Nimfanye nini huyu mwanamke?

lusanasaimon

Senior Member
Jan 19, 2023
111
264
Habari za jioni mabibi na mabwana, kwanza nijambo lakujivunia Christmas tumeimaliza salama na naamini mwaka mpya wote tutafika salama mungu yu nasi.

Niende kwenye mada bila kupoteza muda mimi nimeoa na ndoa yangu ina miaka kadhaa. lakini kuna tabia ambazo mke wangu anazo nashindwa kuzielewa. Mke wangu amekuwa na tabia ya kuleta ndugu zake nyumbani na kuwa shawishi waniombe hela hasa dada zake. na amekua akifanya haya kila anapoona nimehifadhi kiasi cha fedha chumbani. Na tokea nigundue hili niliamua kuwa nina zificha pesa zangu. Sasa kisanga kimeanza tarehe 25 Christmas ambapo alienda kwenye mishe zake lakini alirudi mapema na alikuja na dadake na rafiki yake ambapo alinipigia simu nakuniuliza nilipo. Nikamwambia niko home najiandaa kutoka akaniambia nimsubiri yuko karibu na hazikupita dk5 wakawa wamefika. Nakumbuka tulisamiana tukajuliana hali za siku mbili tatu. Nikaaga ili niondoke ndipo shemeji yangu huyo akaniuliza kama kunitania ya kwamba kwahiyo ndio naondoka kwa sababu nimewaona?

Nikasema hapana hata hivyo nilikuwa na mpango wa kutoka. Hapo hapo mke wangu akadakia akiwa chumbani akisema akupe hela ya Christmas nikajibu kwa LEO sina. mke wangu akaendelea kusisitiza ya kwamba mm ni muongo pesa ninazo.. dah nikajiuliza sasa huyu mwanamke anani chukuliaje? na hicho kitendo sikukipenda na si mara moja anafanya huu ujinga ndipo nilipo mwambia kama anayo ampe nitamrudishia akasema sawa, basi mimi nikawa nimeondoka. sasa juzi asubuhi alinikumbusha akaniambia eti alimpa eflu20,

Ila nikamwambia tabia yako sio nzuri inabidi tukae chini tuzungumze. Nakumbuka alinijibu huku akitoka njee eti kwahiyo natabia mbaya kisa ndugu zangu kukuomba pesa ya sikukuu? eti mbona unapo watumia pesa wazazi wako sisemi? Tena kwa sauti na majirani wanasikia. Aisee nilijisikia vibaya nikamuitia ndani nikamlamba kibao na nikamwambia na pesa sikurudishii maana hizi ni dharau,

Unaongeleaje mambo yangu mimi na wewe njee na kwa faida gani? nikaondoka na nilirudi usiku sana,

Sasa leo ndio nimemuona nimjinga kiasi gani amedamka mapema nakunikumbusha ile pesa sikumjibu. mwisho nikaona anachukua sim nakumpigia yule dadake akamwambia eti iyo tabia yakupenda kuomba omba pesa waache eti mimi nimemwambia. kwanzia leo wasiwe wananiomba chochote na akamdai na ile elfu 20 amrudishie ikabidi dada mtu amuombe mume wake na wakamtumia kwenye airtel money,
nilipigwa na butwaa wala siku ongea chochote

Nasikia wamepigiana simu wote kwa kilichotokea. kwahiyo kaamua kunichoma kwa ndugu zake hadi ukweni
 
Back
Top Bottom