Nimepata Msiba WanaJF

Ndugu wana JF leo mchana nimepata msiba wa Babu yangu Mzaa Mama. Huu msiba mzito sana kwangu kutokana na maisha niliyoishi. Kwa wale ambao hawakukulia kwa Baba na Mama wanajua role ya Babu na Bibi nami ndio inayonifanya niomboleze sana. Kwa kifupi alikuwa ni Baba mzazi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe milele. Amen

Ndugu Sipo Pole Sana kwa kufiwa na Babu yako Mungu amlaze pema peponi amen. Lakini babu alikuwa na Umri gani? na wewe mwenzetu mtu wa wapi?Babu yako inaonyesha amekula Chumvi nyingi sanaa sisi wengine hatuma Baba wala Mama wala mjomba tupo hivi hivi wote wameshatangulia akhera pole sana Mkuu Sipo Mungu akupe subira Amen.
 
Ndugu wana JF leo mchana nimepata msiba wa Babu yangu Mzaa Mama. Huu msiba mzito sana kwangu kutokana na maisha niliyoishi. Kwa wale ambao hawakukulia kwa Baba na Mama wanajua role ya Babu na Bibi nami ndio inayonifanya niomboleze sana. Kwa kifupi alikuwa ni Baba mzazi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe milele. Amen

Pole sana mkubwa, I know how it pains!
Mungu akujaalie nguvu uweze kuhimili machungu.
 
pole sana mkuu,na mungu akutangulie na akutie nguvu,msiba wapi kaka?
 
Pole sana Sipo,tunakuombea Mwenyezi Mungu akupe kheri na ujasiri wa kukabiliana na msiba huo mzito kwako. Bwana ametoa na bwana ametwaa.

Loved ones never die, but rest in the Lord. Amen
 
POle sana Mkuu Sipo. Mungu awape moyo wa uvumilivu wakati mtakapokuwa mnaomboleza msiba huu mkubwa na aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi
 
Pole sana mkuu, ndio kazi ya Mungu. Usijali huyo anaenda mahala pema peponi amen/amin.
 
Mkuu Sipo, pole sana kwa kupoteza Baba Mzaa Mama. Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Pole sana Mkuu.
 
Pole sana sipo kwa kupotelewa na Babu yako. Mungu akupe nguvu katika wakati huu mgumu.
 
Pole sana Sipo katika kipindi hichi kigumu cha kuondokewa na babu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
RIP Babu.
 
nawashukuru sana ndugu na rafiki zangu hapa JF. Ndo tunamaliza kikao cha familia hapa kwa safari ya Arusha kesho. Msiba utakuwa Arusha ndo nyumbani. Asanteni sana
 
nawashukuru sana ndugu na rafiki zangu hapa JF. Ndo tunamaliza kikao cha familia hapa kwa safari ya Arusha kesho. Msiba utakuwa Arusha ndo nyumbani. Asanteni sana

Mungu awatangulie na awalinde katika safari yenu ya kuelekea Arusha.
Amen.
 
Pole sana ndugu, wewe ulimpenda babu yako lakini Mungu alimpenda zaidi! BWANA alitoa na BWANA ametwaa, Jina lake libarikiwe! Amen!
 
Pole sana Sipo.Mungu aiweke roho ya marehemu babu yako mahalai pema peponi.Amina
 
Pole sana Sipo.
Jipe moyo kwani madhila wameumbiwa binadamu, tunakuombea salama katika msafara wako uwe salama, na katika masuala ya familia busara ikutangulie kwani kwenye matatizo busara hutatizika.

Pole sana.
 
Pole sana ndugu yangu...mungu akutie nguvu
bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe
 
Pole Mzee! bwana alimleta, tena amemhitaji amemtwaa, nasi hatuna budi kusema AMEN na jina la bwana lihimidiwe. RIP BABU YETU MPENDWA.
 
Back
Top Bottom