Nimependa msimamo wa Dr Slaa

Nimependa msimamo wa Dr Slaa

Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.

ulichoandika ndivyo hata mim ningeandika-nakushukuru sana na nimefurah sana kuona wazalendo wa kweli bado tupo
 
Nafasi ya mgombea urais Chadema imeuzwa kwa mtu binafsi.

Wafuasi walioamini mabadiiko ya kweli wakumbuke kuwa tuliwaonya kuwa Chadema ni Chama cha kilaghai...

Teh. Na full ukaskazini eti? Kesheni mkiomba Mamvi asiingie magogoni vinginevyo mtakunywa maji kwa karai. Hata angepita kupitia magamba bado mngenyooka tu. Yupo upinzani sasa vipi unasemaje?
 
Na every unsuccessful man there's a woman behind it...Lowassa ni politician na hii ni nafasi pekee anaweza kuwa Presd.
 
Kuna kundi limeibuka ghafla wakijifanya kuwa na uchungu sana na CHADEMA kumbe ni wanafiki, moyoni wako CCM. Wakati Magufuli anatangazwa kundi hilo hilo liliibuka na kuwashauri CHADEMA wakomae na ubunge. Ujio wa Lowassa umeonyesha rangi za baadhi ya watu. Sasa ni kama wamechanganyikiwa na kujifanya washauri wa CHADEMA.

Mimi nilikuwa mmoja wa watu niliyempinga Lowassa na kumuita mwizi wakati wa mchakato wa kura za maoni CCM ili asipitishwe sababu kubwa niliona upepo wake ulikumba hata wasiokuwemo. Nilijua wakimpitisha tu wapenda mageuzi tumekwisha kwani upepo wake ungepiga hadi kwenye majimbo ya upinzani, na badala ya kuongezeka yangepungua. Kuna wabunge wengi wa CCM walitegemea sana upepo wa Lowassa uwapitie. Sasa hivi wamechanganyikiwa wanaomba bora wangejitoa CCM mapema kabla kura za maoni CHADEMA hazijafanyika.

Ndugu zangu upepo wa wanasiasa ni mbaya sana kuna wabunge CHADEMA upepo wa Dr.Slaa uliwapitia hadi leo hawaamini kama wapo mjengoni. Lowassa upepo wake ni mbaya sana. Dr.Slaa angemsumbua Dr.Magufuli lakini asingemshinda. Vile vile kwenye UKAWA ujio wa Lowassa umeleta mshikamano zaidi. Ninaamini kuna wana CUF na NCCR wasingeweza kumpigia kura Dr.Slaa zaidi ya wabunge wao. Lakini Lowassa ni kama amekuja kuwaunganisha UKAWA. Zitabebwa kura nyingi sana hapa.

Hawo wasiomtaka Lowassa ni wale waliotaka wapinzani wawe wapinzani milele. Ndio wale utawaskia Urais CCM, Ubunge upinzani. Huo ni unafiki mkubwa. Tunahitaji CCM itoke kabisa. Sasa ujio wa Lowassa ni kama umewachanganya sana wamebaki kujifanya wanakishauri chama kumbe wanafki wakubwa. Lengo kuu la chama ni kushika dola kama kuna upenyo umetokea wa kukupeleka huko utumie ipasavyo. Muda ndio huu ukipita CCM itatawala milele.
Umemaliza yote mkuu, naomba nisitie neno zaidi ya kusema WEWE NI GREAT THINKER!
 
Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.
Mkuu binafsi maumivu niliyonayo nayajua mimi mwenyewe .

Chadema wamenikatisha tamaa ,ccm ndio hivyo sitaki hata kuwasikia. Yaani nipo nambwela mbwela.

Faraja yangu pekee ni kuona Dr.Slaa akigoma jumla kuungana na genge la kina Mbowe na Lipumba .
 
mm nahisi kuna major force behind this ninavyo mfahamu dr slaa sidhani kama anaweza kuwa mgumu namna hii hapa kuna kitu nyuma kama si yeye kutaka kuwa presidential candidate wa ukawa basi kuna nguvu ya kifamilia yake ktk swala hili au kuna ushawishi wa ccm mm cdhani kama ni uchafu tu wa lowassa ndo tatizo hapa nani leo ni msafi ? kama inshu ya lowassa ni kufata chain in command ambayo wengi inawakuta kuanzia makazini kwa order kutoka ngazi za juu watanzania wengi wamechoka na mfumo ccm hivi lowassa angejiunga CUF au NCCR mageuzi dr slaa angewashawishi chadema wajitoe ukawa?
Unamwongelea tu Dr.Slaa, familia yake na ccm sijui Mbowe unamuweka kundi gani.

Huu ni usukule wa hali juu sana kutoona madhaifu ya Mbowe kwa kujivika bomu la ufisadi na kupoteza kabisa misingi ya chama.
 
Pole Dr ntakua na msimamo km wako. Na mollah atawalaani hao wanaotumia chama kwa maslahi yao binafsi
 
mimi naona anapenda madaraka pia. Yeye kama anataka wapinzani wachukue nchi angetumia busara wawe yeye na edo kitu kimoja. Kwani hii chuki yake Slaa inabomoa upinzani. Naona Zitto anachelekea kwani ataenda Act Chama ambacho kichanga zaidi.
 
Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.

Unaamini yeye Dr....ni msafi km Malaika? au alidhani atakuwa mgombea wa KUDUMU pale CDM
 
Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.

Kwani chadema MNA maadili nyie ?
 
mm nahisi kuna major force behind this ninavyo mfahamu dr slaa sidhani kama anaweza kuwa mgumu namna hii hapa kuna kitu nyuma kama si yeye kutaka kuwa presidential candidate wa ukawa basi kuna nguvu ya kifamilia yake ktk swala hili au kuna ushawishi wa ccm mm cdhani kama ni uchafu tu wa lowassa ndo tatizo hapa nani leo ni msafi ? kama inshu ya lowassa ni kufata chain in command ambayo wengi inawakuta kuanzia makazini kwa order kutoka ngazi za juu watanzania wengi wamechoka na mfumo ccm hivi lowassa angejiunga CUF au NCCR mageuzi dr slaa angewashawishi chadema wajitoe ukawa?

Nahii kitu itamuondolea heshima yake kwa wapenda mabadiliko ambayo ameijenga kwa siku nyingi huu sio wakati wakususasusa.....Eti...sababu jamii kubwa inamkubali so what
 
Huo ni msimamo wake. Utafiti umeonyesha kuwa kama Dr. Slaa atasimama na Dr. Magufuli CCM itakuwa mshindi, lakini kama yeyote atasimama na Lowassa basi hakuna wakumshinda. Hapa UKAWA ni kuiondoa CCM na mfumo wake na tupate mabadiliko. Hivi Slaa anataka nini?. Mbona vyeo baada ya ushindi ni nyingi. Yeye atulie UKAWA tutashinda.
 
Ukifatilia sana watu wanaolalamika niwaCCM mnataka kusema CCM wanakipenda sana CDM NO...Dr...tunamuhitaji cz kwenye mapambano yyt UMOJA ni muhimu lkn sasa asitufane wapuuzi Tukamuabudu hii haikubaliki
 
Msimamo uliopo sasa si wake bali ni wa mkewe,Hii ni aibu sana kwa familia za kiafrika.

Una uhakika gani na unachokisema? No research no right to speak.
 
Back
Top Bottom