Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,445
- 40,291
Kama kuna vitu vya kipuuzi, kijinga na kipumbavu basi ni uwepo wa mikakati madhubuti kutoka kambi zote mbili zinazovutana sasa (Mbowe na Lissu) kutengeneza mikakati tofauti tofauti wa kuwarejesha wasaliti wa Chadema (Dr. Slaa, Msigwa, Covid 19).
Upande wa kambi ya Mbowe wao wanatengeneza mkakati wa Covid 19 kurejeshwa ndani ya Chadema, na tayari miongoni mwao wapo busy kumtia moyo na kumpigania Mbowe abakie madarakani, huku baadhi yao wakiungwa mkono na waume zao ambao ni viongozi waandamizi ndani ya Chadema.
Upande wa kambi ya Lissu, wao wako busy kutaka kumrejesha Dr. Slaa na Mchungaji Msigwa. Tayari Dr. Slaa na Mchungaji Msigwa wametangaza rasmi kumuunga mkono na kumpigia kampeni Lissu ashinde uenyekiti wa Chadema. Na kwa nyakati zote, Lissu na wapambe wake wa karibu (wakiongozwa na Lema) wamesema wazi ni muhimu na lazima kwa Dr. Slaa na Mchungaji Msigwa kurejesha ndani ya Chadema ikiwa Lissu atashinda.
Kwa watu wengi wasioelewa ni kuwa, hao wote wanapiganiwa kurejeshwa ndani ya CHADEMA ili wapewe vyeo au ubunge kwa maslahi yao kwanza na sio maslahi ya chama, wanachama au watanzania.
Huenda huu ni miongoni mwa mpango wa kipuuzi, kijinga na kipumbavu zaidi kufanywa na viongozi wa Chadema. Wanachama, wapenzi na wafuasi wa Chadema simameni sasa bila kujali kambi mnazozishabikia kuupinga huu mpango wazi wazi. Chama chenu kina thamani kubwa sana, kina watu wengi wazuri, watiifu na waadilifu ambao wamejitolea jasho na damu ili kukilinda na kukijenga na kwa nyakati mbalimbali harakati hizo zimekwamishwa na hao wasaliti, litakuwa ni jambo la kitaahira mnoo kurejea kuwakumbatia wasaliti.