Nimesahau mzigo ndani ya basi

Computer/laptop, simu, vitambulisho, kadi za Benki, nk,
Unakuwanavyo bega kwa bega,
i.e, ukikaa viko mapajani, ukiamka viko begani(bila shaka ndani ya begi).
Kamwe usiweke hata ndani ya sanduku. Kama kupotea viwe detached forcebly from your body(unyang'anywe kwa nguvu)
Sawa mkuu
 
Chalinze Kuna kipi kinachoweza kukufanya usahau begi lenye kompyuta?
Wewe unataka kuharibu sifa nzuri za dereva wa Frester.
(Eti ana demu wake na walilala humo humo, unafikiri mke au watoto wa dereva wakisoma huu uongo watafurahi)
Kwa nini useme ni demu wake? Je Kama ni abiria Kama abiria wengine ameomba hifadhi kwa sababu Hana hela ya gesti?
Usipende kuharibu sifa za wengine kwa uchokoraa wako wa kuwahi vipusa vya Chalinze.
Mkuu mimi sisemi uongo kwa sababu haunisaidii kupata mzigo wangu. Ninaposema demu wake ni kwa sababu niliambiwa na mfanyakazi wao niliyemkuta ofisini. Sina sababu ya kusema uongo
 
Kwanini uliposhuka tu chalinze na kugundua umesahau begi hukufanya taratibu ya kuwasiliana na wakala wa frester hapo chalinze akupe mawasiliano ya hilo basi lao lililoelekea Morogoro wakuangalizie begi lako? Pole huna wa kumlaumu ila ww mwenyewe
Ni kweli hana wa kumlaumu lakini kwa nini Jamii msiwalaumu na hao wanaoiba, kwani kuiba ni ushujaa, kwamba kwa kuwa tu Mtu kaacha Mali yake basi una haki ya kujimilikisha?.

Tuwe pia tunawakumbusha Watu wanaochukua visivyo vya kwao kwamba wasitarajie maisha yaliyo na baraka kwa kudhulumu Wengine.
 
Kwenye basi mzigo unaoingia nao ndani ni dhamana yako isipokua ule wa kwenye buti ndio dhamana yao, unashukaje unasahau begi kwenye gari? Kama uliweka kwenye staff carrier kwa nini usijiandae na uandae mzigo ndio ushuke? Imekula kwako
Mkuu ni bahati mbaya, nimesha safiri sana na bus lakini sijawahi kusahau mzigo wangu hata siku moja
 
Najaribu kuvaa viatu vya huyu Jamaa ndio unaenda mbio roho inadunda kwa presha unafika ndio kwanza unaona Basi limepaki, mapigo ya moyo yanaongezeka unafika unauliza unakuta hakuna kitu...duh. oba isikukute hii situation.
 
Hakuna Frester ya Dar Moro mkuu, hakuna kabisa. Tuanzie hapo kwanza.

Ulipanda bus gani?
Mkuu haikuwa route rasmi. Ilikiwa usiku kukaribia saa mbili. Kwa taarifa isiyo rasmi ni kuwa gari ilikuwa inatoka dar garage.
 
Huyo dereva na konda unawaonea tu mwaisa.

Na dereva umemchongea kusema amelala na demu humo.

Sijui ni hasira za laptop. Ukute na wewe ulikuwa na kidemu kikakuchanganya.

Mkuu sina nia ya kumchongea mtu, lengo ni kupata mzigo wangu kwa njia yoyote.
 
Hapana mkuu, nilikuwa na mawazo sana
Watu wengine wanajiandikia chochote bila hata kutafakari. Kusahau inatokea kwa kila mtu na sidhani kama ni ajabu sana. Begi itakuwa shida kulipatav kwa sababu hata kama ni dereva/konda alilipata, anajua kabisa sheria haiwezi kumbana. Hapa ndiyo tunaona umuhimu wa kuwa na kamera kwenye magari ya abiria.
 
Ni kweli hana wa kumlaumu lakini kwa nini Jamii msiwalaumu na hao wanaoiba, kwani kuiba ni ushujaa, kwamba kwa kuwa tu Mtu kaacha Mali yake basi una haki ya kujimilikisha?.

Tuwe pia tunawakumbusha Watu wanaochukua visivyo vya kwao kwamba wasitarajie maisha yaliyo na baraka kwa kudhulumu Wengine.
Kabisa mkuu, ubarikiwe. Siyo sahihi kuwa abiria akisahau mzigo basi ni haki kuibiwa kwa sababu tu mzigo wa ndani siyo dhamana ya kampuni
 
Watu wengine wanajiandikia chochote bila hata kutafakari. Kusahau inatokea kwa kila mtu na sidhani kama ni ajabu sana. Begi itakuwa shida kulipatav kwa sababu hata kama ni dereva/konda alilipata, anajua kabisa sheria haiwezi kumbana. Hapa ndiyo tunaona umuhimu wa kuwa na kamera kwenye magari ya abiria.
Kweli mkuu. Ila nimepata hasara sana. Kwani nina project za watu wengi na wengine walishalipa pesa zao. Sijui hata nasema/nafanya nini.
 
Kweli mkuu. Ila nimepata hasara sana. Kwani nina project za watu wengi na wengine walishalipa pesa zao. Sijui hata nasema/nafanya nini.
Jaribu kumbembeleza dereva umwambie utatoe dau kubwa. Dau likiwa kubwa kuliko kitakachopatikana kwa kuuza vilivyomo ndani ya begi anaweza kushawishika. Lakini ujifanye kumwomba afanye uchunguzi na usionyeshe kuwa yeye anahisiwa.
 
Ukisoma comments ni kama michango mingi huenda inatolewa na Wadau wa Mabasi, either Madereva au Makondakta n.k.

Sehemu kubwa ya michango ni ya kihuni tu na si ya kumsaidia Muhanga kama alivyotarajia.

Watu mnang'ang'ania kuhoji anasahauje Mzigo kwenye Gari...hebu tuache upumbavu.

Watu mnakimbilia kuwatetea Dereva na Kondakta kwani Yeye amewataja hao?...na kwa nini kusiwe na uwezekano wa wao kuiba hiyo Mizigo pia?.

Watu mnamlaumu kusema kamkuta Dereva na Mwanamke, kwanza huyo Mpuuzi kukaa na Mwanamke ndani ya Basi la Abiria kwenu ni sawa kama nyie sio Wahuni Wenzake?....Na alikataa kutoa ushirikiano mara ya kwanza mpaka Mtu akaenda kuleta Polisi ndio akafunguliwa bado mnaamini huyo dereva ni Mtu wa maana?.

Vipi kama alivyokataa kummfungulia Abiria mara ya kwanza ndio alipata chance ya kwenda kukagua Basi na akaukuta Mzigo tajwa na akaamua kuuiba?.

Dereva huyu ni Muhuni na mnaomtetea ni Wahuni wenzake.
 
Kikubwa begi lilishuka kabla yako, waliiwahi laptop.

Hali kama hii usitegemee kupata chochote.

Ripoti polisi upewe ripoti ya kukuwezesha kutengeneza vitambulisho vingine.

Mzigo mmoja na unausahau huo huo kwenye gari.

Pole mwanangu
 
Back
Top Bottom