Nimetembelea shule inayoitwa 'Indian School Dar es Salaam'. Nimegundua wahindi wametuzidi akili sana

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Habari wadau.

Leo nimetembelea shule ya msingi na sekondari inayoitwa Indian School iliyopo kurasini Dsm.

Dhumuni la kutembelea ilikuwa kujua utaratibu wao; mtaala gani wanafundisha na gharama za ada kama nikitaka mwanangu aende akasome hapo.

Baada ya kufika nilipokelewa na wahindi tupu. Yaani shule nzima kuanzia wanafunzi mpaka walimu ni wahindi tupu. Sikuona mwanafunzi mweusi hata mmoja.

Ada yake kwanza ni around milioni 10 kwa mwaka bila usafiri (hiyo chekechea tu na msingi madarasa ya chini). Na sylabus inayofundishwa ni ya India. Yaani mitihani wanayofanya hapo wanapomaliza ni mtihani wa taifa wa india. Ni sawa kuwe na shule inayoitwa Tanzanian school ijengwe india ama marekani then necta wawe wanapeleka mitihani yao ile ile inayofanywa na shule zote Tanzania.

Mazingira ya shule ni mazuri sana na hata macho yanatambua kwamba shule ni quality ya juu.

Maelezo yao ni kwamba shule hii imejengwa hapa dar es salaam sababu ya kusaidia indian expart wanaokuja na familia zao wasipate shida pa kusomesha watoto. Na mtaala wameweka wa india sababu ndio wameuzoea.

Nikawaza je wa Tanzania ama Serikali ya Tanzania tuna uwezo wa kuweka shule yetu ya necta nje ya Tanzania. Na mitihani tukawa tunawapelekea

Kwanini nasema wametuzidi akili?

Nasema wametuzidi akili sababu Kwenye hilo Jambo kuhusu elimu yao walilolifanya! Yaani kuweka mazingira ya kizazi chao kiendelee kupata Yale ya nchini kwao hali yakuwa wako nchi nyingine.
 
Kuna waalimu waafrika hapo ila kabla ya kufundisha wanawatrain pia hata wanafundishwa kuzungumza kiingereza chenye lafudhi ya kihindi.
Kuna nyingine pia wanafundisha masomo kidogo na sports kwa sana watoto baada ya muda mfupi wanaenda nje kuendelea na sports. Waafrika wapo ila wachache.
 
Sioni kwa kufanya hivo wametuzidi akili kivipi. Wahindi nimefanya nao kazi sana.

Nikuhakikishie tu kwamba wengi wao pia ni vilaza. Ila pia kama kawaida kuna vipanga.

Walichotuzidi zaidi ni English tu ila kwingine tupo level, naongea hivi nikiwa nimesoma mtaala wa elimu wa kitanzania kuanzia vidudu
 
Sioni kwa kufanya hivo wametuzidi akili kivipi... wahindi nimefanya nao kazi sana..

Nikuhakikishie tu kwamba wengi wao pia ni vilaza. Ila pia kama kawaida kuna vipanga.

Walichotuzidi zaidi ni English tu... ila kwingine tupo level, naongea hivi nikiwa nimesoma mtaala wa elimu wa kitanzania kuanzia vidudu

Kuweka shule yao ndani ya nchi ambayo sio yao ni kipimo cha akili. Je Tanzania tuna shule yeyote nje ya Tanzania inayopelekewa mitihani ya necta?
 
Kuweka shule yao ndani ya nchi ambayo sio yao ni kipimo cha akili. Je Tanzania tuna shule yeyote nje ya Tanzania inayopelekewa mitihani ya necta?
Tanzania hatufanyi hivo ndio kwa sababu hatuna sababu ya kufanya hivo kwa sababu hatuna expatriate wengi wa kitanzania wanaofanya kazi nje ukilinganisha na wahindi....

Kwahiyo wahindi kuwa na shule yao hapa sioni kama ni kipimo haswa cha akili..
 
Sioni kwa kufanya hivo wametuzidi akili kivipi... wahindi nimefanya nao kazi sana..

Nikuhakikishie tu kwamba wengi wao pia ni vilaza. Ila pia kama kawaida kuna vipanga.

Walichotuzidi zaidi ni English tu... ila kwingine tupo level... naongea hivi nikiwa nimesoma mtaala wa elimu wa kitanzania kuanzia vidudu
Mkuu tukatae tukubali wahindi wametutangulia kwa mfano pamoja na kuwa US kwa mfano kuna wahamiaji kutoka afrika wengi lakini si wengi wapo kwenye nafasi za juu kwenye MNC na International org.

Hapa nazungumzia mfano Google unamkuta Sundar Pichai, Nenda Pepsico kuna yule mmama wa kihindi, nenda USAID alikuwepo Rajiv, Nenda IMF napo kuna muhindi yule lecture wa harvard, Harvard kuna course inaitwa financial engineering aisee wamejaa wahindi, mkuu wa dep inayotoa hiyo course ni mhindi tena wale black, kwenye engineering, IT, medical, bness wamejaa tena wale vipanga wa kufa mtu.
 
Mwandishi huna akili. Au zipo kidogo. Mimi naifahamu hiyo shule sijaona ambacho wametuzidi sisi wenye akili, akili. Ila wewe ambaye unazo kidogo unaona wamekuzidi akili. Hakuna cha ajabu hapo.
 
Mkuu tukatae tukubali wahindi wametutangulia kwa mfano pamoja na kuwa US kwa mfano kuna wahamiaji kutoka afrika wengi lakini si wengi wapo kwenye nafasi za juu kwenye MNC na International org. hapa nazungumzia mfano Google unamkuta Sundar Pichai, Nenda Pepsico kuna yule mmama wa kihindi, nenda USAID alikuwepo Rajiv, Nenda IMF napo kuna muhindi yule lecture wa harvard, Harvard kuna course inaitwa financial engineering aisee wamejaa wahindi, mkuu wa dep inayotoa hiyo course ni mhindi tena wale black, kwenye engineering, IT, medical, bness wamejaa tena wale vipanga wa kufa mtu.
Kuna waafrika kibao kwenye hayo makampuni na taasisi kubwa tatizo ni kwamba hatupendi ku-appreciate vya kwetu.
 
Sioni kwa kufanya hivo wametuzidi akili kivipi... wahindi nimefanya nao kazi sana..

Nikuhakikishie tu kwamba wengi wao pia ni vilaza. Ila pia kama kawaida kuna vipanga.

Walichotuzidi zaidi ni English tu... ila kwingine tupo level... naongea hivi nikiwa nimesoma mtaala wa elimu wa kitanzania kuanzia vidudu
Wahindi wamesharusha mpaka satellite angani wana agni 5. Wewe unayesema tunalingana nao labda kwenye kuwa na makalio kwamba wao wanayo na wewe unayo.
 
Kama ulikuwa unataka tu Kujimwambafai (Kujipalilia Minyama) kuwa nawe Unasomesha Mtoto Shule ya Gharama ya Wahindi Koko hao na kwamba una Hela (Umeukata Kimaisha) wala hukuwa na Haja ya Kuzunguka njia ndefu hivi (kwa Maelezo yako haya marefu) bali ungesema tu Moja kwa Moja na tungekuelewa sawa?
 
Back
Top Bottom