Elections 2010 Nimepiga kura, wewe je?

hatudanganyiki! JAMANI chsms cha mafisadi [ccm] kaeni chonjo maana upepo ni wa kimbunga na ni wa siku moja tu. lakini kishindo cha ni kikubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
icon12.png
 
Unalo sema nikweli nimetoka kituoni kama dakika kumi zilizopita na nilikwenda saa moja kasorobo majina yanao anzia na herufi hayajaandikwa mpaka watu kuanza kubwabwaja ndio waka weka herufi vyema nandipo watu wakawanaja ni foleni gani anatakiwa ajipange ili apige kura kwa kweli bado utaratibu ni mbovu sana NEC hawajajipanga kabisa na tatizo jingine kubwa ni wale walio jiandikisha majuzi hapa majina yao hayapo kabisa na wasimamizi wanawambia eti pigeni simu mtajibiwa ili mjue kama majina yenu yapo wakati huo huo mtendaji wa kata ni mmoja vibanda vya kupigia kura ni vinne ataweza kuhakikije hawa watu kama huyu jina lake lipo na hana ile orodha mpya ya watu wapya waliojiandikisha na kumbukeni huyu mtu hapo alipo ana kitamburisho kipya na kituo alicho jiandikisha ndio hicho alipo kuja kupiga kura na jina ndilo hakuna.

Mama mmoja aliamua kusepa baada ya kupata maelekezo mabovu anambiwa hapa jina lako halipo labda nenda upande wa pili akaenda napo ati hakuna kweli alikutana na maelekezo mabaya na akarudi home. Hii inamaanisha NEC haikutoa semina ya kutosha kwa wasimamiaji wa hilo zoezi la kupiga kura na sidhani kama idadi ya wapiga kura maeneo mengine ita kuwa ni wengi safari hii
 
Kaka tuko pamoja, nimehakikisha ni full suti, diwani mbunge na rais sasa tuone kama watachakachua matokeo

Hahahahaha eti ni full suti, Suruali, kizibao cha ndani na juu ukamalizia na koti babu kubwa naona wengi leo tutapiga full suti, miye tayari tangu saa mbili kasorobo. Hongera sana. :peace::peace::peace:
 
Kusema Ukweli vyama vya upinzani havija jipanga kabisaaaa mawakala ni uduchu i mean ni wachahche kweli

hii imekula kwao kabisa navyoona.
Kwanini naseam hivyo sidhani kama walijua kama kutakuwa na vyumba vi nne kila hema moja kwa hiyo kituo kimmoja unakuta kuna mahema mawili makubwa na vyumba ni vinane sasa inakubidi kila chama kiwe na mawakala wa nane wa kuhakiki anaye piga kura ndie mwenyekitamburisho cha kupigia kura.

Haya kwa mfano hilo jimbo la ukonga lina madarasa 12 means vyumba 12 je hivi vyama vilijua hilo na kuwaanda mawakala mapema??
 
Hata mimi nimeshampa Dk. Slaa kura yangu, nasubiri tu confirmation toka NEC.
 
mm hapa a town tayari nimeshachagua mafiga ma3
Rais= slaa.
Mbunge= lema
Diwani= malley. Tunasubiri ushindi ss.
 
nimeliona jina langu baada ya kuzunguka vituo vitatu kimakosa, sikuwa nimetulia nadhani. Nipo kwenye mstari na uzuri hapa udsm wameweka points kadhaa za kupigia kura kwa hiyo foleni hazikatishi tamaa.
 
Mimi nipo ktk kituo cha Mbagala kizuiani hapa. Foleni ni ndefu na wadau wanaenda kupiga kura huku tukiwa na kumbu kumbu ya swala letu la kulipukiwa mabomu kugeuzwa la kisiasa.
Nipo kwenye foleni bado natamani nipewe karatasi hata mia niwekeke tick kwa shujaa, Dr wa ukweli.
Hivi siruhusiwi kuweka X kwenye picha ya JK?

wacha kabisa..usiweke hiyo kitu utaharibu kura...wanaohesabu watajua aliyeweka hiyo hajui kusoma.....piga risasi moja tu
 
Mimi nipo ktk kituo cha Mbagala kizuiani hapa. Foleni ni ndefu na wadau wanaenda kupiga kura huku tukiwa na kumbu kumbu ya swala letu la kulipukiwa mabomu kugeuzwa la kisiasa.
Nipo kwenye foleni bado natamani nipewe karatasi hata mia niwekeke tick kwa shujaa, Dr wa ukweli.
Hivi siruhusiwi kuweka X kwenye picha ya JK?

