Nimepata Baby Boy

Nimepata Baby Boy

Mkuu Kimox Kimokole na familia yako hongereni sana kwa baby boy. Kwa sisi watumishi hatutaacha hiii habari iende kimya kimya.Tafadhari soma vifungu vifuatavo viendelee kukufundisha na kukuelimisha kuhusiana na bibilia inasemaje kwa habari ya watoto wetu wadogo.

Imeandikwa katika Mithali 22:6 "Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee." Mungu anatarajia nini kutoka kwa wazazi wanapo wakuza watoto wao Imeandikwa Kumbukumbu la Torati 6:6-7. "Na maneno haya ninayokuamuru leo yata kuwa katika moyo wako nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii nakuyanena uketipo katika nyumba yako na utembeapo njiani na ulalapo na uondokapo."

Mungu anawatazamia wazazi wawe wavumilivu. Imeandikwa katika Wakolosai 3:21 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa."

Nidhamu ni namna yakuonyesha upendo kwa mtoto. Imeandikwa katika Mithali 13:24 "Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; bali ampendaye humrudi mapema."
Nidhamu njema humfunza mtoto imeandikwa Mithali 29:15 "Fimbo na maonyo hutia hekima bali mwana aliyeachiliwa humuaibisha mamaye."

Sababu ya kumwathibu mtoto nikumfanya akuwe vema. Imeandikwa Waefeso 6:4 "Nanyi akina baba msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana."

Thats why I like JF!
 
"NSALA" kisukuma, kwa kidhungu wanamwita "an inteligent person" kiswahili "mtu mwerevu, busara, hekima na akili nyingi" awe hivyo daima
 
Preta umemfananisha kwenye avatar? Ahahahahahaaa
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana.
Mungu ampe afya njema daima! Awajalie pia wewe na mama yake wingi wa busara, hekima na upendo katika kumlea.
 
Last edited by a moderator:
Nitashukuru sana sweetlady hatua hii ni ngumu maombi yenu muhimu
Yeah! Ni ngumu kweli dearest, usijali manake Mungu wetu ni mwema na hakika ataenda kukuvusha salama manake huwa hamtupi mja wake!

Nakuombea sana The secretary!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom