Nimfanyeje mtu huyu afunguke akili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimfanyeje mtu huyu afunguke akili?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WALIMWEUSI, Feb 20, 2012.

 1. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Rafiki yangu ni mlemavu wa viungo. Kuna kipindi alikuwa vibaya kiuchumi, and that time wadada wengi walikuwa wanamkataa alipowatongoza. Mungu mkubwa akatokea mdada ambae alimpenda sana pamoja na kuwa mlemavu na hana hali nzuri kifedha. Pitapita mdada kapata mimba na wakati ana mimba jamaa mazali ya pesa yakamuuangukia. Kifupi life ikabadilika. Yule dada alikuwa wa kawaida sana (sio mrembo sanaaa au dada du) na elimu yanke ni form four ila ni mdada wa heshima.

  Sasa ivi jamaa kifedha yuko poa, mademu kitaa wote wanamtaka, sasa yeye anadai yule dada sio chaguo lake (alozaa nae), kampata ambae ni chaguo lake. Hataki kuishi na yule mdada na mtoto tena, na kapata dada du mmoja tena msomi (ana Masters) na ni mzuri sana kwa kweli kiasi kwamba ye mwenyewe hana amani kabisa. Bro wangu kasoma na uyo demu, anasema bonge la kicheche.

  Kwa mtazamo wangu nilimshauri asiachane na yule alozaa nae coz nadhani ndo mwenye mapenzi ya dhati kwake. Yeye anadai sio chaguo lake na ana imani anaweza kupata mke mwingine msomi (kama aliyenae) na wakaishi happily. Nifanyaje nimnusuru jamaa na ili zigo analotaka kulibeba?
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Du Jamaa yako mwache tu aende asije kujuta au nayeye ana tabia kama za Amyner? Huyo demu aliyempenda mwanzo wkt hana kitu ndio wa kua nae karibu sana aachane huyo wa masters anataka fedha tu huyooo!
   
 3. m

  mchambakwao Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo jamaa (mlemavu) ni **** na asiyetumia akili kufikri alikotoka.Pesa ni maua muda wowote yananyauka,mwambie akumbuke alikotoka na ikiwezekana mkutanishe na bro wako apate ukweli kuhusu huyo dada anayempenda now.
   
 4. chriss brown

  chriss brown JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msichana mpaka kufika Masters kashaona direction ya maisha yake inaelekea wapi!ukicheche wake nahisi upo damuni,lakini hamfati huyo bro.wako kwa ajili ya pesa,anamengine huyo.Pesa anazo,sema ukicheche upo damuni.

  Atulie na huyo mama watoto wake wa form four.
   
 5. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huna haja ya kumstua. Atastuka baada ya kumkuta yatakayomkuta. Balaa litaanza mama atakapotaka uhuru wake kufaidi elimu yake wakati jamaa akijishuku kuliwa vyake kutokana na hali yake. Kimsingi huyo jamaa yako hana maana na amini kuna siku atalipwa kiasi cha kutoamini macho yake. Hakuna kitu kibaya kama wizi wa fadhili. Analitafuta la kulitafuta na haraka atalipata piga ua. Mara zote limbukeni akizidaka lazima aingizwe mjini ili alie baadaye.
   
 6. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Kama haelewi mwache, kwani atakuja kulazimika kuelewa.
  Asifyeke kitasa alichojikinga mvua baada ya jua kuwaka na mvua kukatika.
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Subiri yamkute ndiyo atatia akili............................!
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Muambie aoe hiyo masters banaa! Kwanza ana hela, mwanamke wa form four hamfai manake kazoea shida. Sio wa hadhi yake na hajui ku-spend. Afu akipata wa phd achangamkie tenda.
  If there were no women, what will do with all the useless money they earn? I always wonder!
   
 9. i

  ivy blue carter Senior Member

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yah wengio ndivyo walivyo, eti akipata hela sio chaguo lake weye uliyekuwa nae kipindi cha ukata..... inauma haswaa!
  na ni mlemavu wa aje lakin?? nways ngoja yamkuta afunzwe na dunia atakoma ni limbukeni wa mapenzii huyoo hajayajua fresh ss ngoja yampe darasa atulie.
   
 10. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mwambie asidharau dafu , embe ni tunda la msimu ...

  amepata mwanamke wa matumizi mwache atumie ila asije lalamika baadae
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,858
  Trophy Points: 280
  mtoto akililia wembe mpe ajikate mwenyewe....................baadaye yakimfika atajifunza ya kuwa kitunze kikutunze........
   
 12. Vodka

  Vodka JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 909
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sometimes nasema simba akikosa nyama hata majani atakula,..Jamaa kala majani anakuja kupata nyama kumbe ni kibudu mara mia angebaki kula majani.,ajui ila atakapo jua atajuta sana,la muhimu mwanamke aliye mzalisha apiganie haki zake kisheria juu ya mtoto na atulie na maisha yake wala asiangaike na huyo tamaambele.Ipo siku atakuja kuona umuhimu wake.
   
 13. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Demu alozaa nae anamdharau sana. kuna siku alikuja kwangu uyo demu akanambia rafiki yako kanambia niende kokote coz chaguo lake anakuja home so hataki matatizo tena akamwambia aende na mtoto coz hataki uyo mwenye mastaz akasirike! Ni kwa vile jamaa ni mlemavu tu ila angekuwa mzima ningemtwanga mangumi. Dem kakaa kwetu hadi saa 3 usiku ndo anampigia simu arudi eti mastaz kaondoka, lol!
   
 14. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Miguu imepooza na nimifupi so anatembelea magongo!
   
 15. salito

  salito JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  huyo majuto yanamtafuta...
   
 16. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  jamaaaani,huyo rafiki yako mbona kama na utu wake umelemaa?yaani anamtenda hivi mdada wa wenyewe kweli?malipo yake hayatakawia na hatayasahau.
   
 17. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kweli kabisa
   
 18. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  Eti alisali sana ndo akaoneshwa mke mwema, mastaz girl! Kiukweli walemavu wengi niliowaona wameona au kuolewa na walemavu wenzao. Wachache sana wameoa au kuolewa na wasio walemavu (ye mwenyewe analifahamu hilo) ila jamaa anadai its impossible ye mlemavu na God ampe mke mlemavu. I told him mbona God keshakupa uyo ambae sio mlemavu na keshakuzalia mtoto kabisaa!Anadai sio chaguo lake.

  Mie ntasitisha zoezi la kumshauri, mana siku zinavyoenda jamaa anazidi kunchukia asije nifikiria namtaka mastaz wake buree!
   
 19. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Ipo njia ya mtu ionekanayo njema machoni pake mwenyewe, lakini mbele ni njiaya mauti.
   
 20. m

  mkazamjomba Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  zigo la mwizi halipokelewi mwache yamkute hajui akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
   
Loading...