Nimeporwa begi usiku Kariakoo

Nimeporwa begi usiku Kariakoo

Huu wizi umekubuhu sasa jana usiku pale maeneo ya banora wamempora mama wa watu handbag yake ilikuwa na laki tatu ya vicoba mida ya saa moja usiku mama yule amelia sana nilijisikia vibaya sana. Mwizi alikuwa kwenye pikipiki Angalizo; ukitembea pembeni ya barabara usiweke handbag au pochi au bag upande wa barabara ni hatari zaidi
Tahadhari muhimu mkuu, yan nikizfkilia docmnt zngu muhimu, nakosa kabsa usingizi usiku huu.
 
Ilikuwa Gari aina gani?

Polisi wapo kwenye maandalizi ya uchaguzi ujao na mazoezi ya kuwachapa watakaopinga rasimu ya katiba kwa maandamano.

Wizi hasa mjini umekuwa wa kawaida sana tu,sasa sijui walio nje ya mji hali ipoje.
Bora waalim waongezewe miashara ila sio Polisi.
 
Pole sana mwanasheria....Ukiweza tafuta beg la mgongoni (back pack) ni salama zaidi kwani linaonekana 'casual' hivyo halikaribishi wezi tofauti na haya ya kuweka begani unaonekana umetoka Semina tena una laptop! Kaka yangu almanusra akwapuliwe maeneo ya msimbazi na jamaa wenye 'boxer' bahati nzuri mwizi hakuwa mzoefu nadhani kwan alinguka wakati wa kuvutana na akatokomea gizani
salaam wakuu,
mda huu nikiwa napita maeneo ya kariakoo, karibu na makao makuu ya m-beting, nikiwa nmening'iniza begi langu begani.
Ghafla ikaja gari ndogo mbele yangu, kufumba na kufumbua wakanikwapua begi, nilijitahidi kutoa upinzani lakini bahati mbaya likakatika mikanda na wakafanikiwa kulichukua.
Mbaya zaidi watu walikuwa wanaona lakin hakuna msaada nilioupata.
Hvyo tuwe makini wakuu hasa nyakati za usiku tunapobeba vitu tukiwa tunatembea kwa miguu.
 
Pole sana; mkanda usingekatika kuna uwezekano kwamba ungeburuzwa na pengine kuishia pabaya zaidi hasa iwapo ungeanguka chini;

Wizi wa namna hii umekithiri sana kiasi cha mataifa ya nje kuwapa warning raia zao kupitia tovuti za balozi zao hapa nchini; kwa mfano wanashauri:
*Kuhakikisha kwamba ukitembea barabarani unatembea upande ambao unapishana na gari (usitembee upande ambao magari yanatokea nyuma yako);
*kuhakikisha kwamba mkanda wa begi lako unaning'inia kwenye bega la upande ulio mbali na barabara (usiweke mkoba kwenye bega la upande ambao unapishana na magari); kwa mfano kama unapishana na magari kwa bega la kulia, vaa begi bega la kushoto;
*Kuhakikisha begi lako haulivai across kama vile unafunga mkanda wa gari bali unavaa kwenye bega moja au ikibidi ushike na mkono kama briefcase au ukumbatie kama mtoto mchanga; ukiuvaa across kama mkanda wa gari itakuwa vigumu kuuvua ukiporwa na unaweza ishia kuburuzwa na pengine kugonga kichwa kwenye pavement etc;
*vinginevyo ni kuepuka kabisa kubeba mabegi ya aina hiyo in public kwani lazima utavuta attention, kwani wahalifu wa aina hii constantly wapo kazini;



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Pole sana; mkanda usingekatika kuna uwezekano kwamba ungeburuzwa na pengine kuishia pabaya zaidi hasa iwapo ungeanguka chini; Wizi wa namna hii umekithiri sana kiasi cha mataifa ya nje kuwapa warning raia zao kupitia tovuti za balozi zao hapa nchini; kwa mfano wanashauri: *Kuhakikisha kwamba ukitembea barabarani unatembea upande ambao unapishana na gari (usitembee upande ambao magari yanatokea nyuma yako); *kuhakikisha kwamba mkanda wa begi lako unaning'inia kwenye bega la upande ulio mbali na barabara (usiweke mkoba kwenye bega la upande ambao unapishana na magari); kwa mfano kama unapishana na magari kwa bega la kulia, vaa begi bega la kushoto; *Kuhakikisha begi lako haulivai across kama vile unafunga mkanda wa gari bali unavaa kwenye bega moja au ikibidi ushike na mkono kama briefcase au ukumbatie kama mtoto mchanga; ukiuvaa across kama mkanda wa gari itakuwa vigumu kuuvua ukiporwa na unaweza ishia kuburuzwa na pengine kugonga kichwa kwenye pavement etc; *vinginevyo ni
asante mkuu, tahadhari uisemayo, ni sahihi kabisa, hasa unapokuwa unatembea kwa miguu.
 
Pole sana mkuu na hii pia inatokea kwa waendesha pikipiki. Ninawashauri kuwa makini kama unatembea hakikisha bag lako liko upande wa bega ambao gari wala pikipiki haisogei i.e liwe kushoto au kulia mwako kusikopita chombo cha moto. Jitahidi sana ukumbuke hilo. Wao wana kufanyia timina wakiona bag umening'iniza upande wao na inakuwa rahisi. Wanaiba haraka kama umeme vile.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom