srinavas
JF-Expert Member
- Jun 5, 2011
- 4,149
- 3,862
Habari zenu wanajamvi ,
Nakuja kwenu kwa heshima nikiomba msaada wenu wa kisheria baada ya kutumika kwenye tangazo la kibiashara kwenye televisheni bila ya kupewa pesa yoyote na pia bila mkataba au makubaliano yoyote ,
Kwenye tangazo hilo mm ndio mhusika mkuu , kwa maana ya kwamba mm ndio naonekana sana na mimi ndie niliyebeba ujumbe mzima.
Tangazo hilo mpaka sasa linarushwa kwenye televisheni mbali mbali na pia hata kwenye mitandao ya kijamii kama you tube ,twiter na facebook.
Ombi langu ni kwamba ningependa kujua kama naweza kufungua kesi mahakamani na nikapata haki zangu za msingi..
Tafadhali naomba wadau wenye ujuzi na uzoefu kwenye maswala ya kisheria na maswala ya masoko na matangazo wanisaidie au waniambie tu japo kuwa naweza kufanya fanya vipi nikafanikiwa.
Natanguliza shukran za dhati..