Nimevurugwa sina hamu na mwanamke

Nimevurugwa sina hamu na mwanamke

ndio. alishirikishwa. ni mchungaji wa kanisa tunaloabudu. ndio yetu ni ya ki kristo na imefungwa kanisan na harusi kubwa kabisa. hakuna kitu ambacho katika ndoa yetu naweza kusema hakiko sawa. maisha yetu ni mazuri. uwezo wa kufanya mapenz ninao tena uliozidi kidogo. mtoto wa kwanza nimefanana nae kila kitu. nina uhakika ni wangu. hii hali ya utulivu na mapenz nilioonyesha kwa mke wangu na familia ya kwao pamoja na ucha mungu wetu. ndivo vinavyoniumiza nikifikiria kuwa mtoto anaweza kuwa sio wangu. kwa sabb zip. kwa mapungufu gan hayo mpaka niletewe mtoto asie wangu.

Kama aliondoka kwa miezi miwili huyo mtoto ni wako ila hata ukifanya DNA ukadhibitisha ni wako ndoa haipo tena. Pole sana
 
Anaweza kuwa wakwako au siyo wakwako...Ila ukimchunguza mtoto huna chochote ulichomwambukiza???? Kama hamna bado siyo jibu la siyo wakwako turudi kwenye DNA ili tumalize ugomvi mapemaaaaaaaa
 
Cha ajabu kipi hapo? Inawezekana aliondoka na ujauzito usiku ule mlioagana.
Ni vile tu hakuona dalili mapema.
Nina hakika DNA itaonesha mtoto ni wako.

Una uhakika DNA itaonesha mtoto ni wake kwa sababu unahakika zinachakachuliwa. Sababu ya kwa nini zinachakachuliwa unaijua pia
 
Kama huna hamu na wanawake jitahidi kunywa supu ya pweza na pia karanga mbichi kwa wingi.. Hamu lazima ije
 
Inawezekana kabisa huyu mtoto ni wako maana umesema mkeo aliondoka June mwishoni. Si ajabu wakati anaondoka alikuwa tayari ni mja mzito hakustukia mpaka aliporudi na ukahesabu kuanzia huo mwezi wa June mpaka alipojifungua hiyo March ni miezi tisa. Kama una wasiwasi si vibaya kupima DNA lakini mwangalie mtoto kama ana kitu ambacho anashabihiana nawe kwa mfano kucha za vidole vya mikono na miguu basi unaweza kupotezea tu badala ya kuendelea kumshinikiza mkeo kwamba si ajabu amegegedwa na njemba alipokuwa safarini. Kila la heri kama hutajali usikose kupita mtaa huu kuleta mrejesho kama mtoto ni wako au la.

Kwamtazamo wangu hujasoma vizuri hii thread.

Amesema mwanamke aliondoka June an kurudi August. aliporudi walikaribishana kiuwana ndoa. baada ya wiki mbili mwanamke akamwambia ana mimba yake. baada ya miezi kadha jamaa akashika kadi akagundua mimba ni ya mwezi wa sita.

My Take : hiyo mimba sio ya jamaa:
 
Subiri mtoto akue ukapime DNA acha kulia lia siri ya mtoto anayejua ni mama.

dna bongo sishauri kabisa unless dr atakayefanya hicho kipimo awe ndugu yako au uzunguke nyuma ya pazia umwambie aje akwambie ukweli.huwa wanafanya hivi,kama wanamme wawili wanamgombania mtoto kuwa ni wao,huwa wanaangalia unafuu wa maisha uko kwa nani,au uwezo wa kimaisha uko kwa yupo,mwenye muonekano wa uwezo ndiyo atakayepewa mtoto.wao mahesabu yao ni kuepusha mtoto kuteseka na kukosa mahitaji muhimu.sina uhakika but wakienda kusimulia stori yao kuhusu huo ujauzito na kupima dna ts likely majibu yatakuja kuwa huo ujauzito ni wake,hii itakuwa kuepusha ndoa kuvunjika na pia kumuepusha mtoto na usumbufu usio wa lazima.kama unahitaji dna ya ukweli,fanya kama nilipoeleza hapo awali au jikoki hata hapo nairobi ufanye kipimo hicho
 
hiyo penalti kapiga mwingine kafunga ,,,,mtoto sio wako achana nae alizini huko alikokuwa.Usiogope kumuacha she is not innocent
 
umesema kasafiri miezi 2. Inawezekana alipata ujauzito kabla ya kuondoka ila hakujua kama keshapata. That is quite possible. Kuna wanawake wanakaa hata miezi mitatu hawajui km mimba imeingia

Ina maana hyo miez3 yote anaziona cku zake hku akiwa na mimba? Mpya hyo
 
Ina maana hyo miez3 yote anaziona cku zake hku akiwa na mimba? Mpya hyo

Yes wqpo wanaoona siku zao kwa kiwango kidogo cha flow wakodhani wako kawaida kumbe wana ujauzito. It happens to very few but it does. Na wapo wanaoona siku zao mpk wanajifungua na hawajui kama walikua wajawazito. Again very few experience this. Pamoja na kwamba wanakua wameshajifungua once or twice
 
Inawezakuwa siku anaondoka tayari alishanasa kwa hiyo kuwa mpole utaupata ukweli tuu
 
...mke wangu alisafiri kuanzia mwez wa sita mwishon na kurejea mwezi wa nane mwanzon.

Kama aliondoka mwezi wa sita mwishoni, huenda mimba ilitungwa kabla hajaondoka mkuu!

Ila sasa yani hakuona dalili katikati ya mwezi wa sita hadi nane?

Hapo tunarudi kwenye kuchanganyikiwa....
 
duh pole mkuu wanajf gharama za DNA na utaratibu wake ukoje ?make siku hizi watoto tunalea wengi wasowetu
 
Ila nimesoma makini tena. Mwezi wa sita mwishoni hadi nane mwanzoni manake miezi 2 haijatimia toka aondoke. Na kujifungua mwezi wa tatu manake mimba imetungwa wa sita.
 
Cha ajabu kipi hapo? Inawezekana aliondoka na ujauzito usiku ule mlioagana.
Ni vile tu hakuona dalili mapema.
Nina hakika DNA itaonesha mtoto ni wako.

Unataka kusema hiyo miez miwili yote aliyokuwa huko hakujua tu??Au unamaanisha aliendelea kuona cku zake huku akiwa na mzigo tumboni?
 
Mkuu wasiwasi ni hali ya kukosa imani au uhakika au bayana juu ya jambo, hali, tukio, jukumu linalokukabili...

Kutokuwa na uhakika wa kutekeleza wajibu ulio mbele yako huzua wasiwasi...

Machale au shuku ni hisia ya ziada ambayo humjia mtu pasipo kudhamiria yenye kumtambulisha hatari au tukio lisilo la kawaida lenye madhara au lisilo na madhara lililopo mbele yake...

Mtu anaweza akawa na wasiwasi lakini akakosa kuwa na machale...

Pia mtu huweza kupatwa na wasiwasi na machale pia, mtu huyu huitwa shujaa...

Unaweza ukapuuzia wasiwasi na kusiwe na madhara lakini huwezi kupuuzia machale maana kwa kufanya hivyo utakutwa na madhara...

Kwa namna ulivyoelezea matukio haya mawili, tukio la kwanza moja kwa moja linaangukia katika nadharia ya machale na hilo la pili kwa kuwa hujaweka bayana madhara yoyote basi linaweza likawa ni wasiwasi tu wa wahusika au machale pia...

kuna siku nilikuwa alitokea jamaa mmoja alikuja kumwona ndg yake ambaye ni mtuhumiwa aliyewekwa mahabusu yule jamaa aliomba ruhusa kwaaskar aliyekuwwpo pale akaruhusiwa kusalimiana na ndg yake jamaa ile anataka kuanza kuongea na ndg yake akaja askar mwingne akamwita yule jamaa, jamaa alipokuja akamwambia kuna kitu unacho mfukon mwako kitoe jamaa akaanza kusita askar akambana zaidi yule jAmaa likutwa na dawa flan ya unga kumbe alitaka ampe yule mtuhumiwa ili awatie giza askar awatoroke..... Na mwingne huyu kulikuwa na ujio wa kiongoz flan wa kitaifa sasa ktk maandalizi ya ujio huo sku ya ujio ilipofika kuna gari moja ikawa inazunguka maeneo hayo kila ikitaka kufuatiliwa ikawa inakwepa,wale jamaa ikabidi wabadilishe makao ya kiongoz huyo ila kwasiri.. . sasa ktk hayo matukio mawili ipi ni machale na ipi ni wasi wasi?
 
Wewe ndio hujasoma vizuri. Karudie kusoma tena ili uelewe kilichoandikwa.

Kwamtazamo wangu hujasoma vizuri hii thread.

Amesema mwanamke aliondoka June an kurudi August. aliporudi walikaribishana kiuwana ndoa. baada ya wiki mbili mwanamke akamwambia ana mimba yake. baada ya miezi kadha jamaa akashika kadi akagundua mimba ni ya mwezi wa sita.

My Take : hiyo mimba sio ya jamaa:
 
Akikuta ni wake hapo ndo itakuwa aman ya moyo wake na familia yake ....

Huwezi kupata amani mkuu wakati moyoni ulishajenga hekalu la wasiwasi...

Usidhani ni jambo dogo kujiaminisha kuwa mtoto aliye tumboni mwa mkeo si kazi ya kiuno chako...

Halafu kwa majibu tu ya madaktari ujikute umepata amani kwa kupokea majibu chanya ya DNA...

Utaanza kuishi kwa kujilaumu nafsi, dhamira itakusuta, lawama zitafurika nafsini mwako...

Ukiacha hilo bado mkeo naye ataishi akikosa amani nawe kwa kumdhania vibaya hapo awali...

Hivi ukimwona mtu anakuja maeneo ya nyumban kwako anazunguka zunguka bila sababu yoyote hapo utamhisi kivp? Utakuwa was wasi au machale?

Hapo ni dhahiri utakuwa na wasiwasi (kukosa bayana ya dhamira ya huyo mzururaji)...
 
ndugu zangu wa jf. salaam aleikum. ni mara yangu ya kwanza kujitokeza humu ndan kwa kutoa yaliyonisibu. naomba mnishauri wana jf. nimeoa na nimebahatika kupata mtoto mmoja.
mke wangu ni mzur na nimeish nae kwa aman. nimekuwa msaada kwa familia yake. nimewasaidia sana ndugu zake kwa kuwapa mitaji na wengine kuwasomesha mpaka elimu ya chuo.
tatizo lilianza mwaka jana mwez wa nane. mke wangu alisafiri kuanzia mwez wa sita mwishon na kurejea mwezi wa nane mwanzon. alipofika tulifanya mapenz kama ilivo ada kwa wanandoa. baada ya wiki mbili aliniambia kuwa anahis ana mimba. nikafurah as nilikuwa nahitaji mtoto wa pili.
hivyo nilimshauri aende akapime ili tuwe na uhakika tuanze kufanya maandalizi. baada ya kipimo kweli alionyesha ni mjamzito. nikafurahi na kuanza kufanya mipango ya kuweka akiba mahususi kwa ajili ya mambo ya ujauzito na hatimae mtoto.
baada ya miez mitatu nikamshaur aanze kuhudhuria clinic. akaanza na mambo yakaendelea vizur huku nikiendelea kulea mimba.
baada ya miezi kama sita hiv nikaamua kuchukua kad ya clinik ili nione maendeleo ya mke wangu na pia nijue kama kuna taarifa zozote hatarish kwa vile nilikuwa cjaiangalia tangu aanze clinic.
nilichokiona uko ndicho kilichonichanganya. kimenivuruga mpaka cjui nichukue uamuz gan. nilikuta taarifa kuwa mke wangu ana mimba iliyotungwa mwez wa sita na anategemea kujifungua mwez wa tatu mwaka huu.. niimuita na kumuuliza. alinijibu kuwa labda ma ness wamekosea. nilimwambia kuwa lazima nijue. nenda kapige utra sound. majibu ya utra sound yalionyesha kuwa kwel atajifungua mwez wa tatu.
alipima tena sehemu nyingine na majibu yalionyesha hivo hivo. nilitaman kumuua lakin niliamua kujipa moyo as mi ni mwanaume wa ukwel. yeye pia alisisitiza kuwa vipimo vimekosea ye anaamin kuwa alipata mimba mwez wa nane na atajifungua mwez wa tano na c vinginevo. akasisitiza kuwa hajazin. nikaamua kusubiri. ila nikamuahid kuwa nikigundua kuwa mimba co yangu ndo mwisho wa ndoa yetu. nikafanya utafit na kuongea na baadhi ya madoctors wote wanasisitiza kuwa akijifungua ndo ntajua ukwel. lakin pia kuna issue ya 2 wiki plus or minus. najua vizur as mi ni msomi na ni mzazi.
sasa tayar alishajifungua na ni mwez ule ule wa tatu na doctor anadai alijifungua on time. hakuchelewa wala kuwah. which means alipata mimba mwez wa sita wakat hayupo na mm. so kuna uwezekano mtoto sio wangu. lakin yeye ana insist kuwa hajawah kuzin na mtoto ni wangu. amesema hivo mbele ya mchungaji. sasa nimebaki njia panda. nimkubali kuwa mtoto wangu au niende nikapime dna. au nimfukuze. nivunje hii ndoa. nimechanganyikiwa. sijui la kufanya. yaan mpaka kazi zangu zote zinaharibika. nimevurugwa jaman naomben ushaur. nifanyeje.

Lea tu maana inaonekana huna maamuzi, sjui umelishwa nyama ya wapi?
 
Mkuu kama nimeelewa umesema alisafiri mwezi wa sita mwishoni!!! Kama ni hivyo,na mlikuwa mnakutana RELAX!!! Awezakuwa kweli mwanao huyo.
 
Back
Top Bottom