Kuna kundi limeibuka ghafla wakijifanya kuwa na uchungu sana na CHADEMA kumbe ni wanafiki, moyoni wako CCM. Wakati Magufuli anatangazwa kundi hilo hilo liliibuka na kuwashauri CHADEMA wakomae na ubunge. Ujio wa Lowassa umeonyesha rangi za baadhi ya watu. Sasa ni kama wamechanganyikiwa na kujifanya washauri wa CHADEMA.
Mimi nilikuwa mmoja wa watu niliyempinga Lowassa na kumuita mwizi wakati wa mchakato wa kura za maoni CCM ili asipitishwe sababu kubwa niliona upepo wake ulikumba hata wasiokuwemo. Nilijua wakimpitisha tu wapenda mageuzi tumekwisha kwani upepo wake ungepiga hadi kwenye majimbo ya upinzani, na badala ya kuongezeka yangepungua. Kuna wabunge wengi wa CCM walitegemea sana upepo wa Lowassa uwapitie. Sasa hivi wamechanganyikiwa wanaomba bora wangejitoa CCM mapema kabla kura za maoni CHADEMA hazijafanyika.
Ndugu zangu upepo wa wanasiasa ni mbaya sana kuna wabunge CHADEMA upepo wa Dr.Slaa uliwapitia hadi leo hawaamini kama wapo mjengoni. Lowassa upepo wake ni mbaya sana. Dr.Slaa angemsumbua Dr.Magufuli lakini asingemshinda. Vile vile kwenye UKAWA ujio wa Lowassa umeleta mshikamano zaidi. Ninaamini kuna wana CUF na NCCR wasingeweza kumpigia kura Dr.Slaa zaidi ya wabunge wao. Lakini Lowassa ni kama amekuja kuwaunganisha UKAWA. Zitabebwa kura nyingi sana hapa.
Hawo wasiomtaka Lowassa ni wale waliotaka wapinzani wawe wapinzani milele. Ndio wale utawaskia Urais CCM, Ubunge upinzani. Huo ni unafiki mkubwa. Tunahitaji CCM itoke kabisa. Sasa ujio wa Lowassa ni kama umewachanganya sana wamebaki kujifanya wanakishauri chama kumbe wanafki wakubwa. Lengo kuu la chama ni kushika dola kama kuna upenyo umetokea wa kukupeleka huko utumie ipasavyo. Muda ndio huu ukipita CCM itatawala milele.