Consigliere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 12,037
- 24,595
Hicho ndiyo wengi wasichokijua. Wanasoma vitabu ili ku tally kwamba amemaliza kusoma na matokeo yake kumbe anazidi kuwa mjinga na msimuliaji.Sina uhakika kama 7 habits of highly effective people ama Mastery....unaweza ukasoma kwa wiki mbili naukavimaliza....lakini cha pili ni kwamba issue sio kusoma tu kama gazeti issue ni kusoma na kujifunza na ikiwezekana kukumbuka.....itakuwa na maana gani kama tukikuuliza kitabu no flani kilisema nini ukawa hukumbuki......Tatu umefocus kwenye vitabu vya aina isiyozidi 4, vitabu vingi unavyosoma ni vya personal development, investment na politics kidogo....vitabu vya mambo mengine kama afya, biographies za watu sijaviona....wakati afya ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya mtu.....ni muhimu kuchanganya vitabu vya aina nyingi ili kupata different perspectives.....kujua field nyingine wanawaza nini n.k
Hicho kitabu ulichokitaja cha 7 habits of highly effective people mimi ninacho mwaka wa 14 huu bado sijakimaliza, sababu kuna vitu unavisoma, unspaswa kuvielewa kwa kufanya ulinganifu na vingine inabidi kuviishi, inaweza ikakukula zaidi ya mwaka ukiifanyia kazi Chapter moja tu. Lengo la kusoma ni ili kutafuta au kuongeza maarifa ili tufanye maboresho maishani au tuanzishe projects, siyo ili kuwatajia watu idadi ya vitabu ulivyosoma au kusimulia ulicho kisoma.
Kusoma vitabu ni Project, binafsi ninashangazwa sana na huu ukasuku ulioibuka hivi sasa.