Nimetengeneza 15,632,000/= kwenye betting ndani ya miezi minne

Mm binafsi nimekuwa active kwenye kubet tangu mwaka 2017 mwanzoni ila kabla ya hapo sikuwa kubet kabisaa na ukae ukijua mm sio mshabiki sana wa mpira hata ukipanga kikosi uwanjani unambie nioneshe namba tatu au nane mm sijui kwa kwel

Nilianzaje kubet?
Kipindi nipo chuo niliuwa nawatembekea jmaaa zangu nakuta maghetoni wanakula vizuri kipindi mm boom limekata nikawakuta na mikeka ya makaratasi yan premer bet na mm nakumbuka siku iyo nilicopy mikeka kama 12 iv kwa jero jero ila sikula hata mmoja ikawaga ivyo kila nikitoka chuo naenda kukopi mikeka kusema ukwel ni mchezo wa bahati niliwai shuhudia jamaa anahakikisha mkeka alishinda 8.7M kwa jero tu ndio nikaamin kama kwel pesa ipo, ila narudia ni mchezo wa bahati

Basi mm nikaachaga kubet uko kwenye karatasi kwasababu ya muda nikaanza kubet online nikafungua acc premer kipindi iko jmaa zangu hawajui sana kuhusu online coz wao walikuwa karibu na vibanda vya kubet alafu wanaona uvivu kutumia na bando juu

Nikaanza kwa kutafuta platforms zinazotoa predictions pamoja na head to head mwanzo nilianza kukopi predictions zao ila nikawa si shindi
Ikumbukwe mm huwa na sukaga majamvi ya timu kumi kwenda mbele na stake yangu imezidi ni buku mbili
Mwanzo nilikuwa nabet kila itwayo leo
Baada ya kuona napigwa sana kwa kukopi predictions nikanza kuangalia mwenyewe head to head na chambua vizur labda zimekutana mara tano uyu kashinda mara tatu zote akiwa home na leo tupo home basi mm nampa uyo au kila wakikutana hawatoi magoli zaidi ya matatu basi naeka under au wakikutana wanafungana sana naeka both time to score nikawa nimepata njia nzuri sasa unakuta naeka mkeka hata timu 17 inaharibu moja stake ni mwisho buku mbili hapo ndo nimeeka kubwa, badae nikawa nikawa nabet weekend tu yan jmos na jpili.

Mara ya kwanza kushinda ilikuwa mwezi kama watatu iv iyo 2017 nilieka timu 15 moja haikucheza siku iyo nikashinda milioni moja na elfu 19 kwa stake ya jero tu nikaamin kama kwel kuna pesa nakumbuka jamaa zangu wengi sanaa waliansa kubet kipindi iko wengi waliacha njiani wachache bado wapo na baba yetu wa hiati(kanji)
Kama wiki tatu badae nikashinda tena laki tatu kwa 25000 timu zilikuwa nane
Tangu nianze kubet sijawai pata hasra kwasababu na stake kidogo alafu nabet weekend tu mikeka miwili kila weekend

Sasa iv nataka niwe natafuta odds 20 tu nipunguze timu naamin ntafanya poa sana

Betting ni mchezo wa Bahati sanaaaaaaa ila kuna njia za kuongeza bahati
1. Stake kubwa timu moja ukizidi tano
2. Usibet direct win bet magoli kwenye magoli kuna options nyingi sana
3. Usiwe na tamaa ya kuongeza odds au stake pia jiekew limit sio kila siku unabet tu
4. Ukibet usifuatilie matokeo kaa mbali na mikeka yako ili usipate hamu ya kupandilia mikeka kama utachanika mm iyo inanisaidia sana nikibet nakuja kuchek mkeka keshoo yake mara nyingi sibetii timu kubwa na bet timu ambazo hata kanji hazijui
5. Pia fanya analysis kwanza kabla ya kubet japo ni mchezo wa bahati ila historia inajirudia

Asikudanganye mtu betting inalipa sanaaaaa kama unamtaji kama alivyofanya mleta mada,

Alafu betting sio utapeli ni kitu cha halalo utapeli ni izo tatu mzuka na kina biko. Mana betting unampa arsenal unaoba kabisa kapigwa inamna ulikosea
Pia tunalipa kodi kwenye kubet tena nyingi sana kama jamaa hapo amelipa pesa nyingi sana zaidi ya hata ya milioni 5

Huu ni mfano tu wa mkeka nilishinda mwezi wa kwanza hapo

View attachment 1083576
Iyo bonus unayoona ndio kodi ambayo nimekatwa hapo nilieka 2200 nikashinda laki nane kasoro kama buku tano

Ningetuma mikeka mingine niliyowai shinda sema nimebadili simu na uku ishafutikaga mwaka 2017 na 2018 ulikuwa mzuri kwangu ilikuwa karibia kila mwenzi nashinda mkeka kuanzia kiasi cha 300k kwenda juu, hii nikutokana na njia yangu ya kueka timu nyingi ni ngumu sana kushinda ila mwaka huu umekuwa mgumu kidogo
Duh ....very tempting. Huwa natamani kuwa karibu na watu km nyie nitembelee nyota....timu 10+? Hii kitu ni ngumu imenishindaga aisee...
 
unaona sasa mkeka umechanika!!
Ndomana nimesema 'naona chelsea' anashinda sio 'chelsea lazima ashinde', chochote kingetokea pale na kama kusingekua na sare united alikua analala .. halafu pia maelezo yangu nilisema upepo ulikaaga safi kama wiki mbili, ila all in all siwezag na sitaweza bet magoli maana nikifanyaga hivyo napigwa vizuri labda nitembelee nyota ya mtu ..kiufupi nimeshinda mara nyingi ila sio kwa double chance wala magoli (not my favourite options).
 
alafu kuna mabata yanakazana ooh tuache kubet...tufanye kazi...hayo mambo ya kufanya kazi kwa juhudi ni industrial age ndo ilikua ufanye kaz sana upate hela sana..sasa ivi this is information age...watu wanaobet kama kaz wana mawe mbaya...mshahara wa profesa unaingizwa kwa dk 90..mama...eee

Juma mpemba unadharau sana kwahiyo sisi tunaotaka kuwa ma propesa bado unatuhakikishia hatutakuwa na pesa
 
Hhahaha...Noma sana asee...Hata mtu ukila kwa muda fulani, utakuja kuliwa muda fulani...unaweza jikuta umpigwa au ngoma Droo.

Sasa ukijiuliza muda, presha balaaa...ukiwa laini laini magonjwa ya moyo, presha nje nje.

Unaweza kuangukia ama ulevi ili kupunguza mawazo ya ulovyoliwa.
hasara roho pesa makaratasi.
kamari ni mchezo ya kujifurahisha.
kamari itakuwa mbaya kama utaifanya kuwa chanzo cha mapato yako.
 
Kuuza tips una guarantee ya profit.., siku wakiliwa ni jamaa wameliwa na wewe chako umechukua siku wakipata ndio furaha yako sababu na kesho watarudi ..., win, win situation
Sasa Ndugu,
Huoni jamaa sometimes anacheza singles?
Sio lazima ucheze behewa.

Pili kama unauza tips wanunuaji wako wakapoteze hapo win win situation iko wapi?
 
Hujui unachoongea mkuu sure odds hakuna kitu kama hicho kuna sure bets maana yake ni sports arbitrage unatumia odds za kampuni tofauti mbili ambazo odds zake ni zaidi ya 100 percent unabet kampuni hii kiasi fulani timu A kushinda na Kampuni nyingine Timu A kushindwa hence no matter the outcomes unashinda pesa

Tatizo letu binadamu kitu ambacho hujui ukiambiwa unaona mtu anakusema vibaya badala ya kuuliza huenda ukajua kitu.., nobody knows everything and even a Genius asks questions..., na kila anayekwambia kitu sio negativity bali ana mtizamo tofauti kwahio jibu kwa Hoja kwanini betting ni long term business..

huwezi kulinganisha risks involved kwenye kilimo a betting..., odds za ukilima sehemu yenye mvua nyingi, na uwezekano wa kumwagilizia propability ya kupanda mchicha ukavuna bangi sio sawa na probability ya kubet mfano Barcelona msimu mzima kwamba wanashinda the reality is mwenye kubet mwisho wa siku atalia
Hili linawezekana kwenye michezo ambayo kuna sare Kama vile mpira wa miguu. Hapo timu moja yaweza kuzidi 2odds, na ya pili nayo ikazidi 2odds but what about sare??

Pili usidhani Hawa jamaa (bookies) hizi odds wanajitungia tu, nao wananunua pia, na mara nyingi odds hukaribiana au kufanana. So ni nadra sana kukuta bookie mmoja kampa Chelsea Odds nyingi against Man U then mwengine akafanya tofauti.
 
Husifikiri local mkui.. Unajua kwamba ligi kuu Tanzania bara kupitia kampuni moja ya Eastern Europe yenye wawakilishi wake hapa bongo inaruhusu kubet game za ligi kuu Tanzania bara na unaruhusiwa kustake hadi million 50 per single bet ya bongo. Did you know that!?
Not in a million years, si useme ni kampuni gani? Au wana operate kwa siri?? Narudia tena hakuna hakuna!!
 
Sasa Ndugu,
Huoni jamaa sometimes anacheza singles?
Sio lazima ucheze behewa.
short term as a leisure kwamba nimeona hii team bookies wameipa odds ambazo sio za halisi unaweza mtu kuweka wager as a leisure; ila kumbuka kwenye kitu unpredictable its hard to do over a long term ukizingatia mwenye mchezo amekupa a wrong end of the stick..., kujikwaa ni kwingi sana hususan kama wagers zako ni kubwa na sio financially tu hata kwa afya

Pili kama unauza tips wanunuaji wako wakapoteze hapo win win situation iko wapi?
Mkuu ndio maana mganga huwa anapata pesa; mtoa tips hakwambiii utoe pesa kiasi gani, tena mara nyingi anatoa tips za singles, pili ukishindwa unasema bahati mbaya ukishinda unarudi unamlipa, ukishinda wote mnashinda.., ukishindwa yeye anashinda..., you win he wins; you lose he wins
 
Hili linawezekana kwenye michezo ambayo kuna sare Kama vile mpira wa miguu. Hapo timu moja yaweza kuzidi 2odds, na ya pili nayo ikazidi 2odds but what about sare??

Pili usidhani Hawa jamaa (bookies) hizi odds wanajitungia tu, nao wananunua pia, na mara nyingi odds hukaribiana au kufanana. So ni nadra sana kukuta bookie mmoja kampa Chelsea Odds nyingi against Man U then mwengine akafanya tofauti.
cheki hapo juu kuna link nimetoa ya oddsportal kuna suggestions wanatoa za sure bets kila wiki bure..., ukishaona kabala haujafurahia kwamba umepata a gold mine nistue pia hapa hapa nikwambie even this though theoretically ni true ila na yenyewe ina hatari zake kubwa tu...,

mfano cheki hapo

1X21X2Profit
Premier League
03/05
14:00
Yenisey - FK Anzi Makhackala
1.65

4.40

7.80
4.0%

https://www.oddsportal.com/sure-bets/

Jamaa yako alisema nikimwonyesha popote pale atanipa 100K tangu jana nimemuonyesha nashangaa bado kimya sijui hajaona
Wall street
 
Back
Top Bottom