Nimesitisha rasmi kuchangia harusi

Harusi ni upuuzi mtupu. Mi kipindi naoa wote niliowachangia walikuwa wananipiga tarehe na awakutoa kitu kabisa. Kuna jamaa yangu nilimchangia 350,000TZS siku naoa hakutoa hata mia akasema hana kitu. Sema nilikuwa nimejipanga nitafanya sherehe ndogo 75% ikatoka mfukoni mwangu baada ya kuona hakuna watu wenye mpango wa kuchangia. nimepiga marufuku kutoa mchango wa harusi.
 
laki moja na mbili ulitoa duh...kweli tupo tofauti kiuchumi...harusi kibaokwnza huwezitoa zote mi sihangaiki natoa napoweza
 
POLE MKUU..WENZIO TULISHASTUKIA HIYO KITU KITAMBO SANA...NACHANGIA HARUSI 3 TU KWA MWAKA NAZO NI KIWANGO CHA TSH LAKI MOJAMOJA...NA HIZI ZINGINE HUWA HATA AHADI SITOI NAWAAMBIA NITATOA NITACHOPATA ILA SITOI PLEDGE NGOOO.
haha wewe unaliwa ...acha zote wewe vipi???????
 
Naombeni muongozo wa kufanya harusi ya gharama ndogo kwa watu wachache wa karibu na familia.kimsingi ambayo utakuwa nikula na kunywa.
 
Tamaduni hubadilika dada yangu utapata anayeamini katika sherehe maana hata za Tamaduni huwa na sherehe ndogo ambayo ndugu pia uchangia.
Tamaduni zinatengenezwa na watu tu na watu wenyewe ndo sisi.

Unfortunately sababu kuu iliniondolea Wazo la harusi ni ndugu ....harusi ni kufurahia kama watu hawakufurahii what for.

Kama mwanaume atataka harusi, he'll most probably be a foreigner so tutafanyia huko huko kwao ambapo ndugu zangu hawapo.
 
kutokuchanga kabisa hapana labda kama una ttz na jamii inayokuzunguka inajua. mm naona ungejiwekea limit ya mwisho kuchangia maana unaonekana fedha unayo. haaa
 
Back
Top Bottom