bobby dolat
Senior Member
- May 18, 2015
- 167
- 263
Habari wadau
Katikati na mwishoni mwa miaka ya tisini tulikua tukichangia harusi 5000 unapata single card na 10,000 unapewa bibi na bwana
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 hadi Katikati mwa 2000 tulikua tukichangia harusi 20,000 single na double 30-40 k
Michango ya harusi ikaenda inapanda hivyo hivyo, hadi 2010 ilikua 50-70 single na double ni kuanzia 100 k
Hivi navyoandika 2016 harusi ya jamaa yangu iliyoisha nimechangia 200k, hivyo tunaweza kusema sasa harusi nyingi Michango ni kuanzia 150-200 k na kuendelea
Kwa Hali hii naweza kusema Bila kupepesa macho Michango ya harusi za kileo imechangia kunirudisha nyuma maendeleo yangu binafsi kwa kiasi kikubwa
Mwezi Feb nilichangia harusi 4, each 100,000=
Mwezi huu wa Tatu nimechangia 2 tayari zote zinafanyika wiki hii, moja Thursday na nyingine siku ya pasaka wanabariki ndoa, zile ndoa nyingi zinazofungwa kwa pamoja
Kama mjuavyo koo zetu za wachaga ni kubwa mno, kama ukoo wetu roughly tunaweza kufikia watu 400 tuliopo dar, sasa kwa hali hii unaweza kukuta kila miezi 3 Kuna harusi kwenye ukoo huu, bado harusi za kazini, mtaani na alumni society, nimejaribu kupiga hesabu ya harusi nilizoandika kwenye diary tangu 2006 hadi sasa, jumla kuu niliyopata ningekua na nyumba zingine mbili ambazo ningekua nachukua kodi mbali na hii ninayoishi na familia yangu au ningekua hata na dala dala mbili zinazoleta hesabu
Au, ningeamua kufungua akaunti ya ada za watoto basi watoto wangu wangesoma miaka mingi sana Bila mm kuwazia ada, tofauti na sasa ikifika January ya kila mwaka kichwa kinauma
Naweka azimio, baada ya pasaka sichangii tena harusi, Bahati nzuri watu wangu wa karibu wote yaani tumbo letu tumeshamaliza suala hili , watoto wangu bado ni wadogo wapo primary school, hadi waje wafikie hatua ya harusi sio leo sichangii harusi iwe ndani au nje ya ukoo, sitawatamkia maneno haya bali nitakua nawazungusha tu hadi harusi inapita
Mungu nisaidie niweze kutimiza azimio hili kikamilifu, isiwe kama mara ya mwisho nilipoazimia nikashindwa
Amen