litutumbwe
JF-Expert Member
- Mar 13, 2023
- 731
- 1,376
Jamani wanajamvi wazima? Hapa kwangu ninaishi na baadhi ya mifugo,nimewajengea mabanda maalumu uani...
Sasa jana jioni tu kuku wangu alishambuliwa mno,na ndiyo nilikuta nyoka ameshaingia bandani.
Yaani alikuwa ameshamuua jogoo sasa anamnyofoa nyama anakula. Nilikuta kashamla robo tayari na anaendelea kumega mapande ya minofu.
Ama kwa hakika nyoka ni hatari,tulimuua kwa msaada wa kerosene pia. Mkoani nyoka wengi sana... Mabaki ya kuku tukayafukia.
Kuweni makini jamani. Na nasikia nyoka aina ya kobra huwa wanatembea mume na mke, mkewe tulishamuua na huyu ni mumewe.
Huwa anaweza kuingia hata kupitia upenyo mdogo wageti.kuweni makini mno
NB:nyoka huyu alikua anatafuna kabisa minofu aliyonyofoa kwenye mwili wa kuku. Hii inaonesha ata mtoto mdogo anaweza kumla. Tuwe makini