Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Nimewahi kuwa changudoa, nimjulishe?

Wewe kausha kwani yeye unauhakika amekuambia yote kuhusu past yake, usikute yeye alikuwa na tabia chafu kukuzidi. Hata hao wenzio wakimuambia wewe kataa mwambie wanakupakazia. Hata wakiwa na picha yako ukiwa uchi mwambie imetengenezwa. Mungu mwenyewe sio mjinga alivofanya kila mtu na siri zake, vinginevo angeweza kutuumba wanadamu kusomeka mambo yetu kila mtu atuangaliapo usoni.
 
  • Thanks
Reactions: THT
hahaa angalia tu picha zako wakati umeshikishwa ukua tusikute mtandaoni /...........
 
Yaan huyu aseme tu ukweli atajutaaaa,,watu hata wakikutwa wanakataa sembuse yaliyopitaaa kha!!!!!!
Kudadadeki mi nikiamua kukubishia hata gari ntakubishia nikwambie ni baiskeli na hadi ukashawishika kuamini kweli sio gari ni baiskeli...... sasa huyu sijui anagwaya nini kubisha iwapo watamchoma kwa mumewe
 
pole sana nikufariji tu kwamba karibu kila mwanamke ni changudoa tofauti ni aina tu..............hata walioolewa bado ni machangu kwa sababu analazimika kutumika ili apewe hela.................kwa wanaume ndio kabisa ingawa najua okabisa kwamba kwa sababu ya mfumo dume changu na malaya ni wanawake tu ila akikusimulia ya kwake huenda ukajiona wa maana sana.............kumbuka kwa maovu yoote bado unasimama wewe na Mungu wako hivyo tubu na kuungama na hakikisha hurudi huko tena
 
Poleeee kwa uliyopitia ni out of ur malice bt czan kama itakuwa busara kukaa kimya ni bora kuliko hata kutembea naked kwan wwe ndio wastahili kumpa ABC kuliko kuzipat kwa hao rafiki zako ili awe huru kulikabili pindi zimfikiaapo
 
Kama unataka kuoana matokeo yake sema ukweli, utaachiwa manyoya
 
Kama umeshatubu kwa Mungu wako na kuacha hiyo tabia inatosha. Kila mtu ana historia yake na kuna mengine unapaswa kuyahifadhi kwa ajili ya maisha yako na wala dini haitachukulia kama ni uongo. Kila mtu ana historia yake na hao watu mliokuwa nao Nairobi kaa nao mbali sana na usiendeleze mazoea nao. Siku kama akisikia hizo habari mwambie ilikuwa zamani na ulishatubu kwa Mungu na ulishaacha hayo mambo. Kingine ishi kwa kufuata misingi yote ya dini na pia umweleze huyo mchumba magumu makubwa mliyopita katika maisha yenu ila ilo la uchangudoa usimweleze ili akija kusikuwa ataunganisha picha mwenyewe na kuelewa kuwa ilikuwa ni mapito tu.
 
mwambie ukweli wa maisha yako jinsi ulivyoangaika kujisomesha wewe na wadogo zako bila msaada kutoka kwa ndugu mpaka kufikia muda mwingine kutembea na wanaume ili upate hela, as long hajakukuta bikira atakuelewa tu
 
kwani katika hali hiyo ya uchangudoa uliwahi kufanya kinyume na maumbile, kama sivyo kwa nini usimuweke wazi kwani hakuna mtu ambaye anaweza akaoa mwanamke ambaye hajawahi kukutenda tendo la ndoa, japo kuwa wewe mazingira ilikuwa ni tofauti, hivyo la msingi wewe mwambie ukweli isije siku moja akayasikia ikawa sheeda
 
Never try to tell him it wasn't your fault js feel relaxed, akijua from others ndo ufunguke na kumweleza hali halisi. Don't dare please.
 
hayo hayamuhusu wewe kula pande fanya maisha as long as umeacha kula vichwa fanya maisha sasa kimya kama hakikutokea kitu vile
 
tatizo nimekuwa mtu wa dini na sipendi kuendelea kuwa muongo kama mama alivyonidanganya
pia kuna waschana wawili wakenya wanaishi hapa ARUSHA na tulifahamiana KENYA kwenye hotel
Amekuuliza au unataka kujichanganya tu mwenyewe? Akikuuliza kama ulishawahi kuwa CHANGUDOA mwambie ukweli, ila kama hajakuuliza kaa kimya maana sisi WANAUME huwa tunajijua wenyewe
 
Changudoa home Arusha, baba Mngoni, mama Mchagga

Ilikuwa hivi; baba na mjomba waliwekwa Korokoroni kwa kesi ya ujambazi tukiishi na kusoma Arusha. Mimi na wadogo zangu wawili kuna siku ghafla kama saa nne mama akaja shuleni (day skuli) akatuchukua (wawili, mdogo alikuwa hasomi) bila kupitia nyumbani tukaelekea Tanga tukakaa hotelini for two weeks then tukaelekea Kenya Nakuru ambapo mama alinunua nyumba na gari tukaanza maisha bila ya baba na mjomba.

