Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 11,329
- 23,260
Hii tabia nmeiona sana kwa watu imeanza kuota na kukua kama uyoga. Tabia ya kumwagiana matope au maji machafu kama ndio kusheherekea siku ya kuzaliwa.
Walianza na maji ya baridi na mabarafu. Naona wakaona hiyo si kitu sasa wanapakazana matope n.k kuna siku wataanza mwagiana maji ya chooni yalichonganyika na choo.
Leo Jumamosi naenda zangu kazini, walinifanyia surprise ya keki zawadi na vinywaji. Haikuwa tatizo mpaka hapo. Basi nmemaliza kazi akaja dada mmoja kuniuliza naondoka saa ngapi.
Nlimjibu akaondoka sikumfuatilia. Kipindi naondoka naenda parking akauliza tena "Sir are you leaving now?" Nikamjibu yes nikasimama kutaka kujua ana nini. Akanijibu tu "thank you sir, have a nice weekend" nilishangaa kidogo.
But muda huo huo nikaona watu kadhaa wanaongozana kwenye lift then mimi nikaitwa na kaka mwingine nadhani anicheleweshe kidogo wale washuke parking wakaandae jambo
Baada ya dk 4 nikaja kwenye lift then nikashuka kama baada ya dk 2 after waiting.
Nafika hivi kumbe walifanya timing vibaya ndio wamekuja na matope yao kwenye ndoo. Niliwaambia kwa ukali nione mtu ananimwagia huo uchafu na mambo ya kipuuzi. Wakashtuka kidogo maana kiukweli nlikuwa nimeshakasirika.
Ile ndoo ikashushwa, na wale wahusika wakapigwa na butwaa. Nikapita katikati yao nikaingia kwenye gari nikawasha nikageuza nikaondoka.
Huu utamaduni sijui ni wa wapi.
BINAFSI NAUKATAA NA HUWA SIPENDI MAMBO YA KIPUMBAVU KABISA.
Nlikataa toka zamani miigo ya kipumbavu. Girlfriends wangu walipata shida sana siku za valentine, maana sikuwa nasheherekea by any means.
Nadhani leo ofisini wamejifunza kitu, na ninawaambia na watu wengine muwe mnaangalia na watu. Leo ningemfumua mtu mshono. Nimewaambia ole wake mtu aje nimwagia matope. Ole wake.