Nimepata Msiba WanaJF

Mkuu sipo pole sana kwa msiba. Msiba uko wapi? Tupo pamoja kwa sala katika kipindi hichi kigumu, naamini Mungu atakupa nguvu na Hekima ya kumaliza salama.
 
pole sana, jipe moyo ukamilishe shughuli za msiba na uwe jasiri ili kuendelea na maisha, kila mmoja wetu anayo siku yake, hivyo hiyo ndo njia yetu sote.
 
Pole sana kwa kufiwa na babu, mungu akupe nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu. Hasa ukizingatia wote tupo safarini ila yeye ametutangulia.

Msiba upo wapi?
 
Dah pole sana mkuu Sipo kwa kipindi hiki kigumu. Tupo pamoja mkuu.
R.I.P babu wa Sipo
 
Pole sana mkuu, Mungu akupe nguvu hekima na busara ili uweze kuomboleza na baadae kusahau kwani ukizidi kuendelea kukumbuka hautapata nguvu ya kufanya lolote tena. Tuko pamoja mkuu japo sio kimwili bali kiroho tupo pamoja.
 
my condolosence sipo (aka alibi), mbele yake nyuma yetu
 
Nawashukuru WanaJF kwa sapoti mnayonipa ukweli napata faraja kubwa. Asanteni
 
Back
Top Bottom