Fanya hiviView attachment 15994
 
Nimetoka sasa hivi kupiga kura.
Kura ni siri lakini mimi nimepigia kura wagombea wa vyama vyote vitatu vikuu CHADEMA,CUF NA CCM,mpangilio nilivyotaja haufuati utaratibu wowote.
Pale kituoni watu wengi wa kata yetu nawafahamu kwamba ni CCM.Nikichanganya na mwenendo wa kampeni maeneo mengine nchini na kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao,dalili zote zinaonesha Jakaya Kikwete ndiye raisi anayemalizia awamu ya nne ya uongozi wa juu Tanzania.

Sasa natayarisha barua ya wazi kwa raisi huyu kutoka CCM.Nimeshaweka mezani vifaa vyote vya kuandikia isipokuwa maneno sijayapanga katika paragrafu zake.Kila nikijaribu nakuta sina maneno mengi na barua itakuwa fupi mno,haitopendeza.
Nawaomba wana JF tusaidiane vitu vya kujaza hii barua kwa Kikwete ili akiingia ikulu tu aikute barua yetu inamsubiri mezani kwake.
 
naam hapa kilima hewa tayari tushapiga kura kwa amani na sasa nnaelekea amani kwa wazee pale barazani kupata kahawa na kutafuna kashata nikisubiri habari moja mbili hadi jioni nianze kujipanga kupokea matokeo

mji unazizima kwa ukimya watu wote kama wamepigwa na butwaa

Na hapo kwenye kahawa waulize kama wameshapiga kura.Kama kuna mtu hajapiga mhimize akapige.Tuendelee kuhimiza wengine wakapige kura hata baada ya sisi kufanya hivyo.
 
mimi nipo ktk kituo cha mbagala kizuiani hapa. Foleni ni ndefu na wadau wanaenda kupiga kura huku tukiwa na kumbu kumbu ya swala letu la kulipukiwa mabomu kugeuzwa la kisiasa.
Nipo kwenye foleni bado natamani nipewe karatasi hata mia niwekeke tick kwa shujaa, dr wa ukweli.
hivi siruhusiwi kuweka x kwenye picha ya jk?

taratibu utaharibu kura!
 
Nimetoka sasa hivi kupiga kura.
Kura ni siri lakini mimi nimepigia kura wagombea wa vyama vyote vitatu vikuu CHADEMA,CUF NA CCM,mpangilio nilivyotaja haufuati utaratibu wowote.
Pale kituoni watu wengi wa kata yetu nawafahamu kwamba ni CCM.Nikichanganya na mwenendo wa kampeni maeneo mengine nchini na kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao,dalili zote zinaonesha Jakaya Kikwete ndiye raisi anayemalizia awamu ya nne ya uongozi wa juu Tanzania.

Sasa natayarisha barua ya wazi kwa raisi huyu kutoka CCM.Nimeshaweka mezani vifaa vyote vya kuandikia isipokuwa maneno sijayapanga katika paragrafu zake.Kila nikijaribu nakuta sina maneno mengi na barua itakuwa fupi mno,haitopendeza.
Nawaomba wana JF tusaidiane vitu vya kujaza hii barua kwa Kikwete ili akiingia ikulu tu aikute barua yetu inamsubiri mezani kwake.

IKULU GANI AINGIE TENA? kama ya Magogoni atakuwepo Dr Slaa tayari
 
jamani nimejaribu kuuliza uliza waliopiga kura leo hapa arusha, wote wamechagua mabadiliko. Yaani dk.slaa na chadema. Tunatarajia ushindi wa kishindo.
 
Nimetoka sasa hivi kupiga kura.
Kura ni siri lakini mimi nimepigia kura wagombea wa vyama vyote vitatu vikuu CHADEMA,CUF NA CCM,mpangilio nilivyotaja haufuati utaratibu wowote.
Pale kituoni watu wengi wa kata yetu nawafahamu kwamba ni CCM.Nikichanganya na mwenendo wa kampeni maeneo mengine nchini na kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao,dalili zote zinaonesha Jakaya Kikwete ndiye raisi anayemalizia awamu ya nne ya uongozi wa juu Tanzania.

Sasa natayarisha barua ya wazi kwa raisi huyu kutoka CCM.Nimeshaweka mezani vifaa vyote vya kuandikia isipokuwa maneno sijayapanga katika paragrafu zake.Kila nikijaribu nakuta sina maneno mengi na barua itakuwa fupi mno,haitopendeza.
Nawaomba wana JF tusaidiane vitu vya kujaza hii barua kwa Kikwete ili akiingia ikulu tu aikute barua yetu inamsubiri mezani kwake.
Rais hachaguliwi na KATA yenu, anachaguliwa na Watanzania wote!
Nani aliyekwambia JK anaweza kusogea IKULU, kama atakwenda basi ni kukabidhi ofisi kwa Slaa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom