Jinsi kamari (betting) ilivyonipotezea shilingi laki 6 ndani ya siku 60 tu

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,531
3,331
Ahlan wa sahlan.

Leo naomba niongelee experience yangu fupi katika betting (Kamari).

Binafsi, mimi ni mmoja wa watu waliokuwa wanaipinga sana michezo ya Kamari, maarufu kama betting. Ila kutokana na upweke (boredom) pamoja na udadisi (curiosity) wa kutaka kujua nini kipo nyuma ya michezo hii ya kubahatisha nikajikuta nimeweka pesa kwenye simu yangu nikaanza kubeti. Nilikuwa sijui A wala B kuhusiana na masuala haya, Ila kutokana na kielimu nilichojaaliwa kidogo halikuwa jambo zito kwa mimi kuanza kufaham terms mbalimbali kuhusiana na betting pamoja na masoko na mbinu zake.

Nilianza na single bet, nikashangaa baada ya dk 90 matokeo yakaja nimeshinda.. nilipata profit ya zaidi ya 3,0000/= nikajisemea mchezo ndio huu wa kupata pesa fasta fasta. Sikuitoa ile pesa kwenye simu akili ikanituma niendelee kubeti mechi nyingine.

Nikawa nakula baadhi na nyingine naliwa, hali ikaenda nikawa sasa mzoefu kuhusiana na betting. Masoko yote nayajua, mbinu mbalimbali za kubeti nazijua, pia nikawa member wa uzi wa kubeti humu JF.

Hali imeenda kwa miezi 2 sasa. Nimejikuta nazama katika uraibu kidogokidogo umekuwa sio ule mchezo wa kucheza kwa fujifurahisha tu bali umekuwa ni mchezo wa lazima kwangu. Kiasi naweza kushinda siku nzima napanga mikeka tu, huku ukizingatia kuwa sasa hivi tumerahisishiwa kubeti kiganjani kwa kutumia simu.

Hivi karibuni nimekaa nikasema ngoja nicheke bet history yangu, nikachukua na calculator nikaanza kupiga hesabu kiwango nilichocheza kwa muda wa miezi miwili. La haula nimejikuta nimepoteza zaidi ya sh laki 6 (600,000).

Ni kiwango kidogo kwa mwenye pesa na pia ni kiwango kikubwa kwa asiyekuwa na pesa. YES! Laki 6 zimeteketea ndani ya miezi 2. Mbaya zaidi hata ikitokea nimeshinda beti bado ile pesa naona nisiitoe kwenye account yangu ya betting badala yake niendelee kuizungusha kitendo kinachopelekea kuipoteza yote.

Ukiachana na jambo la kupoteza pesa kizembe, betting imenilete depression (msongo wa mawazo) pamoja na kuharibu mahusiano yangu kifamilia na kijamii. Kiasi muda mwingi nakuwa busy na simu yangu tu bila kujali familia inayonizunguka mke na watoto.

Experience niliyoipitia katika miezi hii miwili sitaki mtu mwingine aipitie. Uraibu wa kamari una nguvu sana kuliko uraibu wa sigara. Ni ngumu kwa mvuta sigara kutumia sh 600000 kununua sigara na kuzivuta zote kwa kipindi cha miezi miwili ila kwenye betting ni jambo la kufumba na kifumbua tu.

Wosia wangu kwa vijana ni kuwa KAA MBALI NA KAMARI IKIWA UNATAKA KUFANIKIWA. KAMARI (BETTING) SIO MCHEZO WA KUKUPATIA KIPATO. BALI NI MCHEZO WA KUKUTIA UMASIKINI.

Pia jambo lolote baya usipende kulidadisi ubaya wake, kuna mambo mengine mabaya ukishaingia kuyadadisi ili kujua kwanini ni mabaya utajikuta umenasa humo, mfano ni madawa wa kulevya, kamari, pombe, uchawi, zinaa n.k Wazungu wanasema "Curiosity kills the cat". Kuna vitu humu duniani havidadisiki. Ukiambiwa jambo kwenye vitabu vya dini kuwa ni ovu na ni baya usilisogelee kaa nalo mbali sana. Otherwise utakuja kujuta.

