Sio rahisi mtu kuchukua begi ambalo hamjui muhusika wake ni nani!
Begi lako itakua lilichukuliwa mwishoni kabisa mwa safari baada ya abiria wote kushuka na begi lako kubaki peke yake,uchunguzi wa Polisi uanzie hapo.
Sawa mkuuJaribu kumbembeleza dereva umwambie utatoe dau kubwa. Dau likiwa kubwa kuliko kitakachopatikana kwa kuuza vilivyomo ndani ya begi anaweza kushawishika. Lakini ujifanye kumwomba afanye uchunguzi na usionyeshe kuwa yeye anahisiwa.
Nuksi huanzia kwenye mambo kama haya
Barabarani wanasema wameona maruweruwe,,,,,,,,,kumbe magundu waliyoyabeba hukoNuksi huanzia kwenye mambo kama haya
Looh, pole sana aisee!Hapana mkuu, sikuwa na mzigo mwingine sema nilikuwa na mawazo sana
Asante mkuu, sina uhakika na hiloKWANZA Pole sana........ ila wewe ni mzembe sana...yaani nna hakika aliyeliiba ameshukia kituo kinachofuata.....pole sana..
Pole sana mkuuUmenikumbusha mbali.
Mwaka 2012 nilipotelewa na begi nikielekea Moro.
Ila haukuwa uzembe wangu mana begi likikuwa kwenye buti mbaya zaidi humo kwenye begi niliweka vyeti vyangu na ndio nilikuwa naenda chuo first year.
Aisee nilichanganyikiwa.
Namshukuru Mungu vyeti nilipata ila begi na nguo sikuambulia chochote.
Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Mkuu nimemtafuta mpaka mmiliki wa Bus hizo lakini mpaka leo bila bila. Ni kama hawataki mmiliki kujui hii ishu. Mtu wa mwisho ambaye ni wakala yuko Dar akasema mmiliki ni mgonjwa hivyo hawezi ongea na simu, nikamwomba anitumid namba nijaribu bahati yangu lakini akakataa na kuishia kusema ni uzembe wanguMtoa mada anasema alipiga namba za kwenye tiketi akakuta wengi washaacha kazi hiyo kampuni Mimi nijuavyo kwenye tiketi hua wanaweka namba za mmiliki wa bus au ofisi kiasi angepiga kwa muhusika begi lake ningepatikana
Pamoja mkuuHapo ni kuendeshwa na hisia dereva hawezi chukua mzigo wa abiria
Acha kabisa mkuu. Nimerudi nyuma sana kimaisha kwa kuipoteza laptop yangu. Ki kweli siko sawa mpaka muda huu. Yaani sitaki kuamini kama kweli ndiyo nimeshaibiwa.Najaribu kuvaa viatu vya huyu Jamaa ndio unaenda mbio roho inadunda kwa presha unafika ndio kwanza unaona Basi limepaki, mapigo ya moyo yanaongezeka unafika unauliza unakuta hakuna kitu...duh. oba isikukute hii situation.
Hapana, haikuwa route rasmiFrester wameanza trip za Dar Moro?