Nimesitisha rasmi kuchangia harusi

Hivi kwa nini watu hupanga kufanya mambo ambayo hawana uwezo nayo na mwishowe wanaishia kuwa kero tu kwa wenzao?

Kwani hawawezi tu kufunga ndoa bila makeke kama uchumi hauruhusu?

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Mimi sijachangiwa, sitachangiwa, na nitachangia ninapojisikia.

Waswahili walisema "Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba".

Naona hata harusi inageuka msiba.

Jamii yetu inabidi ijikite katika kujutegemea zaidi. Watu waanze kujiandaa wenyewe katika gharama za harusi, kama kuchangua watu wachangie token, kwa hiyari. Sio wanafanya mchango kama kiingilio cha harusini.

Pia, harusi ya kifahari si lazima. Watu wafanye harusi kwa uwezo wao. Sio ynafanya harusi ya kujuzidi kimo kwa kujitutumua na kutegemea michango ya watu.

Watu wanne tu Mikadi Beach wanatosha kumaliza harusi.

Wengine wanaweza kuisikia kwenye gazeti.

Gharama hata laki mbiki haifiki.

Ukifanya hivyo utakuwa hujaoa?
 
Huwa sitaki kusikia kabisa kuhusu michango hii. Tangu nikiwa shule miaka hiyo nilijiapiza kua sitachangia mtu hela yangu afanye starehe zake hizo za kuoana sijui na kwenda honeymoon
Sijawahi changa na sitakuja kumchangia yeyote. Mimi nilipoamua kuoa nilifanya kiparty kidogo kilicholingana na uwezo wangu nikawaalika ndugu na jamaa tukala tukanywa na tukafurahi pasipo kumchangisha yeyote
Sitaki na huwa sichangii harusi kabisa

This is a good example....
 
Habari wadau

Katikati na mwishoni mwa miaka ya tisini tulikua tukichangia harusi 5000 unapata single card na 10,000 unapewa bibi na bwana
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi Katikati mwa 2000 tulikua tukichangia harusi 20,000 single na double 30-40 k

Michango ya harusi ikaenda inapanda hivyo hivyo, hadi 2010 ilikua 50-70 single na double ni kuanzia 100 k

Hivi navyoandika 2016 harusi ya jamaa yangu iliyoisha nimechangia 200k, hivyo tunaweza kusema sasa harusi nyingi Michango ni kuanzia 150-200 k na kuendelea
Kwa Hali hii naweza kusema Bila kupepesa macho Michango ya harusi za kileo imechangia kunirudisha nyuma maendeleo yangu binafsi kwa kiasi kikubwa

Mwezi Feb nilichangia harusi 4, each 100,000=
Mwezi huu wa Tatu nimechangia 2 tayari zote zinafanyika wiki hii, moja Thursday na nyingine siku ya pasaka wanabariki ndoa, zile ndoa nyingi zinazofungwa kwa pamoja

Kama mjuavyo koo zetu za wachaga ni kubwa mno, kama ukoo wetu roughly tunaweza kufikia watu 400 tuliopo dar, sasa kwa hali hii unaweza kukuta kila miezi 3 Kuna harusi kwenye ukoo huu, bado harusi za kazini, mtaani na alumni society, nimejaribu kupiga hesabu ya harusi nilizoandika kwenye diary tangu 2006 hadi sasa, jumla kuu niliyopata ningekua na nyumba zingine mbili ambazo ningekua nachukua kodi mbali na hii ninayoishi na familia yangu au ningekua hata na dala dala mbili zinazoleta hesabu

Au, ningeamua kufungua akaunti ya ada za watoto basi watoto wangu wangesoma miaka mingi sana Bila mm kuwazia ada, tofauti na sasa ikifika January ya kila mwaka kichwa kinauma

Naweka azimio, baada ya pasaka sichangii tena harusi, Bahati nzuri watu wangu wa karibu wote yaani tumbo letu tumeshamaliza suala hili , watoto wangu bado ni wadogo wapo primary school, hadi waje wafikie hatua ya harusi sio leo sichangii harusi iwe ndani au nje ya ukoo, sitawatamkia maneno haya bali nitakua nawazungusha tu hadi harusi inapita

Mungu nisaidie niweze kutimiza azimio hili kikamilifu, isiwe kama mara ya mwisho nilipoazimia nikashindwa

Amen
Nimeweka azimio kuwa sichangii,na niliweka kwenye status ya whatsapp nafurah nimeeleweka.
Walioniuliza nimewaambia #MagufuliEffects.
Michango ya Harus No
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha

Unacheka? Ni kweli nachosema.

Watu wanapenda sana kulazimisha mambo na kuishia kuwa kero tu.

Halafu ukikutana na jitu lililo lipumbavu hata u-reason nalo vipi wala halitakuelewa.

Sana sana litaishia kukushangaa wewe ulivyo wa ajabu kwa sababu hutaki kuchangia harusi yake.
 
michango nayo ni jipu...jpm apige marufuku hamna namna...
mkiambiwa changieni madawati mnasikia hakuna pesa...harusi ya kula na kunywa siku moja uko tayari ukope ila usikose...
mimi mwenyewe nshaacha kiaina...uzuri ndugu zangu pia wako against hii makitu...hivyo ni bila bila
 
Heri yangu mimi niliyeacha huo ujinga kitambo, sio kwamba michango inakera tu, hizo ndoa zenyewe siku hizi hazidumu kabisa. Mtu unatoa mchango leo hata mwaka haushi mme/mke full kubanjuka na michepuko. Na ukiwa hujaoa michango ya harusi ni kama deci.
 