Wote watatu tukapelekwa boarding skuli Nairobi-Kenya, mama akarejea Nakuru. Miaka minne baadae mama akakamatwa akarejeshwa Arusha kuunganishwa kwenye kesi. Mimi ndiye nlikuwa mtoto wa kwanza na wote hatukuwa tumejua kama mama kakamatwa mpaka tuliporudi nyumbani likizo.

Majirani walitushangaa na kuanza kutuuliza alipo mama. Kwa msaada tukavunja mlango, gari ilikuwepo, kuna chumba ilikuwa inafungiwa. Niliwaambia wadogo zangu mama kaenda kumsalimu mjomba atarejea. Nikaanza misele Nakuru mjini na kiboyfriend changu. Siku moja akaja mama fulani nilipokuwa nimepaki kigari mjini akajitambulisha ni Mtanzania mmarangu na aliongea kichagga nikazuga simsikii.

Akaniambia amenitambua kwa kuwa anaifahamu gari ya mama na anajua mama na nimefanana na mama. Akanieleza kuhusu mjomba, baba na akaniambia mama alikuwa gerezani Arusha kwa kesi. Akanitaka niiuze gari na nyumba fasta kabla havijakamatwa.

Akaniambia nisiwe narudi rudi kukaa muda mrefu pale nyumbani mpaka atakapoachiwa mama. Nilikuwa form three-Nairobi, four days baadae niliuza gari, nyumba ikagoma kwa kuwa collateral ya mkopo alichukua mama benki. Nikawaamuru Madogo tuondoke tuwahi kurudi shuleni mama anatusubiri Nairobi.

With time hata mwaka haukuisha hela ikakata nikashawishiwa na a classmate Elizabeth-Mkenya mkamba wa Nairobi. Tukaanza kujiuza likizo and life ikasonga na nikawa nawalipia wadogo na mimi ada. Nilijiuza mpaka nikasoma chuo na wadogo wakaingia sekondari.

Thanks God mama aliachiwa baada ya miaka mitatu. Kuna wakati tuligombana sana na wadogo zangu wakiamini mama amenipa access ya akaunti zake za benki na natumia hela nyingi kivyangu huku nikiwapa wao kidogo.

Tatizo: Kwa sasa tupo Arusha. nina boyfriend mmasai na kila wakati wa semina kanisani mchungaji husema ni bora wapenzi wachumba muwekane wazi kuhusu maisha yenu hata ya nyuma ili isiwagharimu baadae. Naogopa sana kumwambia jamaa kuwa niliwahi kuwa changudoa.

NOTE: Kuna wadada wa Kenya ambao nilijiuza nao wamehamia Arusha na hawana kazi za maana.

Nlilazimika kuhama kanisa ambalo mimi nlikuwa kiongozi wa vijana baada ya baadhi yao kuanza kusali pale kanisani uamuzi ambao BF na mchungaji wanaushangaa mpaka leo. Kwa sasa nasali kikanisa kidogo nje ya mji kwa kuwaogopa washirika uchangudoa wenzangu wa Nairobi... Nateseka sana kuwaza.

Ufafanuzi: Natumiwa PM nyingi zikitaka ufafanuzi. Hii stori ni 5% ya maisha yangu na inaeleza namna nilivyoanza na kuacha uchangudoa tu. Stori haielezi maisha ya mama wala mjomba, namna walivyokamatwa na nini hasa walichokuwa wakifanya, namna mama alivyotoroka na baadae kukamatwa. Haielezi namna tulivyosafiri toka ARUSHA-TANGA-NAKURU KENYA.
 
Pole sana mamiii kwa uliyopitia,ni vzur ukamuweka wazi bwasheee kuliko aje kupata hzo habari kutoka kwa watu wengine
 
Mwelezee tu ili uone ataupokea vipi,kuliko kuishi kwa wasiwasi.
Na endapo atakuja kufahamu kupitia external sources,basi ujue balaa litakuwa kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom