Nimepata Mpenzi ila mh..! Ushauri wenu wakuu

Nimepata Mpenzi ila mh..! Ushauri wenu wakuu

Huyo ni mkweli kabisa. Vitega uchumi vingi, kimojawapo ni wewe. Maana kumbuka kitega uchumi kazi yake ni kuzalisha/kukuza uchumi/mtaji na sio vinginevyo
atafute kitega uchumi kwingine aisee
 
Toka muanzane amekufanyia nini cha maana? achana nae
 
Rudisha hio Mbuzi bandani!!!!!!

Chagua mbusi ingine dada, Wanaume wamejaa Tafuta mwanaume aliestaarabika, Muombe Mungu akuletee mwanaume mwema,hata kama sio mume mwema,awe mwanaume mwema tu,kuliko hio Mbuzi Ngoja upate bwana anaeleweka.

Narudia tena; Rudisha hio Mbuzi bandani


Ahaa kwahiyo nyie mkitupiga sie vizinga it means kuwa ninyi sio wanawake wema princess ariana
 
Baada ya kupona maumivu ya kuachana na mpenzi ambaye nilitegemea atakua mume wangu, Mungu si athumani nikakutana na kaka mmoja ambae tulijikuta tunaanzisha mahusiano. Kaka huyu anafanya kazi Mkoa mwingine, ila huku nilipo mimi ndio kwao. kipindi nilipokutana nae alikua kaja likizo hivyo baada ya likizo yake kuisha tuliagana vizuri na mawasiliano yaliendelea vizuri tu, akiniahidi mwezi wa tisa ataleta barua ya uchumba nyumbani, na Mungu akipenda basi mwakani tutafunga ndoa.

Wiki mbili baada ya kuondoka, kuna siku alinitumia sms kwamba kuna kiwanja kinauzwa huko anapoishi, nimkopeshe kiasi fulani cha pesa ili akinunue, nilishtuka maana hatuna zaidi ya miezi mitatu toka tumeanza mahusiano. Sikumjibu vibaya nilimwambia kwa sasa sina pesa akakubali kwa shingo upande. Mawasiliano yakaendelea japo sio kivilee kama mwanzoni,

Leo tena nimepokea sms akidai ana shida na laki mbili, hata kama sina basi nijitahidi hata nimkopee kwa mtu atarudisha mwisho wa mwezi huu. Ni kweli nilishaanza kumpenda, ukizingatia nimekua mpweke kwa muda mrefu. Ushauri wenu wakuu huyu kweli ana mapenzi na mimi au anataka kunitapeli then asepe????
HAHA...
 
Rudisha hio Mbuzi bandani!!!!!!

Chagua mbusi ingine dada, Wanaume wamejaa Tafuta mwanaume aliestaarabika, Muombe Mungu akuletee mwanaume mwema,hata kama sio mume mwema,awe mwanaume mwema tu,kuliko hio Mbuzi Ngoja upate bwana anaeleweka.

Narudia tena; Rudisha hio Mbuzi bandani

Wanaumea tuna kazi mweeee
 
Hata hivyo ni ngumu kusema kuwa umempa,
Pia kwa uzoefu mdogo niliyonawo wanawake wengi wenu huwa rahisi sana kuingia katika mausiano kirahisi mkiwa na stress.
alidai hana haraka ya papuchi mpaka atakapoanza process za kunioa, nadhani ilikua mbinu mojawapo ya kutaka kunitapeli
 
atafute kitega uchumi kwingine aisee
Nakuapia, huwezi kumuacha kirahisi hivyo. Wanawake bwana!!! Na akishakumega ndio kabisaaaaa!! Hata boxer utamnunulia tu, hapo alipo (kwasasa likizo imekaribia) atakua anakesha kuangalia porn ili akariri mautundu na lazima kuna watoto wanaumia kwa kugeuzwa kua field materials ili tu akikukamata uchanganyikiwe. Usikute mmoja wa rafiki zako ni mtu wake wa karibu so anakupeleleza unapenda nn
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom