yingamale
JF-Expert Member
- Jan 5, 2017
- 223
- 222
Baada ya kupona maumivu ya kuachana na mpenzi ambaye nilitegemea atakua mume wangu, Mungu si athumani nikakutana na kaka mmoja ambae tulijikuta tunaanzisha mahusiano. Kaka huyu anafanya kazi Mkoa mwingine, ila huku nilipo mimi ndio kwao. kipindi nilipokutana nae alikua kaja likizo hivyo baada ya likizo yake kuisha tuliagana vizuri na mawasiliano yaliendelea vizuri tu, akiniahidi mwezi wa tisa ataleta barua ya uchumba nyumbani, na Mungu akipenda basi mwakani tutafunga ndoa.
Wiki mbili baada ya kuondoka, kuna siku alinitumia sms kwamba kuna kiwanja kinauzwa huko anapoishi, nimkopeshe kiasi fulani cha pesa ili akinunue, nilishtuka maana hatuna zaidi ya miezi mitatu toka tumeanza mahusiano. Sikumjibu vibaya nilimwambia kwa sasa sina pesa akakubali kwa shingo upande. Mawasiliano yakaendelea japo sio kivilee kama mwanzoni,
Leo tena nimepokea sms akidai ana shida na laki mbili, hata kama sina basi nijitahidi hata nimkopee kwa mtu atarudisha mwisho wa mwezi huu. Ni kweli nilishaanza kumpenda, ukizingatia nimekua mpweke kwa muda mrefu. Ushauri wenu wakuu huyu kweli ana mapenzi na mimi au anataka kunitapeli then asepe????