Nimesikia eti mabomu hufuata simu.

Jayfour

Senior Member
Feb 20, 2011
114
11
Kuna tetesi kuwa bomu linapolipuka hufuata mionzi ya simu na eti inashauriwa kuzima au kutupa mbali mara usikiapo bomu limelipuka karibu.

Hivi karibuni wakazi wa Kitunda waliwalazimisha wenzao kuzima simu zao ili kuepusha mabomu kuja upande wao kufuata mionzi ya simu. Je ni kweli simu iliyowashwa ina effect yo yote na bomu linalolipuka?
 
haha haa mbavu zangu mie, so ukisikia booom.. unatupa kisim chako cha mchina! sion uhusiano wa mionz ya simu na mabom labda wataalam watueleze zaid..
 
Hakuna lolote. Waliotoa uongo huo walisababisha taabu zaidi kwa watu kushindwa kuwasiliana siku ya tukio.
 
Stori za Gomz!....nadharia kibao!..nimeskia na nyingine, bomu halikufuati ukiwa nje ya nyumba!
 
Kuna tetesi kuwa bomu linapolipuka hufuata mionzi ya simu na eti inashauriwa kuzima au kutupa mbali mara usikiapo bomu limelipuka karibu.
Hivi karibuni wakazi wa Kitunda waliwalazimisha wenzao kuzima simu zao ili kuepusha mabomu kuja upande wao kufuata mionzi ya simu. Je ni kweli simu iliyowashwa ina effect yo yote na bomu linalolipuka???????
Siyo kweli, ila kuna watu wanaamini kuwa radi ndo huwa inaweza kufuata mionzi ya simu, hata hivyo hata suala hili bado halijawa 'proven scientific fact'. Ila wakati wa maafa watu wengi hujaribu kutafuta njia ya kuokoa maisha yao na huona kila kitu ni hatari.

Hata hivyo nimesikia kwa mhanga kuwa kweli makombora yalikuwa kama yanafuata watu na hata yalikuwa mengine yanabadili mwelekeo. Kwa kuwa mi si mtaalam naomba nisifanye kukisia ila najua kama ni anti aircraft missile inaweza kuwa heat seeking missile inayofuata joto, lakini si joto la binadamu.
 
Back
Top Bottom