Nimetongozwa mbele ya bwana wake

Joined
Apr 11, 2011
Messages
57
Points
70
Joined Apr 11, 2011
57 70
Wadau, wiki liliyopita nilikuwa moro kwa mambo yangu binafsi. Mishale ya saa tano nikatinga baa moja kupata maji ya ilala. Mezani nilipokaa nilikuwa peke yangu, kupiga funda tatu tu, jimama akajipitisha. Baada ya kufika mezani kwangu, akauliza kama anaweza kukaa, nikamwambia kaa. MWANAMKE KUMTONGOZA MWANAUME KAZI. Naye akajiagizia, akaanzisha mazungumzo fastafasta, lakini akiwa tayari kalewa, akajitambulisha yeye ni mwalimu, mc, ana undugu na mwanasheria mkuu wa serikali aliyestaafu (Mwanyika kama sijkosea), vile vile ni mjasiliamali, longolongo kibao. Wakati huo sijamaliza hata serengeti moja niliyojinunulia, akaniagizia. Nikashukuru ila nikamwambia mhudumu akae nayo kwanza maana ilikuwa ugenini na bado sijasoma ramani vizuri.

Awali nikahisi mwanamke yule ni chizi au ana frustration. Akanyanyua simu kumpigia mtu, huku sijui hili wala lile akaja mwanaume mmoja akamkwapua ile simu. Nikaanza kupata ramani ya vita. Jimama likaniomba angalau namba ya simu huku likidai hali ya hewa imechafuka, ikibidi nimpatie mhudumu ili ampatie, bado nazubaazubaa, yule mwanaume akarudi akamwaga pombe iliyokuwa kwenye grasi ya jimama na kufoka "kwani huku kwangu pombe zimeisha". Hapo nikahama meza.

Jimama hakuridhika, akamwachia maelekezo mhudumu amchukulie namba yangu, jimama akaondoka na bwana wake. Kufika mbele jimama akarudi bar, bwana wake akarudi kumchukua tena, ndio wakaondoka jumla.

NILICHOJIFUNZA
  • Hata wanawake wanajimwagia sifa wakati wa kutongoza
  • Wanahonga ili kutongoza
  • Ukiwa ugenini kuwa makini na kila mtu aliyekaribu yako
NB: Baada ya jimama kuondoka, nilimwambia mhudumu aniletee bia yangu ya ofa ya itokanayo na kutongozwa, japo nilikoswakoswa
 

Who Cares?

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2008
Messages
3,532
Points
2,000

Who Cares?

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2008
3,532 2,000
thread yako inatufundisha nini?..am so sorry to ask that na naamini hutochukia wala kujibu kwa jazba coz u r a great thinker..ahahahahahaaa thanx great thinker.
 

IGWE

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Messages
9,021
Points
2,000

IGWE

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2011
9,021 2,000
asee kastori katamu kweli.....mambo ya Morogoro hayo..hilo lilikuwa guberi guberi lol
mkuu kwani dom hayapo haya,...ingawa huyu mwanamke anaonekana ni mbabe kwa mmewe_nafikiri sababu ni ndugu wa mheshimiwa wa zaman,..wanaume wengine ni waoga na hasa inapotokea kaoa kutoka zile familia za mboga saba zinazotoka pande za masaki na ostabei
 

Preta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
24,216
Points
2,000

Preta

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
24,216 2,000
Mkuu muda huo nilikuwa bado sielewi, naona changa, kumbuka matukio yote hayo yalijiri ndani ya dakika 20 tu. Namba sikuchukua wala kumwachia yangu
ungemuachia bana....mwenzio alikupenda ujue....maskini mwanamke mwenzangu....dah ndo basi tena
 

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
35,165
Points
2,000

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
35,165 2,000
Haya haya tena ndugu watazamaji; Jimama ameondoka ila sasa Mdondozi wa mambo atueleze; baada ya kubadilishana namba za simu mbona hutuambii kama alikupigia au ulimpigia? mmmh huko siko mwaya nimeuliza tu!
 

Vaislay

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Messages
4,501
Points
1,225

Vaislay

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2011
4,501 1,225
huna jpya wewe hilo jimama baada ya kukumwagia CV ukalitamani na ndo maana ulidiliki hata kumpa namba yako na am sure unawasiliana nalo
 

Kaizer

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2008
Messages
25,249
Points
2,000

Kaizer

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2008
25,249 2,000
mkuu kwani dom hayapo haya,...ingawa huyu mwanamke anaonekana ni mbabe kwa mmewe_nafikiri sababu ni ndugu wa mheshimiwa wa zaman,..wanaume wengine ni waoga na hasa inapotokea kaoa kutoka zile familia za mboga saba zinazotoka pande za masaki na ostabei
Igweeeeee....umesahau kama Bunge limeisha mkuu, nimesharudi kitaa tayari, ila wakati nipo kule yalikuwepo kimtindo.....ila hapo almanusura jamaa angejilipua aisee
 

Forum statistics

Threads 1,391,496
Members 528,416
Posts 34,082,685
Top