Elections 2010 Nimeshinda Kura za maoni Kuipepersuha Bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Wakuu,

Jana tulikuwa na mchakato wa kura za maoni jimboni kwetu. Tulikuwa wagombea wawili katika chama chetu. Nimefanikiwa kushinda kura za maoni kwa kishindo na kumuangausha mpinzani wangu, hivyo kuipeperusha bendera ya CHADEMA katika jimbo hili.

Nimeandika historia kwa kuwa kijana wa kwanza kugombea kwenye jimbo hili tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi kwa vyama vyote vilivyowahi kusimamisha wagombea ubunge kwenye jimbo hili. Ni mtaji kwangu..

Tuko pamoja...Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Tafadhali naomba msiniulize nagombea jimbo gani. Ni jimbo moja la Mkoani, Wilaya yenye jimbo moja.. Zaidi ya hapo usiniulize.

Alunta continua
wewe usituletee uhuni hapa tabia gani hii? au ndo mabosi wako wa Chadema walivyokutuma? unaficha nini Chadema yetu inaingilia na personal interests nathani Mnyika na Slaa wanaona hii
 
Nitaunga mkono mtu yoyote atakayeungana na Dr. Slaa na CHADEMA kuikwamua Tanzania toka hapa ilipogota. Kwa hivyo namtakia ushindi GS.

Hata hivyo nasikitishwa na usiri uliopo hapa. Si kwa GS tu, bali kwa wengi sana. Chimbuko la huu usiri ni WOGA wa kupindukia. Mtaogopa mpaka lini?

Sisi tunaotumia majina yetu waziwazi tumeathirikaje? Mimi Ni Augustine Moshi, mwalimu wa zamani wa UDSM. Sijawahi kabisa kuwaza kujificha hapa au mahali pengine popote. I say what I want, and I let you know that it I who thinks thus.

GS, be open. Mawazo yako na nia zako zitakuwa na uzito zaidi kama utaondoa woga.
 
Natumia jina langu halisi pia. lakini tunajali mawazo zaidi kuliko identity ya mtu
 
Asante sana Ndugu Mbogela kwa maoni mazuri. Nakaubaliana nawe kwamba cha muhimu ni mawazo. I accept, with humility, your correction.

La muhimu tuendelee kuwaunga mkono wale wote watakaojitokeza kupigana kwa ushirikiano na Dr. Slaa. Ila wakijulikana itasaidia.

Go GS, Go! We support you!
 
A great move from a theorists to a practicalist! Safi sana mkuu! We hope u will stay with us hata ukifika huko bungeni. all the best...
 
Natumia jina langu halisi pia. lakini tunajali mawazo zaidi kuliko identity ya mtu

Hii ina apply kwa JF members, ukishatuambia kwamba unavaa kofia ya mgombea ubunge kofia inayo apply inakuwa ya mgombea ubunge.

Huwezi kutaka kuwa public servant kwa usiri siri, public service na usiri haviendani, mtu anayetaka public service anatakiwa kuwa transparent.

Ukishavaa kofia ya ugombea ubunge una chaguzi mbili,

1.ujitaje jina lako na la jimbo lako, essentially ufanye kampeni hata kama ni kwa kujitambulisha tu. Huwezi kusema wewe umeshinda kura ya maoni kugombea ubunge bila kutaja jimbo na jina lako, kwa sababu kauli hii itakuwa haina uzito na haina tofauti na ndoto na hadithi za alinacha, how can anybody take you seriously? Indeed how can anybody verify what you are saying?

2. Usijitaje jina, uwambie watu kwamba una value usiri wako sana kuliko kazi ya kuongoza watu.Na kwa sababu ukisma hivi utajionyesha usivyo na perspective, usivyo na priority, usivyojua sacrifice za uongozi, tayari moja kwa moja utakuwa ume ji disqualify.

If anything kama ulikuwa hutaki kuhusisha maisha yako ya JF kabla ya kampeni ya ubunge na haya ya kampeni, ungeweza kirahisi kabisa kuomba ID nyingine, ambayo ingekutambulisha rasmi kama mgombea ubunge fulani wa jimbo fulani, hapa pasingekuwa na tatizo la ku compromise privacy ya ID yako.

Mimi napata matatizo sana na mtu anayetaka kufanya kampeni huku anaweka usiri,naona kuna woga hapo, hamna uwazi hapo, hakuna uwezo wa maamuzi hapo, hakuna kuelewa kazi ya utumishi wa umma hapo, kila indicator inanionyesha matatizo matupu mbeleni kwa mbunge kama huyu.
 
Hongera ndugu. Kabla hatujafurahi tueleze nguvu ya mpinzani 'wetu' wa ccm tujue upepo wa ushindi uko wapi
 
Hongera ndugu. Kabla hatujafurahi tueleze nguvu ya mpinzani 'wetu' wa ccm tujue upepo wa ushindi uko wapi

Atakuelezaje nguvu wakati anachelea akikutajia details zaidi utamjua yeye ni nani na anagombea jimbo gani? Na yeye msiri hataki ajulikane ?
 
All the best GS, I'm strongly believe u'r going to win !!! Peace out !!!

We need vote for change !!
 
gs come out tukujue ili kampeni zianze mwaka huu hakuna kulalal mpaka kieleweke

Huyu alivyojiweka sasa hivi hata watu wakimpakazia kwamba ana scandal ya rushwa ya uchaguzi na TAKUKURU hawezi hata kujitetea, atajitetea vipi na yeye anaogopa kujulikana ?
 
GS kama unanisikia endelea kujificha hivo hivo usionyeshe identity yako kwanza maana nawajua waswahili badala ya kukusafisha watakuchafua, wanajifanya sasa wanakupenda eti wanataka kukupa ushauri, utakapojionyesha tu utaniambia, kama wanakitu cha zaidi wataku PM.

Cha muhimu wewe nenda ongea na wapiga kura wako kama kuna member mtakutana naye kwenye field jua huyo ndiye supporter halisi sisi wengine ni wapiga domo tu ndugu yangu, jitambulishe uone moto watu wanaweza kukufungia safari waje jimboni kukumaliza believe me or not muulize Mwakalinga a.k.a Mtanzania atakusimulia.

Wanatolea mifano ya Dr. Slaa, Mnyika na Zitto, hawajui hao wamejiunga JF wakiwa tayari public figures. Kama ulivyosema kisisasa wewe bado mchanga komaa kwanza ndipo ujitambulishe hapa, hata kinda la njiwa hufundishwa kuruka kwa kupiga piga mabawa ndani ya kibweta kabla ya kutolewa nje, ila kama litajifanya limeshajua litaachwa litelemke chini ya mti na halitaweza kupanda tena. Take or don't take my opinion.
 
This girl (GS) is not ready for prime time if she's scared to be asked questions.

You can't tell people that you are running for office and at the same time tell them they shouldn't ask you questions. I'm sorry but that's retarded as hell.
 
Nyani Ngabu

kubali umeonyesha weakness vinginevyo nitanzisha thread 'NYANI NGABU AOMBEA MWANA JF MWENZAKE ASHINDWE' ili tujadili kama hapo kuna busara imetumika.

Hivi mtu kuwa mwanaJF ni sababu tosha ya kumuunga mkono kuwa mbunge?unapaswa kufikiri zaidi ya hivi!!
 
This girl (GS) is not ready for prime time if she's scared to be asked questions.

You can't tell people that you are running for office and at the same time tell them they shouldn't ask you questions. I'm sorry but that's retarded as hell.
Lakini tofautisha ofisi za kisiasa na ofisi zingine mbinu tofauti hutumika, kwenye siasa kuna mbinu nyingi hata kujificha nayo ni mbinu tofauti na kuapply kazi ya u recturer lazima uonekane wazi unashusha materials.
 
Napingana kabisa na wewe. Kwenye siasa hususan utumishi wa umma, kujificha ni mbinu mbaya sana. Kumbuka kuwa kwenye siasa perception is reality. Sasa unapojificha na kudhani unatumia mbinu zenye akili wenzako watadhani unajificha kwa sababu una la kuficha (hata kama huna la kuficha). Kwa hiyo perception itajengeka kwamba hujali, u mwoga, huna sera, na ndio maana umejificha na hutaki watu wakuulize maswali. Sasa kwa nini watu wakupe kura mtu mwenyewe ambaye unajificha ficha?

Mgombea yeyote yule aliye makini, anayejiamini na anayejua anachotaka kufanya haogopi maswali. Kwenye nchi za watu wagombea huwaga wana solicit interviews na vyombo vya habari. Sasa huyu mgombea wenu wa Chadema hata jimbo analotaka kugombea hataki kututajia (as if we don't know it)....y'all can't be serious
 
Kikwete naye alipitishwa kirahisi rahisi hivi hivi, amefulia sasa watu wanalaumu.

Hatujifunzi tu !
 
Napingana kabisa na wewe. Kwenye siasa hususan utumishi wa umma, kujificha ni mbinu mbaya sana. Kumbuka kuwa kwenye siasa perception is reality. Sasa unapojificha na kudhani unatumia mbinu zenye akili wenzako watadhani unajificha kwa sababu una la kuficha (hata kama huna la kuficha). Kwa hiyo perception itajengeka kwamba hujali, u mwoga, huna sera, na ndio maana umejificha na hutaki watu wakuulize maswali. Sasa kwa nini watu wakupe kura mtu mwenyewe ambaye unajificha ficha?

Mgombea yeyote yule aliye makini, anayejiamini na anayejua anachotaka kufanya haogopi maswali. Kwenye nchi za watu wagombea huwaga wana solicit interviews na vyombo vya habari. Sasa huyu mgombea wenu wa Chadema hata jimbo analotaka kugombea hataki kututajia (as if we don't know it)....y'all can't be serious
Hujanielewa inategemea unajificha wapi unaweza kujulikana kwenye TV lakini wapigakura wako wasikujue, hata wote JF tukimjua leo tutamsaidia nini, yeye amesema alikuwa jimboni kwa wiki tatu na alifanya hivyo bila wewe kujua.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom