI KUWA NYUMBA NDOGO YA MTU AWAYE YEYOTE YULE DUNIANI my dear.
1. kukubali kwako kuwa mpenzi wa huyu mwanaume ina-confirm yale yote yanayosemwa na yanayoaminika(myths) kuwa mwanamke hana thamani. Kwanza umekosa nini hadi uanze kumtamani mume wa mwanamke mwenzio? Ndio maana nikakuuliza una umri gani? Kama uko ktk rika kati ya miaka 25 - 36 utakuwa pressurised by society kuwa ukamilifu wako unapatikana pale unapokuwa na mwanaume. Sasa huo ukamilifu wako utapatikana kwa kuibia mume wa mtu? Do not make decisions based on envy. Whatever you see is good for the gander may never be good for the goose.
2. Ninaamini MUNGU ndiye aliyeumba kitu NDOA. Na alipanga kuwa kila mwanaume atapata wa kufanana naye na kila mwanamke wa kufanana naye. KAMWE Mungu hakupanga wewe UWE na huyo MUME wa MTU. Ndio uliwahi olewa je umewahi kujiuliza ile misingi ya ndoa yako uliyokuwa nayo hapo mwanzoni ilikuwa misingi thabiti? Nimeona ndoa za vijana wengi zikivunjika kwa kutokuwa na misingi imara na wamebaki kulaumu matokeo kama kuzaa nje, kuacha kazi, uzinzi n.k. Cha muhimu uelewe ni kwamba ndoa yoyote ili idumu inapaswa iwe na misingi thabiti. This should be a very good lesson for you and your future husband but not your future-someone-else's-husband.
3. Kama huyo mheshimiwa anaweza akakudanganya kuwa mke wake yuko busy sana na ni sababu tosha kwako kurukia opportunity hiyo, je umemuuliza huo ubusy unatokana na nini? Kwa nini asifanye jitihada ya yeye kutenga muda wa yeye na mkewe ku-enjoy? Je anaelewa huo ubusy pengine ni kwa ajili ya kuijenga familia yake?
4. Huyo baba amekusoma na ameona kuwa wewe ni binti mpweke ambaye anahitaji mwenza and he is playing his cards well. Kama unataka another run for love. Go out, mingle na vijana wa umri wako, go out with friends for lunch. You never know......... bora hata ujigonge kwa Zitto maana he is still available or he might have a friend who is in search of a loving wife lakini sio mume wa mtu There is nothing you will gain out of it other than half appreciation, half acknowledgement, half consideration, half admiration, half respect etc etc
5. Why go for less when you can have it all with someone else? You are looking at a very small playing field. Kila siku umezungukwa na waheshimiwa usifikiri waheshimiwa ndio watu pekee duniani. Dunia ni kubwa tembea uone. Nimekutana na watu ambao hawakuwahi kuzaa na waume wa watu, wana elimu tosha ila wamekuja kukutana na their life partners when they were 36 years and beyond when doing PHDs. And they are actually doing better off than most early marriages I have seen. I say so kwa sababu ni watu waliotengeneza union wakielewa wazi nini maana ya ndoa na commitmments zao kwa wenzi wao.
My take you are still young life starts at 40! Do not go cheap liaisons, you are worth more.........
BiMkubwa usimdanganye mwenzako akajajutia maisha yake bure, at 45 menopause kicks in and sex becomes a nightmare- unenjoyable and unpleasant! Kwanini tusimshauri tu atumie condom, anaonekama kakaa muda mrefu bila kamchezo na ana kiu cha kufa mtu, go for it sister but make sure you play it safe. Hao mabachelor wako wapi? tena wengi wao hawapendi wanawake ambao wana watoto.