Imagine ndani ya miezi miwili nimepoteza zaidi ya laki 6, je ndani ya mwaka mmoja ningeenda kupoteza zaidi ya kiais gani? Binafsi sijutii kiasi cha pesa nilichokipoteza ila ninachojuta zaidi ni hii hali ya uraibu (addiction) inayoelekea kujijenga ndani ya kichwa changu.

Je, wewe msomaji nawe unasumbuliwa na tatizo la kubeti (kucheza kamari) kama ndio share basi hapa tuweze kusaidiana.
 
Na hii shilingi laki 6 ni hesabu ndogo tu niliyoifanya katika betting zangu za mchezo wa football tena kwenye kampuni moja tu ya betting bado sijapiga hesabu ktk virtual games ambako nako nimepoteza pesa nyingi tu.

Na pia sijapiga hesabu kwenye kampuni nyingine ambazo nimeshazitumia sana kubeti ndani ya hii miezi 2.
 
Usitupangie we umepoteza laki 6 kwa miez 2 watu tupo ndani ya hii game kwa miaka 5 na kuendelea sema kama vip niwe nakupa odds za uhakika.
Soma vizuri post...nimesema kuwa sijutii pesa niliyoipoteza ila najutia huu uraibu. Kiasi siku haipiti pasi na kuweka mikeka. Ambayo obviously ni loss.
 
Ila vipigo tu, tunapata. Ila hatukomi.
Juzi kati nikajisemae sasa nicheze odds 3 niweke 2500 nipate 10k. Nikafanikiwa kuipandisha ile pesa mpaka ikafika 110k. Nikaitoa. Kwa sasa kila nikiweka, napigwa. Nikama nishairudisha kwa kanjibai ile niliyopata.

Ila sikomi. Sitaki yangu ni 1000-2000. Kama nimekunywa bia tu.
 
jamani wakamaria kuna mpuuzi mmoja kaja kuunguza picha huku kisa eti kaliwa ka laki sita.... watu tunaliwa pesa ya maana na tunakula pesa ya maana wewe unalia lia hicho kidogo
 
Ila vipigo tu, tunapata. Ila hatukomi.
Juzi kati nikajisemae sasa nicheze odds 3 niweke 2500 nipate 10k. Nikafanikiwa kuipandisha ile pesa mpaka ikafika 110k. Nikaitoa. Kwa sasa kila nikiweka, napigwa. Nikama nishairudisha kwa kanjibai ile niliyopata.

Ila sikomi. Staki yangu ni 1000-2000. Kama nimekunywa bia tu.
Soko la kamari ni kama la mihadarati tu, wafanyabiashara (bookies) wanajua wana utitiri wa walaji (punters)
 
jamani wakamaria kuna mpuuzi mmoja kaja kuunguza picha huku kisa eti kaliwa ka laki sita.... watu tunaliwa pesa ya maana na tunamkula pesa ya maana wewe unalia lia hicho kidogo
Soma post uielewe madhumuni yake. Na kuliwa sio sifa sidhani kama kuna punter yeyote anabet kwa lengo la kwenda kuliwa
 
Ukiachana na jambo la kupoteza pesa kizembe ,betting imenilete depression (msongo wa mawazo) pamoja na kuharibu mahusiano yangu kifamilia na kijamii.Kiasi muda mwingi nakuwa busy na simu yangu tu bila kujali familia inayonizunguka mke na watoto.
Hapa Kamanda Sirro angetumia msemo wa kijana wa hovyohovyo.

Pole sana mkuu. Kujua tatizo ni hatua kubwa sana ya kulitatua.
 
Back
Top Bottom