Nimethibitisha ni kweli mke wangu kanisaliti

Nimethibitisha ni kweli mke wangu kanisaliti

Bro ukimchunguza bata Huwezi kumla.
Najuwa psychologically hautakuwa sawa hata miaka 50 ijayo, na uaminifu kwa mkeo utakuwa imekwisha hata aje akupigie magoti bado kumbukumbu itakuwepo tu!
Achana na huyo mwanamke na tafuta chombo kingine usijipe magonjwa ya moyo sbb hata maandiko matakatifu ktk Biblia yanasema " mwanaume hatamuacha mkewe ila kwa tendo la uasherati "

Moral lesson; Kama unapenda mkeo/mumeo usimfuatilie sana yatakukuta ambayo Hutaweza kuamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usichukue ushauri mwingine zaid ya hivi viwili nnavokutajia

1. Msamehe huyo mkeo kiroho safi na muendelee kutunza mtoto na usiwe na kinyongo tena la sivo autakua na amani moyoni

kama unaona ushauri wa kwanza aukai moyoni bas

2. Mpe talaka, as long as ushahidi tayar unao, kama moyo wako hautaridhia kumsamehe ili usije patwa na majanga mengine kama magonjwa ya moyo, stress ukapoteza dira ya maisha

Sent from my Redmi 3X using JamiiForums mobile app
 
Hivyo unavyovirefer kama vitabu vya waarabu havisemi hivyo. kavisome tena au omba usomeshwe
 
Pole sana. Siku ya pili baada ya kumuonya akatoa tam kwa jamaa. Swali langu ni moja... Ulipokuwa una "mchimba biti" uliongea maneno yepi?
 
Mm sitakushauri kitu kwakuwa majibu unayomwenyew. Ww ndio unamjua mkeo, ww ndio unajua unampenda vp,ww ndio unajua umeumia vp na hicho kitendo, ww ndio unajua kwamba utakuwa na iman naye tena au laa!
Hivyo fanya kile moyo wako unakutuma.
 
Ishu za mtoto kupata tabu hazina mashiko.ni wangapi wanazaliwa wanapoteza mama hapo hapo na wanakua fresh!?..Kikubwa mkuu huyo si mwanamke na ukiendelea kumng'ang'anie itakula kwako!.kwan hapo ulipo tayari umeshaingia kwa strees na hutakuja kuwa fit tena coz hlo ni donda la maisha na litakalo kutangukiza mbele za haki kama usipo simama kiume.Na shukuru muumba wako kwa kukuonyesha uchafu huo mapema.ukiendelea kumganda ndipo mungu huwa anasema tunaangamia kwa kukosa maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndoa yako ina miaka mingapi? Huyo muumba unayesema amshukuru kwa kumuonyesha uchafu wa mkewe umeshajua kwa nini amemuonyesha? Ni kweli tunaangamia kwa kukosa maarifa, na kumcha Mungu ndiyo chanzo cha maarifa, na mshahara wa dhambi ni mauti. Dhambi ya uzinzi kwenye ndoa isipotubiwa na kusamehewa itapelekea kifo cha ndoa na kifo cha mustakabali wa watoto na wanandoa kwa ujumla. Huu ni mtihani kama mwingine tu jamaa anatakiwa achukue kalamu ahangaike nao bila kuibia popote zaidi ya kwa Mungu afaulu. Huyu Massawe ni Mkristo na mwanaume wa kikristo anatakiwa kuwa mfano wa Yesu kwa kanisa ambalo ni mkewe. Kanisa ni dhaifu na linatenda dhambi kila siku na kila saa lakini Yesu hajawahi kusema wewe umejichafua sana sikusamehi. Badala yake huacha kondoo 99 na kumfuata mmoja aliyepotea. Anabisha hodi kila siku akitamani tumkaribishe Roho atuonyeshe madhaifu yetu tutubu ili tuweze kuimarika. Hatuwezi kupata vikubwa kwa kuzira na kukata tamaa wakati majaribu yapo hapa duniani kudumu wakati sisi tunapita.

Massawe limekupata gumu lakini liko ndani ya uwezo wako kulishinda. Huyo wifi hajashindikana huyo. Unavyosali "....utusamehe dhambi zetu kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea...." ndo ujue maana yake leo. Usipomsamehe mkeo na wewe ukome kusali na kutegemea majibu ya maombi. Daudi - a man after God's own heart alikuwa dhaifu eneo hilo na lilimletea madhara makubwa kwenye familia lakini aliungama na kuomba msamaha. Nabii Hosea alikuwa na mke kicheche hatari akaamua kumuacha na yule mke akafanya uzinzi wake kwa uhuru hata akapata watoto huko lakini Hosea aliambiwa amrudie mkewe achukue na wale watoto waliopatikana huko nje. Sina nia ya kuhalalisha uzinzi miongoni mwa wanandoa ila tujue si jambo geni na inawezekana kurejesha ndoa iliyokufa kabisa sembuse iliyotingishwa kidogo? Na nimesema hivi kwa sababu mdau amesema watu wa Mungu tunaangamia kwa kukosa maarifa. Maarifa anayosema Mungu ni maarifa ya Kimungu yanayotuwezesha kufanya vitu vya kimungu kama kusamehe na kupenda tena na tena. Mimi nakuombea uvuke salama.
 
