Nimeshuhudia shem akisaliti

Nimeshuhudia shem akisaliti

loyda mdogo wangu....

Naomba unisikilize kidogo tu.

Mwanamume ambaye anaheshimu ndoa yake na kujiheshimu, akiamua kuchepuka atatoka kwa siri kubwa hata shetani hatakaa amuone au ajue. Ila ukiona mwanamume ameamua kutoka nje ya ndoa yake na kufanya wazi wazi, basi huyo yuko kwenye level nyingine kabisa. Yaani huyu keshasema kuwa "liwalo na liwe..."....Umeelewa?

Sasa mtu wa namna hiyo utaanzia wapi kuongea naye? Labda kama unataka kibao kihamie kwako.

Na kama ukiamua kumwambia dada yako, unahakika utampa breaking news? Yaani hajui kila kitu anachofanya mume wake?

Ushauri wangu.... Kwa vile na wewe ni mtu wa club, basi utakuwa ni mdau wa hayo mambo au unaelekea huko (partner or potential partner in crime). Basi jikalie kimya usubiri zamu yako ya kunyoa au kunyolewa.

Hii dunia haiko, haijawahi na wala haitakaa iwe fair...si kwa dada yako tu bali kwa kila mtu!!

Babu DC!!

Nimekuelewa Sana mydia acha niangalie yangu
 
Last edited by a moderator:
mmhhhh kweli kaz ipo,ningekuwa mimi ningemwambia shemeji kitu anachokifanya si kizuri hata kidogo
 
Una uhakika gani kuwa dada yako hajui kama mme wake anatabia ya kuchepuka!
Ina wezekana analijua hilo na amenyuti...Wewe kumueleza inaweza mlazimisha achukue hatua fulani ili asionekane "Boya" kwenu. Kwa maana hiyo. ni wazi wewe ndiyo utakua chanzo cha yote.
Kaa kimya, subiri ndoa yako upambane nayo (katika ndoa kuna mengi zaidi ya haya)
 
Na wewe unamjua dada ako yukoje kama sio mchepuko nae?
 
Pole shoga ila ucjaribu kumwambia ur systr utaharibu ndoa ya w2 bure!
 
That's none of your business. Kua kwanza Uwe na kwako kisha ujipime kama uko na ujasiri wa kumwambia. Inakuuma wewe ndie umeolewa? Ukimwambia dada yako wakaachana unakuwa umepata faida gani? Bado mtoto, kua kwanza uolewe.

Amsubirie tuu hadi sista wake apelekewe ngoma ....halaf aje amwambie 'nilikua namuonaga shemeji akichepuka'....atapata faida hapo!!
 
Ndio maana mnaambiwa msiwe mwaenda hukl club, mie nikuoe afu upeleke vimiguu huko mbona nitavikata
 
ya ngoswe mwachie ngoswe yasije yakawa makubwa kulioko hayo uliyo yaona potezea achana nayo ,, tena ukimwambia dada ako atakuona mshamba kweli unataka kumvunjia mji,, kausha tena kimya nisisikie tena mchepuko saa nyingine hauepukiki utaja ona hata wewe
 
Habari zenu wana MMU,

Mimi nimekuwa nikisoma tu vile mnashauri watu na mimi ni mgeni humu naamini mtanipa ushirikiano.

Jana nilienda club ile tupo na dance nikamuona shemeji yangu yupo na gal mwingine karibu kabisa na nilipokuwa mimi.

Baada ya kuniona aliogopa kabisa mimi nikamsalimia nikafanya kama hakijatokea kitu.

Niliumia kuona yupo anakiss kiss na demu mwingine wakati ana wife Yake!

Nafikiri nimwambie my sister lakini naogopa ntaaribu ndoa yao nafikiri pia nimwambie shem vile sikupenda aache michepuko.

Naomba mnijuze wadau nimweleze my sista?

Mmmmm! Utakuja kuwaharibia,kilicho bora ni kumwita Shem wako umweleze tu na sio sister wako! Tumia Uungwana ktk kutatua hilo!
 
Watu wengine bana! Mimi nilikuwepo kwenye hiyo club. Wewe ndo ulikuwa unakiss na shemejio. Usitake kupoteza maboya ili dadako akijua asikusulubu!
 
Watu wengine bana! Mimi nilikuwepo kwenye hiyo club. Wewe ndo ulikuwa unakiss na shemejio. Usitake kupoteza maboya ili dadako akijua asikusulubu!

Teh teh ulikuwa unakunywa bia gan
 
Habari zenu wana MMU,

Mimi nimekuwa nikisoma tu vile mnashauri watu na mimi ni mgeni humu naamini mtanipa ushirikiano. Jana nilienda club ile tupo na dance nikamuona shemeji yangu yupo na gal mwingine karibu kabisa na nilipokuwa mimi.

Baada ya kuniona aliogopa kabisa mimi nikamsalimia nikafanya kama hakijatokea kitu. Niliumia kuona yupo anakiss na demu mwingine wakati ana wife Yake!

Nafikiri nimwambie my sister lakini naogopa ntaaribu ndoa yao nafikiri pia nimwambie shem vile sikupenda aache michepuko.

Naomba mnijuze wadau nimweleze my sista?

Wewe club ulikuwa na nani..? Hapa lazima uje kuharibu ndoa ya dada yako..! Sio kwa kumsemea shemeji..! hataaaa..! bali kwa kutembea naye..! tena ningekuwa mimi ningeanzia hukohuko ila yeye anavuta subira kwanza...niamini na ukibisha subiri uone kinachokuja..! Pengine alikuwa anakuheshimu ila hali aliyokuona nayo pale club lazima ajenge mtazamo mwingine..! get prepared to be tongozwaring..!
 
Napata hard time sana of course inaniuma pia
akisema umejitongozesha kwake, kakutolea nje sasa unataka kuharibu itakuwaje kwako,,,,mwache dadako ajibebee kapu lake......anapunguza streess za dadako.....kula bata zako jikate......umbea nooo...
 
Back
Top Bottom