Nimeshawishi watu 7 kumchagua Lowassa. Wewe Je?

Nimeshawishi watu 7 kumchagua Lowassa. Wewe Je?

1. Mama yangu
2.Dada yangu mmoja
3.Binamu zangu wawili
4.Shemeji zangu wawili
5.Muuza duka Jirani

Haikuwa kazi nyepesi.

Sasa wewe watu 7? Sisi ukoo wetu una watu zaidi ya 200 wote niwashawishi kumchagua magufuli, afu kuna family frnds kama 60 nao wako pamoja na magufuli!!!
#hapa kazi tu
 
"Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira". Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia:

Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha "wateule" na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, "kulikoni?". Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya "malofa" wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu:

"Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?"Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza "nyomi" katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia.

Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.

Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni "vijisenti", au "fedha ya mboga", wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa "Wapige mbizi" na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa "Ni heri wale nyasi"…

Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni "wapumbavu,amlofa na mbumbumbu". Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili..

Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.

"ALUTA Continua, Victoria Ascerta".... "The Struggle Continues, Victory is Certain"; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
1. Mama yangu
2.Dada yangu mmoja
3.Binamu zangu wawili
4.Shemeji zangu wawili
5.Muuza duka Jirani

Haikuwa kazi nyepesi.

Mkuu mi nilijiwekea target minimum nipate watu 10 hadi sasaiv ninao 6 bado wanne na hawa nina uhakika watampigia lowassa na wataniletea kithibitisho wakishampigia kura....TWENDE NA LOWASSA 2015
 
Nimefikisha 80 wanaoikataa ccm, 60 watapiga kura kwa ukawa, 5 act, 15 ni washangia ushindi wowote tu hawapigi kura
 
Sasa wewe watu 7? Sisi ukoo wetu una watu zaidi ya 200 wote niwashawishi kumchagua magufuli, afu kuna family frnds kama 60 nao wako pamoja na magufuli!!!
#hapa kazi tu
Hapa naulizia juu ya Lowassa siyo Magufuli. Soma vizuri post yangu mkuu
 
mimi watu mitano nimemaliza nao chuo wote watamchagua lowassa na kila mmoja anaenda kumuelekeza mzazi na familia yake kiujumla juu ya umasikini unaotokana na ccm
 
1. Mama yangu
2.Dada yangu mmoja
3.Binamu zangu wawili
4.Shemeji zangu wawili
5.Muuza duka Jirani

Haikuwa kazi nyepesi.

Siku hizi najiunga na kifurishi cha buku mbili kila siku na mpaka sasa nimewashawishi watu 30 na ninaendelea mpaka siku ya uchaguzi.
 
1. Mama yangu
2.Dada yangu mmoja
3.Binamu zangu wawili
4.Shemeji zangu wawili
5.Muuza duka Jirani

Haikuwa kazi nyepesi
.
Ni kweli ndugu, ni kazi ngumu.Niliowapata mimi walinibishia sana kwamba kura moja haiwezi
kubadili kitu.Ni wazazi 15 wa watoto wa darasa la saba nlokuwa nawapiga tuisheni
ya english na maths.Kilichonisaidia sana ni bei za sukari, unga na mchele zilivyopanda
kuanzia 2005.
 
1. Mama yangu
2.Dada yangu mmoja
3.Binamu zangu wawili
4.Shemeji zangu wawili
5.Muuza duka Jirani

Haikuwa kazi nyepesi.
Lazima uchomwe moto kwa kuwaingiza ndugu zako kuungana na fisadi la shetani.
 
Mimi nimeshawishi wengi kuachana na huyu fisadi Lowasa.
 
Wawili haikuwa Raihisi. Walionipinga kwa nguvu hawakuwa na kadi ya BVR nikahesabu hasara kwa Magufuli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom