yohana Malekela
Member
- Sep 12, 2017
- 41
- 42
Pole kaka. Hakuna milima Bila ukungu means hakuna binadamu Bila matatizo/changamoto. Kitu kizuri ni kuwa akili yako inamchukulia ni mchumba na syo mke.Najua wote humu hamjambo maana huwezi ingia humu huku unaumwa
Twende kwenye mada
Wakuu nimepata mke ambaye natarajia kumuweka ndani ila sasa
Kabla ya kufika huko kwenye kuwekana ndani
Nilimpima kwanza je atafaa kweli kifupi huyu binti nipo naye kwenye uchumba karibia miaka 2 navyosema uchumba yaan yupo gheto siwez ita mke mana hutajafunga ndoa
Kasoro ya huyu mwanamke kwanza sio mkweli anaweza kukudanganya hata kwa jambo
Ambalo unaliona hili halipo hivi
Sasa sijajua huwa anamaanisha nini?
Licha ya kumuonya mara kadhaa ila hurudia hivyohvy
Na akiona huna pesa hujinunisha hata wikii nzima na unyumba ulambi najua baadhi ya wadau mtasema tafuta pesa
Ipo hivi pesa hata uitafute vp ila kuna muda mambo hubuma maana kuna kuumwa nk...
Kwa kuliona hilo nikajipigapiga nikamfungulia shop ya nguo ilikuwa vizuri ila mwishon akafanya anachojua yy akajifilisi maana mwenendo aliokuwa nao ilikuwa lazima ajifilisi
Na ilikuwa ukimuonya anasema mnatunyanyasa wanawake Na atanilipa hela yangu mimi huwa sina maneno hua namwangalia tu sasa wakuu
Je kwa tabia hizi je niingie mazima au nifanyeje
Kuna wadau baadhi utawasikia umeshindwa kuamua hadi kwenye hili?
Nasema hivi ndio nimeshindwa naombeni ushauri wenu
Kama ungekuwa unamchukulia kuwa ni mke naamini usingekuja na huu uzi kwa sababu hyo. Namaanisha ungepambana kuhakikisha unaliweka sawa hilo. Sababu ungempenda kama mke na si kama mchumba. Wife material hayuko na tabia kama hizo. Alfu kitu tunachokosea ni kuwa, tunaingia kwenye uchumba wa kuchunguzana wakati uo huo tunaingia kwenye mahusiano na mwisho wa siku tunapenda na kulisahau jukumu la kuchunguzana. Na ukisha mpenda mtu hata kama utayaona madhaifu yake,kumuacha inakuwaga ngumu Sana ndo sababu umekuja na huu uzi.lakin kama ungekuwa hujampenda usinge jiuliza mara mbili mbili hata utake mashauri kwetu. Na kama ilivyo,Aliyeko mchezoni hawezi ona makosa bali aliye nje ya mchezo. Achana nae huyo syo mke kaka.




