Nimependa msimamo wa Dr Slaa

Nimependa msimamo wa Dr Slaa

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
2,956
Reaction score
1,115
Kama kuna kosa CHADEMA watalijutia ni kumfanya Lowassa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo.

Chama sasa hakina tofauti na CCM kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama.

Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono CHADEMA wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa.

Pole Dr Slaa lakini Mungu yuko na atatunusuru.
 
...leo hata manungayembe yanajifanya wanachama wa cdm. sisi waandamizi tunaimani na viongozi wetu na tunaimani na rais wetu lowasa, go go go lowasa go push it kitaeleweka tu....
 
Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.
Slaa anasikitisha. Mwanamme wa kweli huwa anakuwa mgumu, hii mambo ya kununa nuna, kuzira zira, kulia lia kama Pinda aachie wanawake
 
Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.
wewe ni gamba acha uongo
 
Kwa akili yako unafikiri Regina amekubali??sio tetesi tu bali msome tu body language anapokua hadharani na Lowassa utajua hakua tayari lakini baada ya mwanaume kuamua hakua na namna nyingine.
 
...leo hata manungayembe yanajifanya wanachama wa cdm. sisi waandamizi tunaimani na viongozi wetu na tunaimani na rais wetu lowasa, go go go lowasa go push it kitaeleweka tu....

Sasa hivi mnatumia nguvu nyingi sana kuwaaminisha watanzania eti Lowassa ni msafi lakini kamwe na hamtaeleweka, itawasumbua sana hii na mtapata shida kubwa sana
 
...leo hata manungayembe yanajifanya wanachama wa cdm. sisi waandamizi tunaimani na viongozi wetu na tunaimani na rais wetu lowasa, go go go lowasa go push it kitaeleweka tu....

Ni kwasababu nyie ni kama "Nyumbu"
 
Nafasi ya mgombea urais Chadema imeuzwa kwa mtu binafsi.

Wafuasi walioamini mabadiiko ya kweli wakumbuke kuwa tuliwaonya kuwa Chadema ni Chama cha kilaghai...
 
Jibu hoja kuhusu maadili acha kushabikia viongozi waliopofushwa na fedha za mafisadi.
 
Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.

Kuna kundi limeibuka ghafla wakijifanya kuwa na uchungu sana na CHADEMA kumbe ni wanafiki, moyoni wako CCM. Wakati Magufuli anatangazwa kundi hilo hilo liliibuka na kuwashauri CHADEMA wakomae na ubunge. Ujio wa Lowassa umeonyesha rangi za baadhi ya watu. Sasa ni kama wamechanganyikiwa na kujifanya washauri wa CHADEMA.

Mimi nilikuwa mmoja wa watu niliyempinga Lowassa na kumuita mwizi wakati wa mchakato wa kura za maoni CCM ili asipitishwe sababu kubwa niliona upepo wake ulikumba hata wasiokuwemo. Nilijua wakimpitisha tu wapenda mageuzi tumekwisha kwani upepo wake ungepiga hadi kwenye majimbo ya upinzani, na badala ya kuongezeka yangepungua. Kuna wabunge wengi wa CCM walitegemea sana upepo wa Lowassa uwapitie. Sasa hivi wamechanganyikiwa wanaomba bora wangejitoa CCM mapema kabla kura za maoni CHADEMA hazijafanyika.

Ndugu zangu upepo wa wanasiasa ni mbaya sana kuna wabunge CHADEMA upepo wa Dr.Slaa uliwapitia hadi leo hawaamini kama wapo mjengoni. Lowassa upepo wake ni mbaya sana. Dr.Slaa angemsumbua Dr.Magufuli lakini asingemshinda. Vile vile kwenye UKAWA ujio wa Lowassa umeleta mshikamano zaidi. Ninaamini kuna wana CUF na NCCR wasingeweza kumpigia kura Dr.Slaa zaidi ya wabunge wao. Lakini Lowassa ni kama amekuja kuwaunganisha UKAWA. Zitabebwa kura nyingi sana hapa.

Hawo wasiomtaka Lowassa ni wale waliotaka wapinzani wawe wapinzani milele. Ndio wale utawaskia Urais CCM, Ubunge upinzani. Huo ni unafiki mkubwa. Tunahitaji CCM itoke kabisa. Sasa ujio wa Lowassa ni kama umewachanganya sana wamebaki kujifanya wanakishauri chama kumbe wanafki wakubwa. Lengo kuu la chama ni kushika dola kama kuna upenyo umetokea wa kukupeleka huko utumie ipasavyo. Muda ndio huu ukipita CCM itatawala milele.
 
mm nahisi kuna major force behind this ninavyo mfahamu dr slaa sidhani kama anaweza kuwa mgumu namna hii hapa kuna kitu nyuma kama si yeye kutaka kuwa presidential candidate wa ukawa basi kuna nguvu ya kifamilia yake ktk swala hili au kuna ushawishi wa ccm mm cdhani kama ni uchafu tu wa lowassa ndo tatizo hapa nani leo ni msafi ? kama inshu ya lowassa ni kufata chain in command ambayo wengi inawakuta kuanzia makazini kwa order kutoka ngazi za juu watanzania wengi wamechoka na mfumo ccm hivi lowassa angejiunga CUF au NCCR mageuzi dr slaa angewashawishi chadema wajitoe ukawa?
 
Kama kuna kosa chadema watalijutia ni kumfanya lowasa mgombea wao wa urais. Maadili tuliyosimamia tumeyatupa chooni na kuwakatisha tamaa wanachama na wadau wengi mimi nikiwemo. Chama sasa hakina tofauti na ccm kwa uchafu na sasa imedhihirika kuwa ni Dr Slaa tu ndiye aliyeamini katika uadilifu ndani ya chama. Viongozi wengine kumbe wako kimslahi zaidi na hawakumbuki wahanga waliouawa na kuumizwa na polisi kwa kuunga mkono chadema wakiamini ni mkombozi wao. Sasa kimepokea wale mafisadi papa ambao hata chama chao hakiwataki! Tumekata tamaa. Pole Dr Slaa lkn Mungu yuko na atatunusuru.

Mkuu acha porojo.
Huyo Slaa kama analo dai la haki dhidi ya Lowassa tunaomba alifikishe kwene vyombo vya dola.

Enzi za kuongea kwa hisia zimepita,

Hata yeye anatuhumiwa kuiba "kujikopesha pesa za chama" na hawahawa wanaomtetea leo. je hilio tuliamini?
 
Tujulishe huo msimamo wa dr. Slaa ni upi na aliutolea wapi kwa chanzo kipi?
 
Back
Top Bottom