Nimesahau mzigo ndani ya basi

Mkuu ni bahati mbaya, nimesha safiri sana na bus lakini sijawahi kusahau mzigo wangu hata siku moja
Peleleza binafsi usitumie polisi. Toa dau la kurudishiwa laptop yako.

Wanaojua ni kondakta, washusha mizigo na wanaofanya usafi kwenye basi.
 
acha umaskini ndugu yaani kwa uzembe wako uache mzigo alaf uanze kumuhisi dereva na konda ww ni faken nn nyie ndo wale watu nux unaeza singizia mtu kesi ili ulipwémali zako. begi la laptop lina uzito gani usilipakate tena safari ya usiku akili za kifaken sana
 
Ukisoma comments ni kama michango mingi huenda inatolewa na Wadau wa Mabasi, either Madereva au Makondakta n.k.

Sehemu kubwa ya michango ni ya kihuni tu na si ya kumsaidia Muhanga kama alivyotarajia.

Watu mnang'ang'ania kuhoji anasahauje Mzigo kwenye Gari...hebu tuache upumbavu.

Watu mnakimbilia kuwatetea Dereva na Kondakta kwani Yeye amewataja hao?...na kwa nini kusiwe na uwezekano wa wao kuiba hiyo Mizigo pia?.

Watu mnamlaumu kusema kamkuta Dereva na Mwanamke, kwanza huyo Mpuuzi kukaa na Mwanamke ndani ya Basi la Abiria kwenu ni sawa kama nyie sio Wahuni Wenzake?....Na alikataa kutoa ushirikiano mara ya kwanza mpaka Mtu akaenda kuleta Polisi ndio akafunguliwa bado mnaamini huyo dereva ni Mtu wa maana?.

Vipi kama alivyokataa kummfungulia Abiria mara ya kwanza ndio alipata chance ya kwenda kukagua Basi na akaukuta Mzigo tajwa na akaamua kuuiba?.

Dereva huyu ni Muhuni na mnaomtetea ni Wahuni wenzake.
sawa ww ambae sio muhuni tuache wahuni tuendelee kuteteana
 
acha umaskini ndugu yaani kwa uzembe wako uache mzigo alaf uanze kumuhisi dereva na konda ww ni faken nn nyie ndo wale watu nux unaeza singizia mtu kesi ili ulipwémali zako. begi la laptop lina uzito gani usilipakate tena safari ya usiku akili za kifaken sana
Mkuu unaweza toa mchango wako bila matusi na ukaeleweka vizuri tu. Asante mkuu
 
Habari wakuu.

Moja kwa moja kwenye mada, Jumapili iliyopita ya tarehe 05/06/2022 mida kama ya saa 1 usiku kuelekea saa mbili nikiwa natoka Dar kwenda Morogoro ndani ya bus mali ya kampuni ya Frester nikaamua kushukia Chalinze na kusahau begi langu lenye computer na vitu vingine. Nikatafuta usafiri mwingine kwenda Moro ili kufatilia begi langu lakini mpaka nafika Moro nikakuta bus limefika muda mrefu sana na abiria wote wameshashuka na bus limepaki kimya kabisa.

Ikabidi niende ofisini kuulizia maana ilikiwa usiku tayari mida kama ya saa saba. Ofisini sikukuta mtu zaidi ya abiria waliolala wakisubiri kusafiri kesho yake. Narudi nyuma kidogo, ni kuwa baada ya kujua nimesahau begi nilipiga zile namba za simu za kwenye tiketi kama nne ndipo nilipompata muhusika kwani wengi walisema wameshaacha kazi kampuni ile.

Muhusika alipokuja mida kama ya saa kumi tukaenda kwenye bus na kukuta dereva kalala kwenye bus na akajibu kupitia dirishani kuwa hajaona hilo begi. Nikapata wazo la kwenda Polis, nikaja na Polis wa kike na dereva akafungua mlango tukaingia ndani kukagua, kweli hakukuwa na begi ila mkoba tu wa kike uliosahaulika pamoja na demu wa dereva kumbe walilala humo.

Hisia zangu zinaniambia kuwa dereva, demu wake na kondakta ndiyo wamechukua mbegi langu. Naombeni msaada wa kipi cha kufanya kupata begi langu kwani ni muhimu sana na niko tayari kwa njia yoyote ile na kulipa gharama.

Ikumbukwe pia kuwa mzigo wa ndani ni dhamana yako/yangu.
Palepale ulipostuka umesahau begi ungepiga simu ili wautafute na kuhifadhi kabla gari kufika mbali. Mimi nilisahau mzigo basi la BM, nikapiga muda huohuo, wakatafuta wakanipigia wameuona na watahifadhi kesho niendende ofisini, nilipoenda nilipewa kama ulivyo.
 
Back
Top Bottom