Nimeota

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Baada ya kuamka nimetetemeka sana.

Nilikua namsikiliza mkuu uzinduzi wa flyover hapa ubungo , ameanza kwa salaam kwa viongozi alipo mfikia mkuu wa mkoa akaongea kwa vijembe eti kuna watu nasikia hawakutaki hapa dar, nakuhakikishia wao ndio wataondoka.

Akaendelea , Nashangaa haya mambo yanatokea IGP, upo, RPC upo, Waziri wa mambo ya ndani upo, lakini mnaacha mkuu wa mkoa anahangaika pekee yake.

Natoa agizo, IGP ongeza ulinzi kwa mkuu wa mkuuu, pia Tanroad sitaki kuona ile takataka pale , maana tumemsaidia afanyie ibada lakini yeye amefanya kijiwe cha kusambaza maneno juu ya viongozi.

Baada ya hapo niseme, mkuu wa mkoa ataendelea kama mwimbaji yule nampenda sana " acha maneno weka muziki" oohh wananchi wakarukia "acha meneno weka vyeti", fafafaa, zungusha mayai kama bashite,fafaa, wakaendelea kuimba hadi ikawa vurugu, ndio namka hata sijielewi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom