Huyu Mke ni mwema sana.. Jaribuni kumshauri vizuri....
Unayo shida ya mume kwakua u mpweke mda mrefu.... Hii hoja sio nzuri haitakusaidia kupata mume mwema,.. Ndio iliyokutambulisha kuwa wewe umekua dhaifu na uko nyang'anyang'a kwake..... Tambua kwamba baadhi ya wapenzi wengi hawawezi kulipa upendo palipo na upendo bali hujengeka kiburi....
Anza kumpelekea majukumu apaswayo akufanyie kumkumbusha majukumu yake Kama mwanaume, ili uanze kupima uwajibikaji wake akiwa baba wa familia......
Kumjengea tabia ya kumpa pesa na kumdekeza ni kujizika mwenyewe ktk kumpata mume bora wa familia... Kwani mwanaume anayejitambua, hufurahia Maisha yake katika kupambana na kuipigania familia yake pale inapokabiliana na tatizo ktk familia, na Mimi faraja anapokuwa mshindi...
Uchumba wenu ni wa mda mfupi mno,.. Hayo ni machache mno uliyoyafahamu kwake.. Mko bado mbali mbali....
Mwanamke haombagi kuolewa, ni kosa kubwa kumshawishi mume akuoe... Huna haraka kuhusu jambo la ndoa.... Leo unayo nafasi ya kuamua na bado hauna kizuizi, lakini mambo haya yakishakukuta kwenye ndoa hauna pa kuchomokea....
Mwisho; Naomba uendelee kubaki ulivyo,. Mume wako yu njiani, utadeka na utadekezwa... Huyo mume atakuendesha tu.