Tusiache kufadhiri wengine kwenye jambo hili la kheri na la kishujaa. Mleta mada pole sana ila usiache fanya unapokuwa na nafasi ya kufanya na Mungu atakubariki. Ujue hatukuja na kitu duniani na Mungu ndiye mpaji atuapaye riziki hivyo kugomea jambo la baraka kama hili ni kumkufuru muumba kama hutotoa kwenye harusi utatoa kwingine ambako hutopata baraka na hutothubutu kuja kutuambia hapa. Tufadhilini wanaooa na kuolewa hasa tunapopata nafasi.
Hata mm sichangii haruc kama ww kwanza kadi huwa nakataa ya mchango wa haruc.
 
Yesu alihudhria harusi huko kana na waliopotindikiwa na divai alifanya muujiza kwa kuleta iliyo bora. Kumbuka kuwa suala la sherehe ni la kiutamaduni na kutegemea na daraja la mtu ktk jamii husika hivyo inategemea umezungukwa na watu wenye kipato gani maana alivyonavyo vingi kwake huyo vingi vitatakiwa hii ndio kanuni ya maisha. Wengi humu tunawatoto wadogo sana ngoja wakuwe wafikie kuoa na kuolewa ndio mtajua umuhimu wa kushiriki jambo hili. Na wengi wenu mmevutana hamjafunga Ndoa ndio maana mnapinga jambo hi
Huo ni uwoga na kukwepa maaumuzi, kwani akikataa harusi hataolewa au kuoa?
 
Habari wadau

Katikati na mwishoni mwa miaka ya tisini tulikua tukichangia harusi 5000 unapata single card na 10,000 unapewa bibi na bwana
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi Katikati mwa 2000 tulikua tukichangia harusi 20,000 single na double 30-40 k

Michango ya harusi ikaenda inapanda hivyo hivyo, hadi 2010 ilikua 50-70 single na double ni kuanzia 100 k

Hivi navyoandika 2016 harusi ya jamaa yangu iliyoisha nimechangia 200k, hivyo tunaweza kusema sasa harusi nyingi Michango ni kuanzia 150-200 k na kuendelea
Kwa Hali hii naweza kusema Bila kupepesa macho Michango ya harusi za kileo imechangia kunirudisha nyuma maendeleo yangu binafsi kwa kiasi kikubwa

Mwezi Feb nilichangia harusi 4, each 100,000=
Mwezi huu wa Tatu nimechangia 2 tayari zote zinafanyika wiki hii, moja Thursday na nyingine siku ya pasaka wanabariki ndoa, zile ndoa nyingi zinazofungwa kwa pamoja

Kama mjuavyo koo zetu za wachaga ni kubwa mno, kama ukoo wetu roughly tunaweza kufikia watu 400 tuliopo dar, sasa kwa hali hii unaweza kukuta kila miezi 3 Kuna harusi kwenye ukoo huu, bado harusi za kazini, mtaani na alumni society, nimejaribu kupiga hesabu ya harusi nilizoandika kwenye diary tangu 2006 hadi sasa, jumla kuu niliyopata ningekua na nyumba zingine mbili ambazo ningekua nachukua kodi mbali na hii ninayoishi na familia yangu au ningekua hata na dala dala mbili zinazoleta hesabu

Au, ningeamua kufungua akaunti ya ada za watoto basi watoto wangu wangesoma miaka mingi sana Bila mm kuwazia ada, tofauti na sasa ikifika January ya kila mwaka kichwa kinauma

Naweka azimio, baada ya pasaka sichangii tena harusi, Bahati nzuri watu wangu wa karibu wote yaani tumbo letu tumeshamaliza suala hili , watoto wangu bado ni wadogo wapo primary school, hadi waje wafikie hatua ya harusi sio leo sichangii harusi iwe ndani au nje ya ukoo, sitawatamkia maneno haya bali nitakua nawazungusha tu hadi harusi inapita

Mungu nisaidie niweze kutimiza azimio hili kikamilifu, isiwe kama mara ya mwisho nilipoazimia nikashindwa

Amen
Mimi nilishatoka kuchangia harusi mwaka wa pili sasa,we unakuta ofcn una card kama tatu,mtaani unakoishi una card mbili,kwa ndugu pia.ndani ya mwezi unatakiwa kuchangia harusi kiwango kizima cha mshahara wa mtu,huo ujinga nishauacha siku hz,ila ukija unachangisha pesa ya kuhudumia wajane na yatima nitatoa,lakini lijamaa na mchumba wake wameamua wenyewe kuoana wanataka wanunue na friji kupitia michango yetu wakwendeee...sitaki siku hz hzo mambo
 
ukiendekeza haya mambo ni kero, juzi kuna mama kaja ana sare ya dera na mchango wa kitchen party alishaolewa miaka karibia nane sasa, walifunga ndoa bila sherehe eti leo ndiyo wanafanya harusi,
nimeona ni ujinga kuchangia vitu kama hivi.
 
. Wengi humu tunawatoto wadogo sana ngoja wakuwe wafikie kuoa na kuolewa ndio mtajua umuhimu wa kushiriki jambo hili. Na wengi wenu mmevutana hamjafunga Ndoa ndio maana mnapinga jambo hili.
Wengine hatuna mpango na harusi!
 
Duh hela yote hiyo unatoa mchango?????

Nilishaacha kitambo kuchangia....na ikitokea ni lazima sana kuchanga sizidishi 60,000
 
Back
Top Bottom