Kwa mtu asopatwa na hili Janga hawezi elewa maumivu yako kwa sasa mkuu...wanawake hawanaga udhamana mkuu.
 
This is sooooooooooooooooo right, kuwaacha Wazee, tu deal na matatizo yetu. Kama jamaa anataka muacha, alale mbele kimya kimya, sio kumuaibisha mke wake, au kusumbua wazazi, na kama anataka kukaa naye, apige kimya, Kuja jamii iwe imetosha, MI ANAUME HUWA MIJINGA, ATAJIAIBISHA WEEEEEE THEN ATAENDELEA KUISHIA NAYE, THEN WATU WAKIMSEMA ANALALAMIKA!
Kumuaibisha make wake!!.Hutu tayari kajiaibisha,Atakapo muacha no lazima awaeleze wazazi wa pande zote sababu hasa za kutengana.Kuhusu wazazi na nduguze kujua uchafu huu in suala ambalo hatawahenga wanaliunga mkono walisema "mchuma janga hula na wakwao".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee hii ngumu mno, ila mimi ntajiongelea nafsi yangu. Siku nikigundua mke wangu katoka nje ya ndoa ntampa talaka yake bila kuchelewa. Katika suala ambalo sitopokea ushauri wowote ni hili, wakati nipo chuo nlikuwa na demu flani ambae nlikuja gundua anagawa tunda na iliniuma mbaya ikanihunt for months sasa sikwambii mke. Yaani simple sana mkuu, mpe talaka tafuta mwengine mtoto atakuwa tu wala lisikupe mawazo hilo.
 
brother mm nipo very strict na nimeshamwambia nikigundua umenusaliti ndio mwisho Wa ndoa!!labda nawe km unachepuka ila km huchepuki yy ndio kafanya hivyo no discussion goodbye tu!!siwezi kuvumilia usaliti huo
Oya mkuu hii lazima tuelewane, hata kama na wewe unachepuka. mwanamke akichepuka out aisee, hata kama mtasema mimi ni dikteta sawa tu lakini hata kama na wewe ukichepuka yeye akichepuka anatembea. hakuna habari ya haki sawa hapa
 
Hatorudia hiyo tabia kama Akili zake ni timamu ila utaumia saba, hilo donda huwa haliponi mpaka unakufa na mapenzi hayatikuwa kama zamani kwa upande wako japo Yeye atakuwa na mapenzi ya hali ya juu.Moyo wako umeshapata dosari naye.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ikiwa alizungumza naye Leo akamuonya lakini kesho take akaenda kuliwa unasema hotorudia?
Iko hivi jamaa akisamehe huyo mke atajua amesamehewa for the sake of mtoto wao,atakachofanya atamzalia jamaa watoto/motto mwingine ili kupunguza chances za kuachika (kamaa jamaa alishindwa kumtaliki akiwa na mtoto mmoja kuwa mtoto atapata shida obvious hotoweza wakiwepo watoto 3)then baada ya hapo jamaa ataisoma plate namba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujawafahamu wanawake hata 56%!endelea kumtisha utaona majibu yake!mwanamke ukiwa unamtishatisha ndo unamtuma ndugu yangu!we mwambie tu madharaya kuchepuka basi endelea kujifanya afande sasa!mwakani utakuja hapa unalia lia
Kwani ni kutishana? ni ukweli unamwambia, nikiwa sijagundua sawa lakini siku nitakayogundua ndio tumemaliza hapo. sote tuna wake ndugu yangu na wala hatishwi mtu, wewe ruka ruka huko lakini ujane unakusogelea
 
Kwani ni kutishana? ni ukweli unamwambia, nikiwa sijagundua sawa lakini siku nitakayogundua ndio tumemaliza hapo. sote tuna wake ndugu yangu na wala hatishwi mtu, wewe ruka ruka huko lakini ujane unakusogelea


aaahhhh haya mkuu
 
Ndo upuuzi gani huu umeuandika hapa we jamaa...hivi unaujua uchungu wa mke kweli wewe?
Ngoja siku wakotombee na wewe halafu uje hapa utuandikie maloloso yako hapa.

Haya maumivu hata wahenga waliyajua ndo maana wakawa wanawatahiri vijana wao bila ganzi ili kuwaandaa na maumivu kama haya. Walikuwa wavumilivu kweli kweli. Ukisikia kesi imepelekwa kwa wazee ujue ni ile wanayosema italeta laana kwa hiyo inabidi wazee wakaisihi miungu kwa kafara. Mimi na wewe tuko tofauti ndo maana umeona maloloso na naheshimu mtazamo wako.
 
Back
Top Bottom